sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,488
Kuna msemo usemao, mama ni mama na mtoto hakui kwa mama yake. Ni sawa ila tuje kwenye hoja.
Kuna mabinti wakubwa hadi miaka 30 ila wanapenda kufuatana sana na mama zao hasa kwenye misherehe. Wanasahau kuwa mama anahitaji kutoka na mume wake na binti atoke na mume ama mchumba wake.
Mbona vijana hawaongozani na baba zao? Yaani mke anamuaga kabisa mume wake kila weekend anamsindikiza mama sehemu fulani. Hasa mabinti ambao ni wa pekee kwa wazazi hao.
Tuelezane waungwana, je huu ni ungwana? At least miaka mingapi kumsindikiza mama kila mahali? Nani anafanya makosa kati ya binti anayejipeleka au mama anayempokea?