Fadlu ni kocha mzuri ila muoga sana hasa kwenye mechi kubwa. Mashabiki wa Yanga wajiandae kuwa wanashika roho hata zile mechi za kawaida za kushinda na kurelax. Udhaifu mkubwa kwa Fadlu upo timu ikiwa inaongoza goli moja ghafla tu anaibadilisha timu ianze kuzuia badala ya kuendela kushambulia na kutafuta magoli zaidi hata kama mshindani wake ni timu ya kawaida. Na wakati mwingine unakuta ndio mchezo upo mwanzoni kabisa yeye anairudisha timu kwenye kuzuia na kuondoa utamu wote wa mchezo.
Sasa nikiangalia aina ya uchezaji ya Yanga ya kushambulia mwanzo mwisho hapo lazima mmoja akubali kubadilika. Ni aidha Fadlu akubali uchezaji wa Yanga au Yanga wakubali kuingia kwenye mfumo wa Fadlu.