nyembeason
Member
- May 4, 2009
- 44
- 21
Wadau, msaada tafadhali. Binti wa miaka 15 (mwanafunzi-secondary na shule haendi tena) alikanyagwa tarehe 24/06/2016 na gari ya serikali, BOT, na.SU 36797, katika maeneo ya Mkundi-Morogoro, barabara kuu ya lami ya Moro-Dom. Alipelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro. Matibabu yakafanyika na kuwekewa HOGO-POP. Dereva alishitakiwa na kupigwa faini ya TZS 30,000/ AU kifungo cha mwaka mmoja. Dereva alilipa faini.
Mtoto analelewa na mzazi mmoja-mama na maisha ni duni sana-tena sana. Nimekuwa nikiisaidia familia kwa kiasi nikijaliwa, nauli na matibabu na pia kwa kuipeleka kesi yake Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa msaada wa kisheria. Amepewa Wakili na ameandika barua kwa kampuni ya BIMA. Hawataki kulipa. Hali ya mtoto ni MBAYA SANA kwa sasa. Mguu umevimba upya na unaonekana mifupa haikuunga kabisa. Wadau msaada kwa hili tafadhali