Binti huyu ameniharibia weekend yangu!

Binti huyu ameniharibia weekend yangu!

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
6,287
Reaction score
10,947
Jana jioni natoka kazini nikakutana na binti mmoja ambaye kiumbo alinivutia!

Mara baada ya salaam nilimwomba tuzungumze japo 5minutes,

Kwanza alikataa akasema ana haraka anawahi kwenda kupika ametoka sokoni kununua mboga,

Lakini baada ya kumbembeleza sana alikubali kunisikiliza nami baada ya kujitambulisha tuliongea mengi naye akanieleza sio mwenyeji wa hapa ila alikuwa masomoni ndo amehitimu chuo na amekuja kumsalimia mama yake mkubwa.

Nilimwomba tuwe wapenzi akasema atanifikiria,

Tulipeana contact then tukaagana.

Usiku nkampigia hakupokea nkajua amesinzia nikamtumia sms "good knite"

Leo asubuhi akanibeep nkampigia akasema amepata safari ya ghafla anataraji kurudi kwao Shinyanga hivyo nikamwomba ikiwezekana tuonane kabla hajasafiri akasema leo mchana atakuwa free,

kwa kua kwangu ni mbali na kwao alishauri nitafute guest mitaa ya karibu ili asichelewe kurudi nyumbani jioni.

Saa 8 unusu nshalipia chumba na kumuelekeza nilipo akasema anamalizia kuoga anakuja,

saa 9 nampigia simu hapokei baadaye anapokea anasita kuongea kisha anakata na kunitumia sms "honey niko njiani nakuja,

Je uko chumba no ngapi?"
Nikamjibu "niko no 9"
Nkiwa chumbani nikapata wazo la kwenda duka la hapo jirani kununua condom,

Ile natoka dukani namwona demu anashuka kwenye tax akiwa na wanaume wanne!

Nilisita kidogo na hawakuniona,demu alitangulia halafu wale jamaa wakasimama nje kama wanapanga jambo flani kisha wakaingia ndani!
Demu akanipigia na kusema"baby nimefika chumbani hakuna mtu naona kuna vinywaji tu! Uko wapi?"
nikamjibu "niko toilet nakuja"

Nimejaribu kuchungulia naona wale jamaa wamesimama koridoni kama kuna mtu wanamsubiri!

Kwa bahati nzuri sikuja na usafiri wangu hivyo nlizima simu nikaondoka kimyakimya nkachukua tex mpaka home!
Sijui nini kiliendelea huko lakini sa hivi nawasha simu nikakuta ujumbe huu
"I'm sorry baby,sikuwa na nia mbaya ila wakati nataka kuja mme wangu alinikuta na kugundua nawasiliana na wewe,amenipiga sana na kulazimisha nimlete gesti ulipo ndo tukaja ila nashukuru Mungu umenusurika alikodi watu watatu!
I love u,
Mme wangu akisafiri ntakutafuta"

Wana MMU Wenzangu najiuliza huyu alikuwa na maana gani aliponiambia hajaolewa ndo kamaliza chuo na anaishi kwa mamkubwa!
Namshukuru Mungu kuninusuru na balaa hili mpaka sasa nimelala sina hamu na hawa mabinti!
 
Ndio shida ya vile vya fasta fasta mtu hamjajuana vizuri.
 
Du nenda kamshukuru Mungu kwa imani yako maana wabongo siku hizi wanawafanyia sana wanaowafumania na wake zao na kuwatoa ktk media.
 
Mmmh, ck nyingine uwe makini na inakuwaje mtongozano unakuwa rhc hivyo and within short time tyr quest. Unamwona mtu mara moja ila unamchunguza zaid ya kipind flan.
 
Shukuru umepona

Lengo lilikuwa wakufanyie ujambazi

Muongo huyo ni mwanamke na kundi lao ni majambazi wote
 
Aisee hii hatari sana. Hapo leo usingepona 'mduku' yani tigo. Huyo hafai, kwa nini afiche kuwa hajaolewa???Pole sana, vinginevyo leo ungeanza ukurasa mpya wa ukamerumi bila kupenda. Huyo binti futa namba, na umwambie hutaki mazoea, tena kwa ukali kabisa.
 
Wadau bwana, unamshuru Mungu kwa kunusurika au kwa kukuepushia dhambi? we unafanana na wale wanaoshangilia wakati wa kugegedana et "Yesu wangu" wakati wapo dhambini.
 
Du! Pole sana, michepuko noma, baki njia kuu!!


Na ya nyuma iravusha teri
 
We kweli inabidi umshukuru Mungu, mana ilibaki kidogo tu utatuliwe marinda.
 
Hiyo noma sana mshikaji,heri umeponea chupu chupu
 
Mjini shule!! Demu raha yake akusumbue kidogo bana, we demu gani unajibebea kama mzoga na wewe unajiamini na kufurahia!!! Bahati yako ungetoa kifurushi wewe...!!
 
Hao wengi sana siku hizi. Asilimia 40 ya fumanizi za siku hizi ni feki zinapangwa.
 
Kaa mbali na na mademu.....
Jitahid kutafuta mdada
 
mkuuu umenudurika kuvurugwa kinyesi aiseee
 
Back
Top Bottom