Blog mpya ya wanafunzi wa elimu ya juu.

TzCampusVibe

Member
Nov 1, 2011
9
0
Wanafunzi wa Elimu ya juu sasa wanauwanja mpana wa kutoa na kuhabarishana taarifa mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya chuo ambazo zinahusu maisha mazima ya elimu ya juu nchini.

tzcampusvibe | Life of University Students ni jukwaa jipya la wasomi kuweza kutoa habari za kinachoendelea chuoni kwao kama mahafali, matukio ya kimichezo, shughuli za kijamii, kimasomo, kisiasa na hata kiuchumi zinazohusu wanafunzi wa elimu ya juu nchini. Kumekuwa na habari nyingi zikitokea vyuoni lakini zinakosa vyombo vya habari vya kuvipa nafasi ya kutosha. TzCampusVibe imeamua kwa dhati kabisa kufanya shughuli hiyo.
Tembeleo Leo ujue kinachoendelea chuoni kwako na vyuo vingine nchi.

tzcampusvibe | Life of University Students
 
kwa hiyo sis ambao hatujasoma haturuhusiwi?????
 
kwa nini msitengeneze vyenu.University mnashindwa hata ku-create website za kawaida,mkapata pa kuhost bure mpaka mtumie wordpress.com,blogspot.com.hii ni aibu,.

sasa kuna tofauti ipi na bloger wa darasa la 7 na bloger wa CHUO KIKUU maana nyote mnatumia tamplete zile zile.

kaza vichwa,achana na miziki,starehe
 
@Rutunga mawazo mazuri kabisa ni kweli lakini kila kitu kina mwanzo wake na si swala la kwamba haiwezekani kufanya hivyo bali ni uwamuzi wa kuanza kuangalia kipi kinafaa kufanya kwa wakti huo na muda ukiwadia wa kufanya lengine zaidi basi litafanyika hakuna lisilowezekana katika dunia hii.
Asante kwa changamoto yako.
 
Habari ndugu yangu.
Si kwamba hii blog haaisomwi na ambao hawasomi la hasha bali hii blog inarusha habari zinazotokea vyuoni lakini jamii yote inaweza kusoma habari hizo kwani kuna matukio mengi sana yanatokea kwenye vyuo amabayo yanaelimisha jamii lakini hayapati nafasi kwenye vyombo vya habari nchini kwaiyo kupitia humu jamii itapata kujua nini kinatokea katika chuo fulani..na kujifunza au kuhabarika kutokana na habari hizo.
Unakaribishwa sana.
 
Hii ni blog inayotoa habari zinazotoka taasisi za elimu ya juu ndugu Connetected Guy kwaiyo hao wote wanaruhusiwa kublog na wanakaribishwa sana.

Tutumie tu habari kama unazo kutoka huko na sisi tutazipublish kulingana na malengo yetu.

Asante.
 
Mbona hiyo blog yenyewe haipo kitaaluma zaidi? nilzani nitaona vijana wakiwa wanafanya utafiti kwenye maabara au maeneo mbalimbali ya kitaama, au hata wakiwa wanajadili mambo ya kujenga na kuinua sarafu yetu, nimebakia kuona watu wanaruka kwanja, au vyuoni ndio kupo hivyo???? jamani tuelimisheni hata sisi wenzenu ambao hatujabahatika kusoma hadi chuo kikuu ili siku tukibahatika tuje na viwalo vya kupatia BURUDANI???
 
mbona kuna taarifa nzuri tu ndugu? au wewe umebase kwenye negative tuu? huu ni mwanzo wao kwaiyo tarajia maboresho sizan kama niwakati muhafaka wa kuwakatisha tamaa
 
mbona kuna taarifa nzuri tu ndugu? au wewe umebase kwenye negative tuu? huu ni mwanzo wao kwaiyo tarajia maboresho sizan kama niwakati muhafaka wa kuwakatisha tamaa

thanxs, wazo ni zuri ila natamani hizo picvha zingine waziondoe waweke za kitaaluma zaidi
 
Mwanzo mgumu kk endelea kuiboresha kadri unavyoweza.hayo maneno yasikutishe hata kwenye kanga yapo.
 
Asanteni wote kwa michango yenu na changamoto zenu,
1. Imebase sana SAUT kwasababu wanaondesha ni mwanafnzi kutoka SAUT lakini blog inajitihadi kupata habri nyengine toka vyuo mbalimbali nchini kama baadhi ya post nilizotuma kwenye blog, hata vyombo vingi vya habari vilivyo Daar es salaam vinahabari nyingi za dar es salaam kuliko mikoa mingine ni kutokana na uwezo mkubwa wa kukusanya habari sehemu husika lakini dhumuni la blog ni kuhabarisha kila kitu kinachotokea katika vyuo mbalimbali pale wawakilishi wetu wanapotutumia habari.

2. Kuhusu kuweka habari za kitaaluma, kutokana na mission na vision ya blog zinavyoeleza, zimeelezea madhumuni ya blog kwamba ni kuelemisha, kuburudisha na kuhabarisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa vitu vinavyotokea..ukiingia kwenye blog utakuta habari na taarifa mbalimbali kutokana na philosophy na ethics za blog hiyo..

Asanteni wadau , naomba kuwasilisha.
 
ila shida hakuna habari mpya.. Wahusika wa hii blog mko wapi Mtujuze?
 
Back
Top Bottom