BLUE SCREEN OF DEATH a.k.a windows stop error!

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,277
Watu weng wemakuwa wakisumbuliwa na tatizo hili bila kujua ni kiti gani hiki na ni jinsi gani ya kulitatuwa. Mtu yeyote anayetumia Microsoft Windows (iwe XP vista au seven) anaweza kukutana au pengine alishakutana na tatizo hili. Heri yao wale waliowahi kutana nalo na wakajua nini cha kufanya ila kwa wale ambao waliwahi kutana nalo na hawakujua nini wafanye au hata wale ambao hamjawahi kutana na tatizo hili (naamini ipo siku litakukumba) basi si vibaya tukapeana somo hili. Hili ni tatizo la kawaida kabisa ambalo hutokea mara nyingi pale Windows senses a software, hardware, or driver error preventing it from operating properly. Hivyo basi, almost anything from a minor glitch to a major system malfunction inaweza leta hii kitu. Mara chache sana tatizo hili linaweza kuondoka kwa kufanya simple normal restart tu ya pc yako na ukaona mambo yakawa shwaaari na Blue screen isirudi tena ILA kaa ukijua ii ni dalili mbaya ya tatizo moja kubwa baya sana linalokujia. Sasa ukitaka kujua TIBA hasa ya tatizo hili ni nini hakuna ajuaye sababu inahitai mtu afanye diagnosis ya kina kujua nini hasa tatizo la pc yako.

BLUE SCREEN OF DEATH (BSOD) ni nini?
Sasa basi kabla ya kujua ni jinsi gani ya kutibu embu tujue ni nini hasa hii BLUE SCREEN OF DEATH...Simple. blue screen ni error message ambayo hutokea pale tu system inapotambua tatizo lolote lile litakalosababisha kuifanya system ishindwe kuendelea na kazi zake kama kawaida kwa namna yoyote ile. Hapo ndipo system inaposimamisha shughuliii zooooote kwa pamoja na kukupa ujumbe huo kuwa system imejizima ili kuokoa pc yako isiharibike kutokana na tatizo lililotokea na ujumbe huu huwa unakuja ukiwa kwenye screen ya rangi ya BLUE (ndo maana ya BLUE SCREEN) ingawa maandishi yenyewe huwa meupe..na mara nyingi Windows Xp huwa inaleta na numbered error code ambayo inaelezea tatizo hasa nini ambayo ukiitafuta maana ya code hiyo (online) unaweza jua tatizo ni nini! Kwa windows zingine sijachunguza kwa kina kama mara zote huleta numbered code kama kwenye XP...ila ni vyema ku note down hiyo error pale linapotokea tatizo hili ili ufanye uchunguzi zaidi (ingawa ni vyema ku note kila error unayoipata pale linapotokea tatizo ili upate ufumbuzi wa kina maana mtu mwingine anaona message ya error imetokea hasomi afu anaclik tu YES au NO then kuanzia hapo matatizo tu kwenye pc na ukimuuliza alifanya nini utaskia ah ah skufanya kitu!! Pumbafu!)

JINSI YA KUTIBU BLUE SCREEN
Sasa kama wewe ni mmoja wa wale wanaobahatika kutibu tatizo la Blue Screen kwa ku reboot tu basi pia itakubidi ukae chini na ufanye ucunguzi wa kina ili ujue tatizo hasa ni lipi la sivyo utakuja lia siku moja! Kutokana na uwezekano wa sababu nyiiingi wa tatizo hili inakuwa vigumu sana mtu kwa mara moja tu kusema tatizo la pc yako itakuwa ni hili baada ya blue screen.Ila unaweza tumia njia zifuatazo kukusaidia kutibu:
  1. Embu jaribu ku hisi labda tatizo litakuwa ni nini? Si unaijua pc yako vizuri? sasa ambu narrow down all possible causes za tatizo...mfano umeweka software mpya tu au hardware mpya tu ikaleta blue screen au unadhani baada ya kufanya nini ndo kumesababisha!!? Hii itakusaidia kwenye kuokoa kutumia mda mwiiingi kuanza kutafuta tatizo nini na kutibu yasiyohusika!
  2. Kama tatizo hujui basi washa pc yako kwa safe mode (naamini unajua safe mode ni nini wajameni...kama sivyo bas google it...:confused2: ) na kama tatizo litakuwa linaendelea kujitokeza hata ukiwa ndani ya safe mode basi kwa kiasi kikubwa tatilo hili linasababishwa na hardware either mojawapo imekufa au kama kuna hardware mpya umeongeza kwenye pc yako. kama hi hivi just take it out na kama hujui ni nini kimekufa basi nakushauri ni vyema uipeleke kwa wataalamu zaidi wakusaidie ila kama unauhakika kuna kifaa kipya umefunga mda mfupi au siku chache zilizopita basi kitoe kwanza then ujaribu kutumia bila kifaa hiko...na ikiwezekana badilisha au angalia compatibility issues hapo!
  3. ikiwa umepita hapo na unauhakika hamna hardware iliyokufa wala hujafunga kitu chochote kipya (hivyo unauhakika kuwa hardware sio ishu) basi ukiwa katika safe mode kule kule scan computer yako for virus or spyware kwa antivirus iliyoapdated..fanya full scan( sku hizi kuna hadi antivirus unaweza ku install kwenye flash uka update then ukatumia kwenye pc nyingine) ila hakikisha una uhakika na hiyo antivirus..baada ya hapo kama utapata kitu safisha then iwashe pc yako kama kawaida(sasa angalia inawezekana hao virus wakawa waliharibu baadhi ya systems file na kusababisha pc yako isiwake kabis baada tu ya ku scan..hao inabidi ufanye windows repair).
  4. Kama scanning hukupata kitu na tatizo bado lipo basi sasa ukiwa kwenye safe mode fungua system restore utility (jinsi ya kuipata inatofautiana kulingana na windows gani unatumia ila pia waweza search google how to get system restore in windows (.....) ukaweka window yako na utaipata ila mara nyingi kwa xp huwa kwenye start>all programms>accessories>system tools utaona system restore hapo chagua tarehe ya nyuma ambayo walau una uhakika pc yako ilikuwa ipo poa).
  5. Sasa vipi kama hamna date yoyote zaidi ya tarehe hiyo hiyo ambayo inatatizo? au kama haija solve tatizo? Basi zima pc yako kisha unapoiwasha press F8 mara nyingi mpaka itakapoleta ile windows ya kuchagua safe mode ila usichague safe mode, chagua Run your system from the last known ‘good configuration'.... on the other hand, if you know a recent software installation is the cause, then restore to the point created at that date.
  6. Kama haya yoote hayaja solve tatizo lako basi sasa itabidi uingie ndani zaidi kutafuta suluhisho na hii itahusiana na kujua kwa ukamilifu code numberau hata sehemu u ya error code unayoonyeshwa pindi inapotokea blue screen, copy hiyo error then tafuta online habari zaidi kuhusiana na hiyo error. Kumbuka unaweza ukawa unasumbuka na tatizo kumbe kuna maelfu ya watu walishapitia tatizo hilo na walishalipatia ufumbuzi..hivyo na wewe unaweza pata majibu. Kumbuka blue screen sio tatizo kama matatizo mengine ambayo ukieleza tu utaambiwa aah hiyo..fanya hivi au toa hiki...NO! it differ from one pc to another wakuu..
  7. The bottom line with this error is that you will need to be patient as it may require a lot of trial and error.
Sasa basi kwa wale waliokuwa hawajui, habari ndo hiyo..
Nakaribisha maoni, ushauri au ujuzi zaidi...

fxb

Senior Member
Jun 22, 2011
123
24
ASANTE SANA kwa skuli.....Maskini PC yangu ilipatwa na hii kitu miaka mitatu iliyopita kila aliyepitia hakuweza kufanya chochote ningekuwa na maelezo haya miaka hiyo labda ningereza okoa vitu vingi zaidi.
 
sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,277
ASANTE SANA kwa skuli.....Maskini PC yangu ilipatwa na hii kitu miaka mitatu iliyopita kila aliyepitia hakuweza kufanya chochote ningekuwa na maelezo haya miaka hiyo labda ningereza okoa vitu vingi zaidi.
pole sana mkuu...ila itakusaidia siku nyingine maana haya mambo yapo tu...
 
baghozed

JF-Expert Member
May 26, 2011
532
96
Dah,somo liko powa, Mi nilipata HP pavilion dv 2000,ina Win vista nilipotaka kutumia modem ya airtel ikawa haitambui,so nikaamua kupiga chini vista nikaweka Win 7,cha kustaajabu kuanzia hapo niliweza kutumia modem ila sasa PC ina sleep any time inapoamua wakati naitumia,some time niki i resume inaweza kufanya kazi vizuri tu,sasa sijui hilo tatizo la ku sleep laweza kuwa ni matokeo ya BLUE SCREEN coz inawezekana iliwahi tokea.
Naomba ushauri wako
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,938
1,427
Kwa nyongeza kuna nyezo moja kwenye windws ina weza kukupa mtu taarifa kujua tabia za mashine kabla na baada ya tatizo. Hii inatwa event viewer. katika evenrt viewe unaweza kuona system logs, application logs etc . Detail za Mtatizo yeyte makubwa yanakuwa kwenye system logs na yanakuwa na alama ya error nyekundu

So ni muhimu mtu kuwa sometime anacheki cheki systems events logs za mashine mara moja moja kwenye compter managament.
 
sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,277
Dah,somo liko powa, Mi nilipata HP pavilion dv 2000,ina Win vista nilipotaka kutumia modem ya airtel ikawa haitambui,so nikaamua kupiga chini vista nikaweka Win 7,cha kustaajabu kuanzia hapo niliweza kutumia modem ila sasa PC ina sleep any time inapoamua wakati naitumia,some time niki i resume inaweza kufanya kazi vizuri tu,sasa sijui hilo tatizo la ku sleep laweza kuwa ni matokeo ya BLUE SCREEN coz inawezekana iliwahi tokea.
Naomba ushauri wako
mkuu kwa kungezea blue screen ni kitu kilichowazi kabisa...yaani erroe inapokuja creen huwa ya blue na baada ya hapo labda uzime kabisa computer yako then ujaribu kuwasha tena coz huwezi kuendelea kuitumia hapo hapo baada ya blue screen...ila kwa hili tatizo lako inawezekana kabisa ikawa imesababishwa na version ya window uliyoweka baada ya ku change, inawezekana system yako ni 32 bit ila wewe uliweka win7 64 bit au vice versa...maana kwa kufanya mara kadhaa system hukubali kupokea window hiyo ila matatizo yake ndo hayo ya ku freeze au ku sleep bila sababu maana processor inakuwa imepewa kazi tofauti na inavyotakiwa kufanya kazi...inawezekana pia win ilikuwa sawa ila baadhi ya drivers zilikuwa forced kuingia wakati si za system ya pc hiyo thts why ni muhimu sana mtu unapoamua kuchange window uwe na uhakika na unachokifanya...tatizo letu wabongo mtu pc ikizingua kidogo tu anakimbilia kuchange window bila kujali upatikanaji wa drivers zake au utendaji kazi wa hiyo wind kwenye pc ya aina yake...
 
Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,399
3,197
Mkuu mimi kimeo changu HP G5000 kilikuja na Vista nikadowngrade kwenda Xp ikawa powa, baadae nikapiga chini XP nikaja Win7.
Sasa ninatatizo moja, mfano nikitumia hadi betrii iishe chaji na ijizime yenyewe(hutokea maana betri imechoka na umeme unapokatika ghafla inakaa dk 3 tu inajizima) baada ya hapo ukija kuiwasha inatokea hiyo blue screen kwa sekunde moja na inapotea na lapy inajirestart.

Yaani inawaka vizuri kwa kuonyesha logo ya hp kisha inaboot kwenye windows hadi pale inapotokea logo ya windows7 na inakuwa kama inaload kisha ndio inakuja hiyo blue scren na inapotea kwa sekunde kisha inaji restart kisha itarudia tena kabla ya kukupa option ya kurepair windows, na hata ukirepair hamna kitu.

Nika google sana na nikapata ufumbuzi lakini sio permanent, kwamba ninapo washa tu nipress f8 kisha niinge BIO na ku disable sata, na baada ya hapo inaboot fresh.
Kinachoudhi ni kurudia rudia hiyo process kila mara pindi inapozimika kwa kuishiwa na chaji.

Najua nahitaji betri mpya, nalifanyia kazi lakini kwasasa nifanyaje kuepukana na hili?
 
Kwanza pole sana mkuu..ila naomba nirudie tena kwa mara nyingine (Nadhani itabidi siku moja nitoe hii mada) juu ya kufanya uchunguzi wa kutosha pale unapotaka kubadili window kwenye pc yako...mara nyingi sana pc huwa inaweza kukubali kubadili window ila tatizo likawa kwenye baadhi ya drivers au softwares unazotumia kwenye hiyo pc. si kila driver ya computer yako inaweza fanya kazi sawasawa kwa kila window utakayoweka! ndo maana ni vizuri sana kuhakikisha upatikanaji wa drivers zote kabla ujaamua kubadili window kwa kwenda kwenye web yao afu angalia hiyo window unayotaka kuweka je kwa pc yako ina drivers zake? kama hamna ndo hapo utakapoanzia matatizo ya "kishenzi" (sorry..!) ila yanaudhi! kama unaona hiyo pc inaruhusu window unaytaka kuweka then weka na itakuwa fresh ila kama hairuhusu bora utafute fresh copy ya window ile original iliyokuwepoa au angalia zingine zinazoweza kukubali maana cha msingi ni kupata drivers tu!

Sasa kwa hiyo pc yako inaweza ikawa na sababu kuu mbili...kwanza ni hiyo window uliyoweka si yake so that unaforce drivers zisizo zake kufanya kazi humo (blue screen) na pili ni inawezekana CMOS battery yako imeanza kuisha na ndo maana kila ukiset hiyo SATA pc ikizima inarudi tena na tena...sababu settings zote za BIOS zinatunzwa kumbukumbu yake na CMOS battery... kama sivyo basi nakushauri nenda kwenye web ya hp angalia model sahihi ya pc yako (tafuta run then typr :dxdiag) utaona complete pc model yako) then tafuta kwenye web yao drivers/software ya BIOS kisha u update...
zaidi ya hapo mkuu you better start thinking about installing a new fresh copy ya window ambayo unauhakika inaweza fanya kazi humo!!!
Ni PM kama kutakuwa na ishu zaidi!
 
Nimekupata kwa uzuri mkuu
Nikitulia home nitajaribu hilo zoezi kwanza la ku update BIOS
 
Mlamoto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
351
135
Kuna tatizo pia kama utakuwa ume'enable power saving feature hasa hibernation. Inaonekana hizo dakika hazitoshi kuset sleeping mode. Disable hibernation.
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,207
8,689
Mi laptop yangu ni ya kuvizia!
Naweza nikaiwasha ikawaka fresh nikafanya nayo kazi kwa muda. Lakini nikiizima tu, inakuwa kimeo, haiwaki tena. Yaani sehemu ya kubonyeza kuwasha inawaka vizuri, lakini window kimya kabisa!..sielewi shida ninini, na ni muda sasa!

Pia huwa napata hiyo shida ya BSOD mara nyingi tu, especially nikiwasha laptop huku ikiwa imechomekwa external memory hardware!..nalazimika kuizima kwa ku-power-off, then na-restart, ndo inaendelea!

Mkuu naomba nisaidie nifanyeje kwa shida hii ya kwanza!
 
kwa tatizo la BLue screen nadhani imeshajieleza wazi kuwa ni hiyo usb unayoweka wakati unawasha, inawezekana hiyo ndo inaleta shida wakati wa kuwaka hivyo ndo mana pc inajizima kwa kuleta blue screen...sasa hapo inaweza ikawa tatizo ni hiyo hardware au hiyo port unayoweka hiyo usb au settings katika bios zinazohusiana na usb ports..sasa tatizo kama ni hardware unajua tena ...hapo ni kuchange..na ili ujue kama ni yenyewe unaweza check perfomance yake wakat pc inawaka au kwa kutumia pc ingine..na kama tatizo si hilo basi check port kwa kujaribu kutumia ports zingine...na ikishindikana hiyo basi itakuwa ni settings katika bios, sasa hapa njia ya haraka ni ku reset all settings to their defaults afu check inakuaje ...then baada ya hapo waweza set upya fresh...au pia waweza check vizuri settings zote zinazohusiana na usb uone zimekaaje coz unaweza kuta kuna settings zinaingiliana na usb wakat pc inawaka (kama vile ku boot from usb device ikiwa enabled) na kufanya pc ishindwe kuwaka so kuleta blue screen...ikishindikana kabisa basi wakati inapoleta tu hiyo blue screen embu copy hizo details za hiyo error then check online utapata tu maana yake ni nini na hiyo itakusaidia ku jua tatizo na kusolve.

kuhusu hilo swala la kuwaka bt hai display kitu pia inasababishwa na vitu vingi tu...mfano inawezekana pc yako ilikuwa haijazima kabisa mara ya mwisho(pengine iliingia kwenye sleep mode au hibernation wakat unazima) sasa inapokuwa inawaka mara nyingine huwa inatokea pc inapata shida kuwaka kutokea ktk hali hiyo. hii hutokea pale mtu anapozima laptop afu kabla haijamalizia kabisa kuzima unakuta ameshafunika mfuniko then anaondoka...ukifanya hivi pc haizimi( kama uliwahi kufunika mfuniko/lid kabla haijazima kabisa) matokeo yake huwa ni ku sleep na baadae unapoiwasha ndo unakuta pengine yenyewe ndo inaendelea kuzima na hapa mara nyingi huwa inatumia mda mrefu sana kuzima kulingana na ilikaa mda gani katika hali hii ya kufunikwa bila kuzimwa..sasa hapo ndo inakubidi uizime kabisa thenndo uwashe tena..tatizo hili linawakuta wengi sana bila kujijua na ni chanzo kikubwa sana cha kuua pc maana unakuta mtu anafunga na pc kabisa kwenye begi kumbe bado ipo ON..processor inakufa kwa kasi zaid sababu ya joto!! sasa hakikisha unapokuwa unazima pc yako (na usipende kuzima kwa kushikilia ile button ya on unless imebid sana kufanya hivyo) basi tumia njia sahihi ya kuzima...start,turn off computer, then turn off! sio kushikilia tuuu button ya kuzimia...NOT GOOD!

Sababu ya pili ya kutoonyesha kitu ni drivers za display...inawezekana kabisa hizo drivers zimeiingia si zake(ingawa zimekubali kuingia vizuri) hii inasababisha mara ingine pc ishindwe ku di splay chochote maana wakati mwingine unakuta hizo drivers zimefeli so inabaki giza tu baada ya kuonyesha ile boot screen au wakat mwingine hata hiyo usiione...we unaona pc inawaka ila hamna kitu unaona...ingawa wakati mwingine unakuta inawaka vizuuuri kabisa...!! drivers!! jaribu kutafuta drivers zingine za display ujaribu ikiwezekana tafuta ile litu inaitwa driver detective afu install kisha unaweza kutumia ile kupata details sahihi za drivers za mashine yako na kuzidownload...

ishu ya tatu ni kama huwa inatoa mlio(beep sound) wowote wakati inapofanya hivyo, yaan unapowasha inawaka afu inatoa mlio afu huoni chochote! hii pia inategemea na mlio unaotoka(kama upo) sababu kila beep sound ina wakilisha error code flani..sasa kama ina beep mara moja ina maana yake, mara mbili ina maana yake au idadi yoyote ile inamaana yake..so hili pia linawezekana..

sababu ingine inaweza ikawa ni software ulizoinstall, inawezekana kuna software uliinstall ndo inaleta shida..sasa kutatua hili inabidi ukumbuke angalau ni lini ulianza kupata hilo tatizo kwa mara ya kwanza then uende kwenye system restore ufanye restoration kwenye tarehe ya nyuma zaidi ya hiyo uliyoanza kuhisi hayo matatizo...

nadhani hpo nimejitahidi kueleza kama kuna la ziada we toa details tu naamin wadau wapo wengi tu tutasaidiana...!!!
 
Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872
Mimi juzi juzi ilinitokea mara 2 hiyo blue Screen ya kwenye Laptop ya Rafiki wangu nilikuwa nai format Laptop ya Rafiki yangu Laptop yake ya dell kisha baada kuweka drive ya Graphic card nika kosea kuweka Software yake baada ya kuweka inter graphic mimi nikaweka Nvidia ikatokea hiyo Blue screen mara 2 ikaniumiza kichwa sana kiasi cha kuitoa na kuweka tena yenyewe intel mambo sasa ni poa
 
Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,153
30,872
Mkuu mimi kimeo changu HP G5000 kilikuja na Vista nikadowngrade kwenda Xp ikawa powa, baadae nikapiga chini XP nikaja Win7.
Sasa ninatatizo moja, mfano nikitumia hadi betrii iishe chaji na ijizime yenyewe(hutokea maana betri imechoka na umeme unapokatika ghafla inakaa dk 3 tu inajizima) baada ya hapo ukija kuiwasha inatokea hiyo blue screen kwa sekunde moja na inapotea na lapy inajirestart.

Yaani inawaka vizuri kwa kuonyesha logo ya hp kisha inaboot kwenye windows hadi pale inapotokea logo ya windows7 na inakuwa kama inaload kisha ndio inakuja hiyo blue scren na inapotea kwa sekunde kisha inaji restart kisha itarudia tena kabla ya kukupa option ya kurepair windows, na hata ukirepair hamna kitu.

Nika google sana na nikapata ufumbuzi lakini sio permanent, kwamba ninapo washa tu nipress f8 kisha niinge BIO na ku disable sata, na baada ya hapo inaboot fresh.
Kinachoudhi ni kurudia rudia hiyo process kila mara pindi inapozimika kwa kuishiwa na chaji.

Najua nahitaji betri mpya, nalifanyia kazi lakini kwasasa nifanyaje kuepukana na hili?
kinachotakiwa uwe unatumia hiyo laptop yako pasipo na betri. Kwani betri uliyokuwa nayo kwa sasa imekwisha kufa hiyo nunua nyengine ukisha nunua Betri nyingine uieweke kwenye Laptop yako masaa 8 uichaji kisha uitowe kwenye laptop yako utakuwa unaitumia hiyo betri yako wakati utakapo katika umeme usitumie betri pamoja na waya wa umeme wa laptop yako pamoja nina maanisha unapotumia Laptop tumia kwa njia ya umeme toa nje hiyo Betri tumia umeme itakuwa hiyo betri yako ina maisha marefu hata kama umeme ukikatika iataweza kukaa japo hata masaa 2 chaji yake. Huo ndio ushauri wangu.
 
baghozed

JF-Expert Member
May 26, 2011
532
96
100% uko sawa ndugu,coz kama hii pc haipo ktk pc zinazo support win 7,niliforce tu,na drivers kweli niliforce tu za vista kwenye win 7.Ahsante kwa ushauri,hope nikirudisha win vista itakuwa poa.Thanx again
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom