Captain Donor
Member
- Jul 24, 2022
- 13
- 19
Zimebaki siku 30 tu hadi kufikia siku ambayo muendelezo wa filamu ya Black Panther kuanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kama alivyopata kusema Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, "Elimu ni kujifunza kutokea kwenye vitabu, kutokea kwenye radio, kutokea kwenye filamu, kutokea kwenye mazungumzo kuhusiana na mambo ambayo yanaathiri maisha yetu".
Filamu ya Black Panther imenifunza mengi, binafsi nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mazungumzo kuhusiana na vipi itakuwa muendelezo wake baada ya kifo cha Chadwick Boseman ambaye aliigiza kama King T'challa?
Nimejifunza kwamba mchango wa Chadwick kuanzia kwenye uandaaji wa filamu hiyo na uigizaji wake ndani ya filamu, ulikuwa ni wa kiwango cha juu sana katika kuuvaa uhusika wa King T'challa.
Jambo ambalo limewapa wakati mgumu Marvel Studio kwa ujumla wake kujua utakuwaje muendelezo wa Black Panther bila ya Chadwick Boseman hadi kufikia hatua ya kutaka kuurecast uhusika wa King T'challa kama ilivyofanyika kwenye uhusika wa Paul Walker ndani ya filamu ya Fast&Furious baada ya Paul kufariki.
Jambo ambalo lilipingwa na watu wengi lakini mwisho wa siku kilichokuja kufanyika kinaashiria ukubwa wa legacy aliyoiacha Bwana Chadwick Boseman.
Tarehe 11 mwezi ujao Black Panther 2 itaanza kuonyeshwa kwenye kumbi za Cinema. Kwa hapa kwetu Tanzania sijajua itaanza kuonyeshwa tarehe ngapi ila nitafurahi sana kama Century Cinemax watatupatia "Experience" ya kuuona muendelezo huo siku hiyo. Licha ya kutokujua itaonyeshwa tarehe ngapi hapa Tanzania, natumai nitakuwa miongoni mwa mamilioni ya waafrika watakaopata nafasi ya kuiangalia kwa mara ya kwanza itakapoonyeshwa kwenye nchi zao.
Urithi aliouacha Chadwick Boseman (King T'challa) utaenziwa kwa ukubwa mno siku hiyo, tangu alipoaga dunia mnamo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka juzi akiwa na miaka 43.
Tutashuhudia "Experience" burudani ya kipekee itakayojawa na wakati wa furaha, huzuni, na shauku katika kila kipande cha filamu hiyo inayohusu maisha ya uhusika ndani na nje ya uigizaji. Nje ndani ya filamu hii kwangu binafsi inahusu maisha ya Chadwick kama King T'challa na ni ukweli usiopingika kwamba kuanzia muandaaji mkuu na wahusika wengine kwa pamoja wameamua kuuenzi mchango wa Chadwick Boseman kupitia muendelezo huu mara baada ya kipindi kirefu cha kufikiri ni kipi kifanyike.
Migogoro ya hapa na pale baina ya Marvel Studio na baadhi ya waigizaji katika mchakato wa kutengeneza muendelezo huu. Kiufupi ulikuwa ni wakati mgumu ambao hatimaye unaenda kuzaa matunda kutokana na kuupa kipaumbele urithi (legacy) wa Chadwick Boseman ambaye aliigiza kwa shauku na ukubwa wa kiwango cha juu katika sehemu ya kwanza.
Tasnia ya filamu ilimpoteza jemedari wakati ambapo alihitajika zaidi na wakati huohuo umma wa Wamarekani weusi pamoja na dunia kwa ujumla ukawa umepoteza shujaa wa aina yake ambaye safari yake ya maisha ilikatizwa na ugonjwa wa saratani ya utumbo mpana.
Licha ya hivyo urithi wake bado utaendelea kuishi kizazi baada ya kizazi na tarehe kama ya leo mwezi ujao utaenziwa mchango wake kwenye tasnia ya filamu akiwa kama baba, mume na mwanaharakati, kwa ule msemo maarufu wa "WAKANDA FOREVER". Binafsi nitamuenzi kwa ule usemi wa "YIBOMBE"!