blackberry bold 9700

cheeter

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2011
Posts
475
Reaction score
155
Nani anautundu wa hii simu??can I use internet without suscribing with BBm services?
 
Nani anautundu wa hii simu??can I use internet without suscribing with BBm services?

Unaweza, unaingia tu kwenye browser na unatumia mtandao kama kawaida. Mimi nnayo na nnaitumia kwenye mtandao bila BB Service. kumbuka BBM ni kitu kingine na BBS ni kitu kingine, bbm ni ile messenger tu na hii ni lazima uwe na BBS ndio unaitumia bure, ukiitumia BBM bila BBS haikubali na inapokubali basi ujuwe inatuma sms badala yake ambayo inakula pesa kutokana na mtandao uliokuwa nao.

Natumai nimeeleweka.
 

Nijuavyo BB hazikubali SKYPE unless kuna ujanja unafanyika mimi siujuwi nnatumia BB miaka 3 sasa lakini sijapatapo kuona SKYPE ikikubali, kama kuna ujanja huo tujuze.
 
Nijuavyo BB hazikubali SKYPE unless kuna ujanja unafanyika mimi siujuwi nnatumia BB miaka 3 sasa lakini sijapatapo kuona SKYPE ikikubali, kama kuna ujanja huo tujuze.
Kuna mtu kaniambia uwe na skype kwenye hiyo Blackberry na pia mwenzako unaye chat nae pia awe nayo hiyo hiyo Skype kwenye blackberry yake ndiyo inaweza kukubali kutumika hiyo skype pasipo na internet connection. Je wewe unaye Mtu mwenye blackberry kama yako wewe ?
 

Ndio nnazo BB mbili 9700 na 9900, lakini mpaka sasa huu ujanja wa skype sijaujuwa, kama kuna ujanja huo jaribu kumuulizia mtu atujuze, nnajuwa kuwa BB kuna apps nyingi sana ambazo watu wanazifanyia ujanja na zinafanya vizuri, hii ya Skype ikiwa ipo basi itakuwa vyema sana, tafadhali niulizie.
 
FF, hebu tuambie vizuri bana, mimi najua haiwezekani kutumia browser ya BB ku-access internet kama haupo kwenye pay plan ya BBS. It is just impossible.

Lakini ukiweka browser nyingine say Opera, inawezekana ku-access internet kwa plan ya kawaida ya mobile internet kutokana na aina ya mtandao unaoutumia. Pamoja na kuweka browser nyingine, unaweza kutakiwa kufanya certain settings ili ikubali.

Kwa ambae anafahamu otherwise atujuze.
 

Mimi natumia BB 9700 na BB 9900 na zamani nilishawahi kutumia 9600 zote zina browser ya BB na nnaingia mtandao wowote ule, niliwahi kuweka browser zingine kama Opera na nyingine nyingine lakini nimependa zaidi ya BB. Na hakuna tatizo lolote kwa hizo simu nnazotumia mimi, sijui kwa model zingine sijawahi kuzitumia,

BB yangu moja iko kwenye BBS na ni kwa sababu ya BBM na apps tu, BB yangu moja haipo kwenye BBS na nnaingia nayo mtandao wowote kwa browser yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…