Inaelekea CCM weshapanga kila aina ya mkakati kutaka kumsafisha Kapuya.
Alianza afande Kova,licha ya tuhuma hizi zinazomkabili Kapuya za kubaka kuripotiwa kwenye kituo chake cha polisi cha Oysterbay,afande Kova alijegeuza chombo cha mahakama na "kuhukumu" kuwa Kapuya hana kesi ya kujibu,kwa kuwa suala hilo la kubaka,ni jambo binafsi,kati yake Kapuya na hako kabinti!
Jana amekuja Le Mutuz,naye amejigeuza mahakama,kwa kudai kuwa licha ya kuwa anao uhakika kuwa Kapuya alisex na hako kabinti,lakini akatoa hoja ya kuwa binti huyo wakati anasex na Kapuya,hakuwa na umri wa miaka 14,bali yeye ni mama mzima,ambaye tayari ana mtoto mmoja!
Tayari maelezo ya Le Mutuz,yanajikanganya na tamko,lililotolewa na Kapuya mwenyewe,kupitia kwa wakili wake kuwa Kapuya hamfahamu kabisa huyo binti,na hajawahi kukutana naye katika maisha yake yote!
Sasa ndiyo anakuja na huyu incredible,naye anakuja na story yake kuwa huyu ni binti hatari,ambaye ni mzoefu wa kublackmail watu!
Pamoja na Le Mutuz na huyu incrredible,kutoa hukumu kwa kumsafisha Kapuya kuwa hana hatia,lakini hoja za msingi kwenye kashfa,hawazitolei ufafanuzi.
Miongoni mwa hoja hizi ni kuwa licha ya kuthibitika kuwa meseji za vitisho zilizotumwa kwa binti huyo zilitoka kwenye namba iliyosajiliwa kwa jina la Juma Kapuya,ni kwa vipi wakili wa Kapuya adai kuwa ingawa ni kweli namba hiyo ilikuwa ya Kapuya,lakini alishaigawa miezi 6 iliyopita,jambo ambalo hata kama lingelikuwa la kweli,ni uvunjifu wa wazi wa sheria,kwa kuwa lengo la kusajili line,lilikuwa kuwa kuwabaini wahalifu wanaozitumia line zao kutoa vitisho kwa wengine.
Mkanganyiko.mwingine ni kuwa pamoja na Le Mutuz na huyo incredible kudai kuwa wakati Kapuya anasex na huyo binti hakuwa under 18,lakini na wao pia hawatwambii huyo binti kwa sasa ana umri gani,ili ijulikane wakati Kapuya anasex kwa mara ya kwanza,je alikuwa over 18 au under 18?!
Maswali haya ya msingi yanapaswa yakajibiwe mahakamani,na siyo kwa staili hii inayofanywa na maCCM,ili kutaka kuiokoa meli yao inayoelekea kuzama kutokana na kashfa hii nzito,inayomkabili kada mwrnzao Kapuya.
Ikumbukwe kuwa suala la kuelewekwa umri halisi wa huyo ni muhimu sana ukafahamike mahakamani,kwa kuwa sheria za ubakaji ziko wazi kuwa hata kama binti anaridhia mwrnyewe kufanya sex,lakini ikithibitika kuwa alipofanya hivyo alikuwa under 18,tayari hiyo inakutia hatiani kuwa umebaka!
Si mnakumbuka hata the former PM wa Italy,Berlusconi alivyotiwa hatiani baada ya mahakama kuthibitisha kuwa binti aliyesex naye,wakati anafanya naye alikuwa na miaka 17?
Kwa mazingira hayo sioni kitu gani jeshi la polisi linashikwa na kigugumizi kuifikisha kesi hiyo mahakamani,ili mbivu ikajulikane huko?
Kama jeshi la polisi linatekeza kikamilifu Katiba yetu kuwa wananchi wote wako sawa mbele ya sheria,basi kwa speed ile ile walivyoipeleka fasta fasta kesi ya babu seya na mwanae Papii Kocha,ambao kwa sasa wanatumikia.kifungo cha maisha kwa kutiwa hatiani,kwa kosa la kubaka,basi kwa speed ile ile waipeleke fasta,kesi hii inayomkabili Kapuya ya kubaka na kutishia kuua!