BIOS Imekufa HP laptop Haicharge Help!!

Sabode

Senior Member
Apr 11, 2008
160
21
Salama wanaJF.
Nimepata HP Omnibook xe4400 Laptop kutoka kwa mshikaji inachapa kazi uzuri kama ninavyo taka. Ila tatizo lililopo haicharge battery, na hii inanifanya nifanyie vijishughuli vyangu pale tu palipo na power, yaani ofisini au nyumbani lkn nikiwa mahala pengine nakwama. Nimepeleka kwa fundi kaniambia bios imekufa na wao hawawezi kudoo jambo lolote kuiponya! Sasa kama mnavyo jua wenyewe JF pamekamilika hebu nisaidieni la kufanya maana bila kucharge battery hii inakuwa haina maana kamili ya laptop.

Msaaada plizzzzz.
 
BIOS ingekua imekufa sidhani kama ungeweza kuwasha na kutumia hiyo laptop, Battery itakua imekufa, nunua battery mpya.
 
Ndugu kama uko dar es salaam nenda mitsumi computer garage samora ave au kvd indira ghandi wanazo battery unaweza kununua nyingine kama ingikuwa ni bios usingeweza kuwasha
 
Nimenunua new battery
tatizo ni kuwa haicharge battery ila niki plug direct power mambo mazuri kabisa.
ili bila kuwa pluged problem
 
Nimenunua new battery
tatizo ni kuwa haicharge battery ila niki plug direct power mambo mazuri kabisa.
ili bila kuwa pluged problem

Mkuu heshima mbele.

Sasa "battery" ulionunua ni ya model gani hiiohio ya HP Omnibook xe4400 au mradi tu ni "battery"?
 
Mkuu heshima mbele.

Sasa "battery" ulionunua ni ya model gani hiiohio ya HP Omnibook xe4400 au mradi tu ni "battery"?
Anyway Battery niloo nunua ni battery yake.
yaani nimepata genuine battery ambayo ni exactly the same na niliyodhani kuwa imekufa, na ndipo kwa uelewa wangu nikabaini problem ni kuwa laptop haicharge battery.
Si ndo nikapeleka kwa fundi AA computers Arusha baada ya diagnosis jamaa wakaniambia BIOS imekufa hivyo haita charge, lakini kifaa kinapiga mzigo kama kawa kwa direct power.
 
Mkuu,

Kinadharia ni kwamba BIOS (Basic Input/Output System) inasaidia kazi kufanyika kati ya "micro processor" na "IO device control" na inadhibiti "flow" ya "information" na "data".

Kwa mfano ukichomeka device kama video card, BIOS inasadia kusafirisha hizo video kwa uharaka ili uone video hizo katika monitor ya computer yako.

Kwa hio kama hao mafundi wameshindwa kubadilisha BIOS kwenye kipengele cha ufanyaji kazi kupitia Setup menu basi hio laptop inafaa tu kwa kazi za kawaida tu ukitumia applications za office na kadhalika.

Nafikiri umenielewa.

Naishia hapo.
 
Nimekusoma mkuu Richard.
Suala langu nifanye nini ili iweze kucharge battery ili niweze kuitumia hata wakati nikiwa nje mahali ambapo hakuna ulazima au uwezekano wa kuplug to mains.
Hope this way nitakuwa nimesaidika kabisa.
 
Oh pia angalia connector zinazogusa battery kwenye laptop, labda zimeharibika.
 
Du Kunta
Mzee hapa bongo kama si fisadi, hauwezi kusumbuliwa na laptop kidogo tu ukimbilie kununua mpya unakomaa nayo kwanza. Au siyo bana kwa hiyo bado nakomaa nayo kiaina kwanza
 
Back
Top Bottom