Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,882
Blackmailing tumezoea kuona ikifanywa na wahuni na wezi wa kutumia mbinu hii ama vikundi vya kihalifu.... BLACKMAILING HAIFANYWI NA MFANYAKAZI WA UMMA TENA WA NAFASI YA JUU...ni aibu kubwa kwa taifa kwa aliyeuteua kwa chama chako ofisi yako jamii inayokuzunguka familia ndugu jamaa na hata viongozi wako kiroho
Kwamba kwa mamlaka uliyonayo unayatumia vibaya kwa kuanzisha operation ambayo utawasakama uliowachagua kwa sababu unazozijua mwenyewe ili uwatikishe na kuwatisha kwa kuwabambikia tuhuma na mwisho wa siku urudi kwa mlango wa nyuma kumalizana nao kiaina... Hii ni blackmail
Unaweka wapi uso wako aliyeuteua anapogundua kuwa mali ulizonazo unazipata kwa njia haramu kabisa za kiharamia hasa?
Unawezaje gari binafsi ubandike namba na nembo za serikali ikiwemo bendera ya taifa? Tafsiri yake ni nini hapa KUKWEPA KODI! mamlaka ya mapato mpo hapo???
Huu ni utapeli wa kijinga kijuha na kiwendawazimu kabisa.. Utapeli na wizi wenye kuacha alama! Wenzako wajanja huchukua cash tu! Strictly cash na kuzitakatisha... Ujuha huu umeacha mlolongo mrefu wa ushahidi pasipo shaka
Magari na nyaraka zake zote zenye umiliki wa wahusika wa watuhumiwa wako unamiliki wewe!!! Ninini hiki unafanya? Kwanini umejipalia mkaa wa moto ili ujibanike mwenyewe? Mteuzi wako ataweka wapi uso wake ?
Mnaweza wote kuvaa uso wa kima na mkakausha kau.... Lakini mmechafua mbaya
Hii blackmailing imejulikana kote.... Jitafakarini upya