Birmingham City masharti lukuki kutua Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Birmingham City masharti lukuki kutua Dar

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, May 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MABINGWA wa Kombe la Carling nchini England, Birmingham City, wanatarajiwa kutua nchini Julai mwaka huu kwa ziara maalumu ya kimichezo ambapo watakipiga na vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga, jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa baadhi ya maofisa wa juu wa timu hiyo, akiwemo kocha msaidizi, Andy Watson, pamoja na daktari Ian Mc Guinness, wanatarajiwa kuwasili nchini Mei 9 kwa ajili ya kukagua Uwanja na Hoteli.

  Rage alisema, ujumbe huo utakagua Uwanja wa Taifa utakaotumika, pamoja na hoteli ya Kilimanjaro Kempinski ili kuona kama vinakidhi vigezo vya timu hiyo, ambayo itaambatana na mashabiki wasiopungua 1,000 ambao watajilipia gharama za hoteli na uwanjani.

  Alisema, usiku wa Julai 7, Birmingham itakipiga na Simba kabla ya jioni ya Julai 12 kukipiga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2010/2011, Yanga.

  “Tunafurahi kupata wasaa wa kuwa wenyeji wa timu kubwa kama hiyo, ujio wao huo utafungua mipaka ya kimataifa baina yetu na wao…tayari tumeshazungumza na watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya ujio huo,” alisema Rage.

  Katika hatua nyingine, Rage alisema mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa klabu hiyo, unatarajiwa kufanyika Mei 15 katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam na wanachama watakaoruhusiwa kushiriki ni wale ambao watakuwa wamelipa ada ya mwaka ambayo ni sh 12,000 pamoja na ile ya uwanja sh 20,000 na kwamba malipo hayo yafanywe katika akaunti ya wanachama.

  Pia Rage alisema, uongozi umetoa saa 48 kwa wapangaji wanaotaka kuendelea kupanga katika jengo lao kuwasiliana na uongozi, kinyume cha hapo watakwenda kuomba kibali chama mahakama kwa ajili ya kuwaondoa kwa nguvu.

  Wakati huo huo, beki wa timu hiyo Kelvin Yondani amewasilisha barua ya kuomba msamaha kutokana na utovu wa nidhamu huku akisihi arudishwe kundini, wakati mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi ambaye naye aliadhibiwa kutokana na kukiuka mkataba kwa kuzungumza sana na vyombo vya habari, akitakiwa kusoma upya mkataba wake na kutoa maelezo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Birmingham City masharti lukuki kutua Dar
  • Rage aishangaa Yanga, aanika Nchunga ndiye aliyemwaga wino

  na Juma Kasesa


  [​IMG] WAKATI benchi la Ufundi la mabingwa wa Carling Cup, Birmingham City ya England, likitarajiwa kutua jana usiku, uongozi wa klabu hiyo umeanika masharti lukuki kabla ya kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga Julai mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema benchi hilo la ufundi linakuja kwa ajili ya kuja kukagua uwanja, hoteli na hospitali ambavyo watavitumia wakitua jijini kwa michezo hiyo.
  Akifafanua kuhusu masharti hayo, Rage alisema mabingwa hao wa Carling, wanataka kucheza mechi hizo katika uwanja usio wa nyasi za bandia, huku ukisisitiza kuwa ziwe na urefu usiozidi sentimeta sita.
  Alisema, licha ya kugoma kucheza uwanja wa nyasi bandia, pia Birmingham wanataka kufikia katika hoteli yenye hadhi ya kimataifa na kutibiwa katika Hospitali ya Agakhan, ambayo benchi hilo la ufundi linatarajiwa kwenda kufanya ukaguzi ili kujiridhisha kabla ya timu hiyo kuja jijini Dar es Salaam.
  Bechi hilo la ufundi linaongozwa na meneja msaidizi na daktari wa timu hiyo kwa ajili ya kufanya ukaguzi, tayari kwa mechi hizo za kirafiki, ambazo zitakuwa ni sehemu yao ya maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini England.
  Birmingham ambao wako katika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ambao hivi karibuni walilitwaa Kombe la Carling baada ya kuifunga Arsenal 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley, bao lao likifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Obafemi Martins, itaanza kutupa karata yake kwanza kwa kukipiga na Simba Julai 12 kabla ya kuvaana na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Julai 14 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
  Katika hatua nyingine, Rage alisema, ameshangazwa na hatua ya uongozi wa Yanga kusema hauna taarifa za michezo hiyo, ilhali mwenyekiti wake, Lloyd Nchunga, ndiye aliyesaini makubaliano ya kucheza mechi hizo.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  ingekuja Man U je, si tungedeki hotel wanayofikia kwa ulimi, chakula chao kitoke england kwa ndege maalum - duh kazi ipo.

  Kitimu chenyewe kipo hatarini kushuka daraja, makeke kibao.
   
 4. k

  kommen Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kisa sie hatuonekani kwenye 'ramani ya soka' ndio maana hata timu isiyo na mashiko kwao kwetu yataka kututoa kamasi!
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hahaha lol
   
 6. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  BIRMINGHAM CITY ARE PLANNING PRE-SEASON TPIP TO TANZANIA
  first team coach.Andy Watson and Chief medical officer Ian Mc Guinnes have travelled to Africa to inspect facilities. Birmingham are expected to undertake a four days trip,although details have not yet been finalised.Tanzania top flight sides Simba and Yanga could provide opposition at the National stadium in Dar es salaam. Watson said 'The people of Tanzania that we have met have been very hospitable and kind.For what we've seen of country so far it looks an amazing place.We have been made aware of how much the people of Tanzania love their football-especially the Premier league when everythng is fully in the place we look forward to coming in july and playing."
  source THE SUN 11/5/2011 ​
   
 7. Mkasika

  Mkasika JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Blues are set to visit the African country of Tanzania on pre-season tour this July.
  Although exact dates and details are yet to be confirmed the four-day trip is expected to include a game against one of the Tanzanian top flight sides Simba and Yanga, or possibly both, in the National Stadium (pictured, above) in Dar-es-Salaam.[​IMG]
  First team coach Andy Watson and chief medical officer Ian McGuinness are currently in the country inspecting facilities.
  Watson told bcfc.com: "The people of Tanzania that we have met have been very hospitable and kind and from what we've seen of the country so far it looks an amazing place.
  "We have been made aware of just how much the Tanzanian people love their football - especially the Barclays Premier League - and when everything is fully in place we look forward to coming back in July and playing."
  As and when more details are available you will be able to find about them first here at bcfc.com.
  [​IMG]
   
 8. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndo hadhi wanayostahili, kwa akili yako ulitaka wafikie wapiwapi guest house?
   
 9. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Afya na Usalama wa mchezaji ni kitu muhimu sana katika professional football. Usikute hata Madrid ya jk haikuja kwa vile walichunguza na kukuta hatuko vizuri iwapo ingetokea Sergio Ramos kaumizwa na Canavaro.
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hawa waandishi wenu wa habari wameona uvivu hata ku-google matokeo halisi ya fainali ya carling cup? Au wamefanya hesabu ya 2-1=1?
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,002
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Rage kishaanza kulikoroga,mpaka alinywe.Asije kuanza sanaa zake.mara wameghairi,mara nini sijui.Au anataka umaarufu tu hamna kitu?
   
 12. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sometimes hata wakiwa uwanjani hawajui goli limefungwaje, na mchezaji gani kafunga!
   
 13. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,469
  Likes Received: 4,741
  Trophy Points: 280
  Najaribu kujiuliza lengo hasa la ziara hii na mantiki yake, huenda wanakuja kugonga kikombe au kutalii na njia rahisi ni minajiri ya kukipiga nchini, sijasikia kama hizo hoteli nani atagharamika, isije kuwa mambo ya Brazil hapa.........
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,307
  Likes Received: 22,111
  Trophy Points: 280
  Kweli Man U ni mashetani na mashetani ni mapepo, mnayatumikia na kuyashabikia mapepo, tena nayo yanawatumikisha thats y mko tayari kupiga deki kwa ulimi kwa kuwa nyie ni watumwa wa mashetani mekundu
   
Loading...