Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,487
- 20,268
Njaa ilipozidi huko Gombe, wazee wakakaa kikao ili kupata ufumbuzi. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, wakakubaliana watafute sokwe mrembo. Wamkate mkia na kumremba na kisha wamuoze kwa binadamu. Walijua kuwa binti yao huyo atawapa access ya kula mahindi kwenye shamba la binadamu kirahisi.
Wakafanya hivyo, wakampata binti mrembo, wakamkata mkia na kumpamba sana. Hata hakujulikana kama ni sokwe. Binti yule akajipitisha kwa mkulima mmoja mkubwa bachela aliyeitwa Maduhu. Maduhu akampenda na kumuoa.