Binti ang'atwa ulimi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti ang'atwa ulimi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Oct 21, 2010.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  WIVU wa kimapenzi wamsababishia ulemavu wa maisha mkazi wa Izia Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa Grace Senga (29)baada ya kung’atwa ulimi wake na kipande kutolewa wakati wakigombea bwana.  Mama mzazi wa binti huyo Salome kapele ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Izia aliwaeleza waandishi wa habari hizi jana waliofika nyumbani kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 usiku wakati binti yake huyo akitoka klabu ya pombe za kienyeji kunywa pombe.  Alisema kuwa akiwa amelala aligongewa mlango wa wasamaria wema kumjulisha juu ya tukio hilo la kuvamiwa kwa binti yake huyo japo hakuweza kutoka nje kwa kuhofu usalama wake kutoka kwa wavamizi hao .  "Kweli siku ya tukio kuwa vijana walikuja kunigongea mlango wangu na kunieleza kuwa motto wangu anapigwa ila sikuweza kutoka kwani niliogopa kuchomwa kisu katika ugomvi huo iwapo ningetoka……baada ya hapo alikuja kijana mwingine na kunieleza kuwa motto wangu amng’atwa ulimi basi sikutoka hadi alipokuja mme wake ndipo nilitoka na kwenda kumkuta akiwa hoi”


  Mwenyekiti huyo alisema baada ya kufika eneo la tukio alimwona binti yake huyo akiwa amelala chini jirani na eneo hilo la klabu ya pombe za kienyeji huku damu zikiwa zinamtoka kwa kasi .


  Kapele alisema kuwa baada ya hapo walikwenda kumkamata mwanamke huyo ambaye mbali ya kumng’ata ulimi binti huyo pia usiku huo huo alikuwa amemng’ata kidole mme wake ambaye alikuwa akimuuliza sababu za kulowa damu .


  Hata hivyo alisema mbali ya kumkamata mwanamke huyo na mpenzi wake huyo ambaye walishirikiana naye kumfanyia unyana huo binti huyo bado walilazimika kwenda eneo la tukio na kufanikiwa kuokota kipande cha ulimi ambacho baada ya kumng’ata alikitema chini.  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Isunto Mantage alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kinyama na kumtaja mwanamke huyo ambaye alitenda unyama huo kuwa ni Agnes Mandi (25) mkazi wa mtaa huo wa Izia pamoja na Mpenzi wake Mashaka Lupasha (32) pia mkazi wa mtaa huo wa Izia .


  Alisema kuwa watu hao wote wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumjeruhi mwanamke huyo wakiwa katika klabu cha pombe ya kienyeji kijulikanacho kama Katamakondo na kuwa kwa pamoja walisaidiana kumshambulia mwanamke huyo na kung’ata ulimi wake.


  Kwa mujibu wa kamanda Mantage kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mwanamke huyo aliyetendewa unyama huo alipata kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume huyo Lupasha kabla ya kutengana .


  Hivyo alisema kuwa kuwa siku hiyo ya tukio mwanamme huyo akiwa na mpenzi wake wa sasa Agnes Nandi alimkuta Grace Senga akiwa katika eneo hilo la pombe akiendelea kunywa pombe na ndipo ugomvi baina yao uliponza na kupelekea wapenzi hao kumchangia kwa kipigo huku wakimkaba koo .


  “Mbinu waliyotumia kumng’ata ulimi ni ile ya kumkaba koo na baada ya kuzidiwa alitoa ulimi wake nje mithiri ya mtu anayetaka kufa na ndipo wanamke huyo alisogea na kumng’ata ulimi wake na kutoa kipande cha ulimi ….hadi sasa binti huyo hawezi kuongea kabisa “

  Kamanda huyo alisema kuwa watuhumiwa hao wote wawili wamekamatwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa .
  source; Francis Godwin ni mzee wa matukio daima
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah inasikitisha sana.
  Hivi huyu binti si ndo basi tena atakuwa BUBU?
  Cha kusikitisha zaidi denda ndo basi tena hata utamu wa vitu hawezi kuupata tena.
   
Loading...