hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,250
- 26,639
Kwa makala hii, Utaelewa sababu na kiini cha mgogoro na chuki ya Waislamu kwa Wayahudi.
Waislamu kuwachukia Wayahudi sio jambo la ajali, kila jambo lina sababu na asili yake. Hakuna siasa ya ajali duniani. Wao wanawaita "Mayahudi" neno hilo likiwa limebeba uzito ndani yao. Allah kupitia mtume wake katika Quran 5:51 anawaonya Waislamu wasifanye urafiki na Wayahudi na Wakristo sababu wao ni marafiki wao kwa wao. Na katika Quran 5:82 anabainisha kuwa katika maadui wakubwa zaidi wa Waislamu ni Wayahudi.
Chanzo cha chuki hii
Inatokana na mgogoro wa kidini, kiuchumi na kisiasa kati ya Wayahudi na Muhamad na wafuasi wake (Waislamu). Mgogoro huu ndio uliopelekea vita vikubwa kati ya Waislamu na Wayahudi na pia ndio uliopelekea Muhamad kurogwa na hatimaye kufa kifo kichungu sana cha sumu hapo baadae. Ili tuweze kupata yakini ya asili ya mgogoro huu sharti turejee historia.
Kabla ya Mtume kuhama kutoka Makka hadi Madina (Hijra) mnamo 622 B.K. Madina (iliyokuwa ikiitwa Yathrib) ilikuwa na makabila mawili ya Kiarabu ya Aws na Khazraj. Pia kulikuwepo makabila matatu makubwa ya Kiyahudi:
i) Banu Qaynuqa
ii) Banu Nadir
iii) Banu Qurayza
Wayahudi hawa walimiliki ardhi, bustani, na walikuwa matajiri na wakiendesha uchumi wa Madina na bara Arabu kwa ujumla. Na zaidi hasa Banu Qaynuqa walikuwa wanatekinolojia ya zana za kisasa za vita, pia walikuwa wahunzi na masonara na watengenezaji wa mapambo na vyombo mbalimbali. Hivyo walitengeneza pesa nyingi na kujenga miji mikubwa. Waarabu (hasa Aws na Khazraj) mara nyingi walipigana vita vya kikabila, na Wayahudi walishiriki kwa upande mmoja au mwingine na ndio waliokuwa wakopeshaji na wadhamini wa vita. Na mwisho wa vita walivuna faida kubwa sana na kuendelea kuwatawala Waarabu kiuchumi na kisiasa.
Mabadiliko ya kisiasa
Wakati Mtume Muhammad kahamia Madina (Hijra), alikuta jamii iliyogawanyika.Ili kuleta utulivu, alitengeneza katiba ya Madina (Sahifat al-Madina), hati ya kihistoria ambayo iliunda muungano wa dini mbalimbali, Waislamu na Wayahudi, kuwa “umma moja” ya kisiasa, kwa masharti kwamba, Kila kundi litashirikiana kulinda Madina. Halitasaidia maadui wa nje. Wote watakuwa huru katika dini zao.
Hivyo mwanzoni, hakukuwa na uadui kati ya Muhammad na Wayahudi.
Kinyume chake, alikuwa karibu nao na alisali kuelekea upande wa Yerusalemu (Qibla ya kwanza), na aliwaheshimu kama watu wa kitabu (Ahl al-Kitab).
Sababu za kuinuka kwa migogoro
1. Migongano ya Kidini
Kadiri Uislamu ulivyokua, uhusiano ulianza kuharibika. Mtume Muhammad alitangaza kuwa yeye ni mjumbe wa Mungu wa mwisho, akiwathibitisha manabii kama Musa na Isa.
Wayahudi wengi walikataa kumtambua kama nabii, wakisema Ujumbe hauwezi kutoka kwa Mwarabu, kwani wao waliona unabii ni wa kizazi cha Israeli pekee. Qur’an inataja majibizano haya;
“Na walipoambiwa: Aminini katika yale aliyoyateremsha Allah, walisema: Tunaamini katika yale tuliyoteremshiwa sisi tu.” (Qur’an 2:91).
Hivyo kwa mujibu wa Torati walimchukulia Muhamad kuwa ni nabii wa uongo. Jambo ambalo liliamsha chuki kati ya wafuasi wa Muhamad dhidi ya Wayahudi. Hadi leo hivi Wayahudi wanamwona Muhamad ni nabii wa uongo.
2. Migogoro ya Kisiasa
Baada ya Mtume kuwa kiongozi wa Madina, alihitaji umoja wa kijamii ili kujilinda dhidi ya Makka. Baadhi ya makabila ya Kiyahudi (hasa Banu Nadir na Banu Qurayza) walivunja makubaliano ya katiba, kwa:
Kusaidia maadui wa Waislamu kutoka Makka. Kufanya njama za kumuua Mtume (kama ilivyotokea Banu Nadir).
Kusaliti makubaliano wakati wa Vita vya Khandaq (Ahzab).
Hayo yakawa chanzo cha vita na kuwatimua baadhi yao.
3. Uchumi
Waislamu wengi walikuwa masikini sana baada ya Hijra walitegemea msaada wa jamii ya Kiyahudi. Baadhi ya Waislamu waliamini Wayahudi walitumia riba na biashara ya dhuluma (ingawa kwao ilikuwa halali kisheria. Ona Kumb 23:19,20 ).
Muhamad alikemea tabia hizo, jambo lililoanzisha uhasama wa kiuchumi kati ya Wayahudi na Waislamu. Shas bin Qais mzee na kiongozi wa Kiyahudi baada ya kuona hilo aliwafitinisha makabila ya kiarabu ilikuwa manusura yarudi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kama Muhamad asingeingilia kati. Hivyo tokea hapo Muhamad na Wayahudi wakawa maadui. Namwona hapa Muhamad kama Pan Arabinism.
Matokeo ya Migogoro hiyo
1. Wayahudi wa Banu Qaynuqa (Mwaka 624 BK)
Walisema maneno ya kejeli baada ya ushindi wa Waislamu katika Badr. Vita vikazuka; walizingirwa siku 15; hatimaye wakatolewa Madina.
2. Wayahudi wa Banu Nadir (Mwaka 625 BK)
Walipanga kumvizia Mtume wakati wa ziara ya kijamii. Walizingirwa na kuhamishwa kuelekea Khaibar. Katika mgogoro huu ndipo Muhamad aliporogwa na kuathirika kwa uchawi.
Riwaya zinataja kwamba kiongozi wa Banu Nadhir alimpa Labid Ibn al Asam pesa na amri ya kumfanyia uchawi Mtume Muhamad. Labid alitokea kabila la Ban Zuraiqa, riwaya zingine zinasema ni Myahudi na zingine zinasema ni muarabu mwenye ushirika na Wayahudi.
"Labid ibn al-Asam alitumia uchawi juu ya Mtume, akitumia nywele na vitu vingine, na akamsababisha uchungu mwilini mwake na kushindwa kuingiliana na wake wake."
Katika Riwaya kutoka Sunan Abu Dawud (Kitabu cha Sihr – Uchawi), hadithi no. 4297. Aisha r.a. alisema:
“Labid ibn al-Asam alitumia uchawi juu ya Mtume, akitumia nywele, kichanga, na shaba, na kuviacha kwenye nyumba ya Mtume. Baada ya muda, Mtume alianza kuhisi uchungu na dhiki isiyo ya kawaida..."
Na sehemu nyingine anasema:
“Siku moja Mtume alifanyiwa uchawi kiasi kwamba alianza kudhani amefanya jambo ambalo kwa hakika hakuwa amelifanya.” (Sahih al-Bukhari, Kitabu cha 58: Tiba, Hadithi 3175)
3. Wayahudi wa Banu Qurayza (Mwaka 627 BK)
Walisaliti wakati wa Vita vya Khandaq, wakaruhusu maadui kuingia upande wao. Baada ya vita, walihukumiwa kwa mujibu wa sheria za Kiyahudi (Torati). Wanaume waliopigana waliuawa, wanawake na watoto wakachukuliwa mateka.
4. Wayahudi wa Khaibar (628 BK)
Baada ya makabila ya Kiyahudi kuhamishwa, wengi walikusanyika Khaibar na kuunda ngome za kijeshi. Mtume Muhammad aliwashambulia ili kuzuia mashambulio ya baadaye.
Hapo ndipo alipokutana na Safiyyah bint Huyayy, binti wa kiongozi wa Kiyahudi aliyeuawa vitani. Akawa mateka wa vita na baada ya hapo mtume Muhamad kupata habari zake za urembo, akamtwaa kutoka kwa mtekaji muislamu na hivyo baada ya mtume kulala naye kwa siku tatu, akapendezwa naye akaamua kumwoa kabisa na kumtoa kuwa mtumwa.
Tukio la sumu katika Khaibar
Baada ya ushindi wa Waislamu katika Vita vya Khaibar (628 BK), watu wa Khaibar walimwalika Mtume Muhammad kula chakula kama ishara ya upatanisho. Hapo ndipo mtume alipotiwa sumu kwenye chakula.
Katika Sahih al-Bukhari (Hadith 2617), Sahih Muslim (Hadith 2190), tunasoma;
“Baada ya Khaibar, mwanamke wa Kiyahudi (Zaynab bint al-Harith), mke wa Sallam ibn Mishkam, alimletea Mtume mbuzi aliyechomwa na kuweka sumu. Mtume alikula kipande kidogo, kisha akatema, na akasema:
‘Mfupa huu wa bega unanijulisha kuwa umewekwa sumu.’”
Zaynab bint al-Harith ni Nani?
Alikuwa mmoja wa wanawake wa ukoo wa Qurayza, waliokuwa washirika wa wapiganaji wa Khaibar. Mume wake, Kinana ibn al-Rabi’, aliuawa katika vita hivyo. Yeye ndiye aliyepika na kuweka sumu kwenye mbuzi wa kuchoma, akilenga kulipiza kisasi kwa hasara ya watu wake waliouawa.
Matokeo ya sumu hiyo
Mtume Muhammad aliumia, lakini hakufa wakati huo; alitema chakula haraka. Lakini mmoja wa maswahaba aliyeitwa Bishr ibn al-Bara’ ibn Ma’rur alikula zaidi, na alikufa kwa sumu hiyo. Mtume aliwaamuru kumhoji Zaynab. Alikiri wazi:
“Nilitaka kuona kama wewe ni kweli Nabii. Kama ni Nabii, Mungu atakujulisha; kama sivyo, basi tumepata kisasi.” (Ibn Hisham, Sirah, Juz. IV)
Alifanya hayo kwasababu Wayahudi wanaamini kuwa nabii wa kweli wa Mungu hawezi kufa kwa sumu. Hata Wakristo pia ndio imani yao.
Athari za sumu
Ingawa sumu iliingia kidogo tumboni mwa mtume lakini athari zilianza kuonekana baadae na kuanza kuteseka kwa maumivu ya kichwa na tumbo kwa muda wa miaka mitatu mfulilizo. Vyanzo vinasema:
Alitema chakula mara moja, lakini sumu ilishaanza kuingia mwilini.
Alianza kuhisi maumivu ya mara kwa mara, hasa kwenye bega na kichwa.
Kwa miaka michache baada ya hapo, alilalamika kuhusu “uchungu unaorudi kila wakati”.
Katika siku zake za mwisho yaani miaka 3 mbele mtume alishuhudia mateso anayopitia. Katika riwaya ya Bukhari inasema:
“Mtume alisema katika siku zake za mwisho: ‘Nilihisi athari ya chakula kile cha Khaibar; sasa muda wangu wa kufa umekaribia.’”
(Sahih al-Bukhari, Hadith 4165)
Na tena katika Sahih al-Bukhari (Hadith 4165) imenukuliwa,
“Sikuwahi kusahau siku ile ya Khaibar; sumu ile bado inanihisi hadi leo. Na sasa, muda wangu wa kuondoka (kufa) umekaribia.”
Na katika Ibn Sa’d – Tabaqat al-Kubra (Juz. II) inasema,
“Mtume alisema: ‘Nilihisi mishale ya sumu ile, sasa ni wakati mwili wangu unamalizia kuishiwa nguvu kwa ajili yake.’”
Siku tano kabla ya kifo chake, alisema:
"Laana ya Allah iwaangukie Mayahudi na Wakristo..Sahihi Bukhar, juzuu ya kwanza, uk. 62.
Siku ya nne kabla ya kifo chake, aliusia mambo matatu na moja lake ni:
Mayahudi, Wakristo na Wapagani wafukuzwe Arabia. Ona, Bukhari mlango wa maradhi ya mtume.
Siku ya kifo chake
Akiwa katika nyumba ya Aisha akiegemea kifuani mwake huku anapiga mswaki, kwa maumivu makali ya kichwa na homa, Muhamad alinyanyua mkono wake juu na alisema maneno haya:
“Pamoja na wale uliowakirimia kwa hisani yako ambao ni Mitume, wasema kweli (As-siddiqīn), mashahidi na watenda mema. Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe na Uwe na huruma kwangu, na Niinue katika daraja la juu (rafīq al-aʿlā).”
Kisha alitamka maneno hayo mara tatu na akawa amekata roho, Innā lillāhi wa inna ilayhi rajiun.
Tukio hili lilitokea asubuhi pevu siku ya Jumatatu, tarehe 12 Rabiul Awwal, mwaka wa kumi na moja Hijra (11 A.H.) ambao ni mwaka 632 BK kwa kalenda ya Greogory. Alipofariki dunia alikuwa na umri wa miaka sitini na mitatu na siku nne.
Hivyo basi leo ukiona Waislamu wana hasira na Wayahudi jua hoja sio kwasababu ya Palestina tu, kuna asili yake huko nyuma. Makundi kama Hamas, Hezbollah, Houthis na Iran mdhamini wao: msingi wao mkuu ni kuifuta Israeli katika uso wa dunia. Hata katika vita vya siku sita vya mwaka 1967 hoja ilikuwa ni kulifuta taifa la Israeli. Kwahiyo sio jambo la ajali. Katika riwaya za kislamu zinasema kiyama hakiwezi kuja hadi waislamu wawaue Wayahudi wote duniani. Hoja hii Netanyahu alishaipeleka katika baraza la umoja wa mataifa na akasema kamwe Israeli haitafanya muhafaka na yoyote juu ya usalama wake.