Blunder ya wabunge wa EALA ni kiashiria cha 'Political immaturity' ya CHADEMA

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,902
Bila kupepesa kope, Chadema bado hakijakua kisiasa kutosha kuweza kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili.

Tumekuwa tukilisema hili, lakini party fanatics wamekuwa wakitupinga kwa kila hoja hata vioja mradi wasikie amani tu.

Sasa uhalisia umeamua kuwa muamuzi wa kauli zetu na kuiumbua Chadema mchana kweupe.

Kitendo cha Chadema kuvurunda katika teuzi zake za wabunge wa EALA, ni ushahidi mwingine tosha kwamba bado Chadema haina uwezo kuliongoza Taifa letu.

Ni jambo la aibu na la ajabu sana, Chama kikubwa kama Chadema, kushindwa kuteua watu sahihi wawili tu kukiwakilisha.

Kosa hili linaweza onekana dogo ila ni kubwa sana kwa mtu yeyote makini! Kosa hili linafuta tuhuma zozote zile zilizowahi kutolewa na Chadema kwa uwezo wa CCM kuongoza. Asiyeweza kuteua hata watu wawili atasema nini mbele ya Chama zoefu kama CCM.
 
CHADEMA hawakuteua wawakirishi. Nakumbuka Mbowe aliwapa wajumbe watu anahitaji yeye akakimbilia Tanga kwenye uchaguzi wa kanda ya Kaskazini. Huko nako akakuta Ndesapesa amemkalia shingoni akaishia kuahirisha uchaguzi na Kuvunja Uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Mhenza.

Hii ni tatizo la chama kuongozwa na mtu aliyefikia mwisho wa kufikiri kama Mbowe.

Tunaomba wanachama wenzangu huyu jamaa asikatishe uchaguzi ujao.
 
Ni kwenye mambo ya kiimani tu ambapo aliyesoma anakubali kuongonzwa na hasiyesoma lakini leo CHADEMA wamekubali zero ya form six kugeuza chama chao kutoka chama cha siasa mpaka kuwa NGO
binafsi ambayo mwenyekiti anaweza kufanya maamuzi nyumbani kwake wanachama wakatumika kama rubber stamp
 
Sawa lakini vyeti kwanza, na ccm mwache kukumbatia watu wasio na vyeti ni aibu jamani.

Bastola ya nini tena!?

Tume huru idaiwe mapema Tanzania
 
Ni kwenye mambo ya kiimani tu ambapo aliyesoma anakubali kuongonzwa na hasiyesoma lakini leo CHADEMA wamekubali zero ya form six kugeuza chama chao kutoka chama cha siasa mpaka kuwa NGO
binafsi ambayo mwenyekiti anaweza kufanya maamuzi nyumbani kwake wanachama wakatumika kama rubber stamp
Mbona mkoa wa Dar e Salaam unaongozwa na Daudi Bashite. Ulizia kama alikanyaga hata hiyo form six. Bashite zero kapatia right away standard four na kakoleza zaidi form four. Au kwa upande wenu ni manukato
 
Ni jambo la ajabu utetezi wa makosa yako unachukua reference ya ujinga wa Jirani yako kama utetezi wako
 
toka 2015 hiki sio chama tena.. ni genge tu la walevi ambao wakishapata viroba vyao vya kutosha ratiba inakua ni kufanya vioja then kuporomosha matusi kwa yeyote atakae wapinga..
 
hivi kwa mfano bashite akisema mbowe akitoa cheti cha six na yeye anatoa vya kwake,hivi mbowe atakubali kweli?
 
kama blunder ni kiashiria cha political immaturity je pale JPM alipokwenda kinyume na kanuni kwa kuzidisha idadi ya wabunge wanaume wa kuteuliwa kwa kuwateua wabunge 6 badala ya watano ile nayo utaitaje? hadi ikalazimu ili kuwapunguza ampe mmoja ubalozi wa nchi ya nje.
makosa yakifanyika yanarekebishwa na siasa zinaendelea.period.
 
Bila kupepesa kope, Chadema bado hakijakua kisiasa kutosha kuweza kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili.

Tumekuwa tukilisema hili, lakini party fanatics wamekuwa wakitupinga kwa kila hoja hata vioja mradi wasikie amani tu.

Sasa uhalisia umeamua kuwa muamuzi wa kauli zetu na kuiumbua Chadema mchana kweupe.

Kitendo cha Chadema kuvurunda katika teuzi zake za wabunge wa EALA, ni ushahidi mwingine tosha kwamba bado Chadema haina uwezo kuliongoza Taifa letu.

Ni jambo la aibu na la ajabu sana, Chama kikubwa kama Chadema, kushindwa kuteua watu sahihi wawili tu kukiwakilisha.

Kosa hili linaweza onekana dogo ila ni kubwa sana kwa mtu yeyote makini! Kosa hili linafuta tuhuma zozote zile zilizowahi kutolewa na Chadema kwa uwezo wa CCM kuongoza. Asiyeweza kuteua hata watu wawili atasema nini mbele ya Chama zoefu kama CCM.

Vipi kuhusu CUF yenye nafasi moja tu lakini bado ccm inataka gender balance?Ni vizuri kusimamia usawa wa kijinsia,lakini tusiishie kuijadili chadema pekee,turudi nyuma na kuijadili blunder ya mkuu wa nchi aliyeteua wanaume 6 kinyume na katiba kuwa wabunge,hadi akapelekea kumlazimisha mmoja ajitoe kafala.

Kwa hoja yako kuwa chadema haijakomaa kuongoza nchi eti kwa sababu imeshindwa kubalance gender,vipi kuhusu yule aliyeteua wanaume 6,yeye bado anafaa kuwa kiongozi wetu?Nafikiri kwa maneno,maamuzi na matendo yake naye hafai kabisa hata kuitwa kiranja wa darasa kama ambavyo chadema haifai kabisa kuongoza nchi.

Nawapongeza waliosimamia gender balance,rai yangu wasiishie kwa Chadema tu,wafike mbali na kuihoji serikali kwa nini mkuu alikurupuka na kuteua wabunge 6 kinyume na utaratibu?Je,kitendo cha kumtoa Mh.Posi bungeni hakikuwa ni unyanyapaa ikizingatiwa mh.Posi alikuwa muwakilishi wa kundi maalumu la walemavu?Nani aliteuliwa kuziba nafasi yake ya uwakilishi wa kundi hilo?

Tushirikiane kulirudisha Taifa letu kwenye mstari bila kujali ni nani aliyepotoka,tukifanya hivyo tutakuwa tumelisaidia Taifa letu katika msingi wa kuheshimu sheria na taratibu tulizojiwekea.
 
Namna ya upatikanaji wa viongozi ndani ya CHADEMA ni madudu matupu.
Hapa ndipo Mbowe alipotufikisha huku akiungwa mkono kwa kila kioja na fanatics wake.
 
Back
Top Bottom