Biteko: Rais Magufuli anatamani kuona Kiwanda cha kusafisha madini kinaanza kazi

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
BITEKO: RAIS MAGUFULI ANATAMANI KUONA KIWANDA CHA KUSAFISHA MADINI KINAANZA KAZI

Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatamani kuona kiwanda cha kusafisha madini cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinachoendelea na ujenzi wa kusimika mitambo ya kusafisha madini jijini Mwanza kinaanza kazi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Waziri Biteko amesema baada ya kukamilika kwa kiwanda hicho, Tanzania kama nchi itapata faida nyingi ikiwemo ajira kwa watanzania, kukua kwa teknolojia nchini, kuongezeka kwa mapato ya Serikali, pia nchi kupitia Benki Kuu ya Tanzania itapata akiba ya dhahabu na Watanzania watashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa madini.

“Nchi nzima inakiangalia hiki kiwanda wakiwemo wachimbaji wadogo ambao watapata soko la uhakika kwa madini yao na kwa bei ya soko la dunia kwa siku husika na pia watapata madini mengine yaliyochanganyikana na madini yao, hivyo hakikisheni mnamaliza kusimika mitambo kwa muda ili kiwanda kianze kufanya kazi na kuleta faida kwa wana mwanza na watanzania kwa ujumla,” alisema Waziri Biteko.

Pia, Waziri Biteko amewataka STAMICO kuwatendea haki wabia wao na kuhakikisha wanawashirikisha kila jambo ambapo amewapongeza wabia hao kwa kutoa mitaji yao na kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Aidha, baada ya Waziri Biteko kutembelea kiwanda hicho, alipata fursa ya kuzungumza na bodi ya STAMICO ambapo ameipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya mpaka kupelekea Wizara ya Madini kupata heshima kubwa kupitia Shirika hilo ambalo kwa sasa linajiendesha kwa faida.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amesema, ili Shirika la Madini la Taifa liondokane na changamoto ya wafanyakazi, Shirika halina budi kuajiri wafanyakazi wa mikataba ambao watakuwa wa muda mfupi ambao wataangaliwa utendaji wao wa kazi kama ni nzuri waongezewe na kama ni mbovu mkataba usitishwe.

Pia Prof. Msanjila, amesema Wizara ya Madini imeshapeleka ombi la kupatiwa fungu la kununua mashine ya kuchoronga miamba ambapo mpaka sasa hivi lipo katika hatua za mwisho ili wapatiwe fungu hilo kutoka Wizara ya Fedha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dkt. Venance Mwase amesema, utegemezi wa STAMICO wa fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake umepungua kutoka asilimia 73.8 kwa mwaka wa fedha 2015/16 hadi asilimia 32.5 kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha, Dkt. Mwase amesema kuwa, Shirika limeongeza bajeti ya makadirio ya kiasi cha mapato yake yanayotokana na vyanzo vyake vya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22 makadirio ya mapato ya ndani ni shilingi bilioni 45.2 ukilinganisha na shilingi bilioni 19.4 za mwaka wa fedha 2020/21.

“Lengo kuu la mtambo huu ni kuongeza thamani ya madini ya dhahabu yanayochimbwa nchini kabla ya kusafirishwa, pia mradi huu utaongeza mapato kwa nchi kupitia mlabaha na kodi mbalimbali pamoja na kutoa ajira mbalimbali kwa watanzania,” amesema Dkt. Mwase.
 
Kilo tano za mwanzo za zaabu tunamzawadia Rais wetu JPM,kama heshima kwa kuipapatua Tanzania kutoka katika giza kubwa sana tena nene la walanguzi ambao leo hii wanavitumia vyama koko vya siasa kutaka kuivuruga Tanzania yetu. Raisi kupitia chama pendwa amewaona wadhoofu hao na amewanyamazisha vizuri tu, kelele zao sasa ni kama sauti ya fisi nyakati za usiku au yale majibwa koko aliepigwa jiwe.
 
Nina wasiwasi na manpower ya STAMICO kama wanaweza kuendesha such huge investment.

STAMICO wanaendesha shughuli/operation zao like the old school. STAMICO wanatakiwa wabadilike sana ili kuendana na kasi ya Mh. Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. STAMICO waachane na mambo ya ukiritimba ana redtapism!!

Lakini let's give them another chance!!!
 
Otherwise, I will volunteer myself to prepare the blueprint and 5 years business plan for STAMICO at free of charge kwasababu mimi ni mzalendo!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatamani kuona kiwanda cha kusafisha madini cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinachoendelea na ujenzi wa kusimika mitambo ya kusafisha madini jijini Mwanza kinaanza kazi.
Kwahiyo objective ni kumfurahisha Rais na siyo kuchakata madini
 
BITEKO: RAIS MAGUFULI ANATAMANI KUONA KIWANDA CHA KUSAFISHA MADINI KINAANZA KAZI

Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatamani kuona kiwanda cha kusafisha madini cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinachoendelea na ujenzi wa kusimika mitambo ya kusafisha madini jijini Mwanza kinaanza kazi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Waziri Biteko amesema baada ya kukamilika kwa kiwanda hicho, Tanzania kama nchi itapata faida nyingi ikiwemo ajira kwa watanzania, kukua kwa teknolojia nchini, kuongezeka kwa mapato ya Serikali, pia nchi kupitia Benki Kuu ya Tanzania itapata akiba ya dhahabu na Watanzania watashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa madini.

“Nchi nzima inakiangalia hiki kiwanda wakiwemo wachimbaji wadogo ambao watapata soko la uhakika kwa madini yao na kwa bei ya soko la dunia kwa siku husika na pia watapata madini mengine yaliyochanganyikana na madini yao, hivyo hakikisheni mnamaliza kusimika mitambo kwa muda ili kiwanda kianze kufanya kazi na kuleta faida kwa wana mwanza na watanzania kwa ujumla,” alisema Waziri Biteko.

Pia, Waziri Biteko amewataka STAMICO kuwatendea haki wabia wao na kuhakikisha wanawashirikisha kila jambo ambapo amewapongeza wabia hao kwa kutoa mitaji yao na kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Aidha, baada ya Waziri Biteko kutembelea kiwanda hicho, alipata fursa ya kuzungumza na bodi ya STAMICO ambapo ameipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya mpaka kupelekea Wizara ya Madini kupata heshima kubwa kupitia Shirika hilo ambalo kwa sasa linajiendesha kwa faida.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amesema, ili Shirika la Madini la Taifa liondokane na changamoto ya wafanyakazi, Shirika halina budi kuajiri wafanyakazi wa mikataba ambao watakuwa wa muda mfupi ambao wataangaliwa utendaji wao wa kazi kama ni nzuri waongezewe na kama ni mbovu mkataba usitishwe.

Pia Prof. Msanjila, amesema Wizara ya Madini imeshapeleka ombi la kupatiwa fungu la kununua mashine ya kuchoronga miamba ambapo mpaka sasa hivi lipo katika hatua za mwisho ili wapatiwe fungu hilo kutoka Wizara ya Fedha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dkt. Venance Mwase amesema, utegemezi wa STAMICO wa fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake umepungua kutoka asilimia 73.8 kwa mwaka wa fedha 2015/16 hadi asilimia 32.5 kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha, Dkt. Mwase amesema kuwa, Shirika limeongeza bajeti ya makadirio ya kiasi cha mapato yake yanayotokana na vyanzo vyake vya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22 makadirio ya mapato ya ndani ni shilingi bilioni 45.2 ukilinganisha na shilingi bilioni 19.4 za mwaka wa fedha 2020/21.

“Lengo kuu la mtambo huu ni kuongeza thamani ya madini ya dhahabu yanayochimbwa nchini kabla ya kusafirishwa, pia mradi huu utaongeza mapato kwa nchi kupitia mlabaha na kodi mbalimbali pamoja na kutoa ajira mbalimbali kwa watanzania,” amesema Dkt. Mwase.
HIVi waungwana serikali inapata mapato makubwa sana kutoka kwenye sekta ya madini kwanini isije na mbinu ya kuwainua hawa wachimbaji wadogo wadogo kwa kuwapatia mashine hata kama kwa kukodi kwa bei ambayo ni nafuu watu wachimbe madini na kulipo kodi iih pia inakuwa ni uwekezaji mzuri kama utaenda sambamba na utelekezaji mzuri Sana.
 
Serikali ipo kwa ajili ya faida tu.
Wala haitaki kuingia hasara yeyote
 
BITEKO: RAIS MAGUFULI ANATAMANI KUONA KIWANDA CHA KUSAFISHA MADINI KINAANZA KAZI

Imeelezwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatamani kuona kiwanda cha kusafisha madini cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinachoendelea na ujenzi wa kusimika mitambo ya kusafisha madini jijini Mwanza kinaanza kazi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Waziri Biteko amesema baada ya kukamilika kwa kiwanda hicho, Tanzania kama nchi itapata faida nyingi ikiwemo ajira kwa watanzania, kukua kwa teknolojia nchini, kuongezeka kwa mapato ya Serikali, pia nchi kupitia Benki Kuu ya Tanzania itapata akiba ya dhahabu na Watanzania watashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa madini.

“Nchi nzima inakiangalia hiki kiwanda wakiwemo wachimbaji wadogo ambao watapata soko la uhakika kwa madini yao na kwa bei ya soko la dunia kwa siku husika na pia watapata madini mengine yaliyochanganyikana na madini yao, hivyo hakikisheni mnamaliza kusimika mitambo kwa muda ili kiwanda kianze kufanya kazi na kuleta faida kwa wana mwanza na watanzania kwa ujumla,” alisema Waziri Biteko.

Pia, Waziri Biteko amewataka STAMICO kuwatendea haki wabia wao na kuhakikisha wanawashirikisha kila jambo ambapo amewapongeza wabia hao kwa kutoa mitaji yao na kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Aidha, baada ya Waziri Biteko kutembelea kiwanda hicho, alipata fursa ya kuzungumza na bodi ya STAMICO ambapo ameipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya mpaka kupelekea Wizara ya Madini kupata heshima kubwa kupitia Shirika hilo ambalo kwa sasa linajiendesha kwa faida.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amesema, ili Shirika la Madini la Taifa liondokane na changamoto ya wafanyakazi, Shirika halina budi kuajiri wafanyakazi wa mikataba ambao watakuwa wa muda mfupi ambao wataangaliwa utendaji wao wa kazi kama ni nzuri waongezewe na kama ni mbovu mkataba usitishwe.

Pia Prof. Msanjila, amesema Wizara ya Madini imeshapeleka ombi la kupatiwa fungu la kununua mashine ya kuchoronga miamba ambapo mpaka sasa hivi lipo katika hatua za mwisho ili wapatiwe fungu hilo kutoka Wizara ya Fedha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji STAMICO Dkt. Venance Mwase amesema, utegemezi wa STAMICO wa fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake umepungua kutoka asilimia 73.8 kwa mwaka wa fedha 2015/16 hadi asilimia 32.5 kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha, Dkt. Mwase amesema kuwa, Shirika limeongeza bajeti ya makadirio ya kiasi cha mapato yake yanayotokana na vyanzo vyake vya ndani ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22 makadirio ya mapato ya ndani ni shilingi bilioni 45.2 ukilinganisha na shilingi bilioni 19.4 za mwaka wa fedha 2020/21.

“Lengo kuu la mtambo huu ni kuongeza thamani ya madini ya dhahabu yanayochimbwa nchini kabla ya kusafirishwa, pia mradi huu utaongeza mapato kwa nchi kupitia mlabaha na kodi mbalimbali pamoja na kutoa ajira mbalimbali kwa watanzania,” amesema Dkt. Mwase.
Mbona leseni za wachimbaji zinachukua muda mrefu hazitoki? Sababu hasa ni nini? Lazima tujifunze kuwapa wawekezaji confidence kwamba tunachosema tuna maanisha
 
Mda mwingine serikali nayo miyeyusho
 
Back
Top Bottom