MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,035
- 64,850
Katika hali isiyo ya kawaida Tony Blair amekiri kufanya makosa huko Iraq lakini bado anadai alitimiza wajibu wake kama Waziri Mkuu wa nchi.
Ukweli wa Ripoti ya Chilcot inasema kulikuwa hakuna mahusiano yeyote kati ya serikali ya Iraq na Al Qaeda wala kundi lolote la kigaidi.
Silaha bado hazijapatikana lakini raia wasio na hatia wa Iraq wanahangaika mpaka hivi sasa. Nchi yao haikaliki ni ugaidi na mauji ya kutisha kila kukicha.
Leo nimeangalia nimeshangaa tu na kusikitika kwa jinsi mataifa ya Magharibi yanaendelea kuleta saisa kwenye maisha ya watu.
Hasa aliposema "THE WORLD IS A BETTER PLACE WITHOUT SADAM HUSSEIN"
Huyu jamaa ni mharifu wa kivita, kifupi hawa ICC ndiyo ingewahusu sana ili wajiunge na wahuni wenzao kina Konyi, Ntaganda, Taylor etc
Link: Blair pledges ‘no excuses’ for Iraq, then spends 2hrs making excuses
CC: Dotworld , Bukyanagandi , vyuma , Masunga Maziku , kahtaan , MOTOCHINI , melkiorysaranga , MSEZA MKULU