Bingo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bingo..

Discussion in 'International Forum' started by The Boss, Jan 2, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mamia wamiminika kwenye ATM inayotoa hela mara dufu
  [​IMG]
  Wateja waliomiminika kwenye Bank hiyo kuwania pound za bureFriday, January 16, 2009 11:38 PM
  Zaidi ya watu 100 walipanga mstari kwenye mashine ya kutolea fedha ATM baada ya kugundua mashine hiyo ilikuwa ikitoa kiasi cha fedha mara mbili ya kilichotakiwa kwa muda wa masaa manne kabla tatizo kugundulika.Inafikiriwa kwamba maelfu ya pound yalitolewa katika mashine hiyo kwa muda wa masaa manne kabla ya tatizo katika ATM hiyo ya kampuni ya Sainsbury iliyopo Welshpool,Powys nchini Uingereza kugundulika.

  Bank ya Sainsbury imesema haina mpango wa kuwataka wateja wake kurudisha hela hizo.

  Mashine hiyo ilianza kuvuta watu jumatatu jioni baada ya kugundulika mashine hiyo ilikuwa ikitoa 'bingo'.

  Msemaji wa benki hiyo Natasha Virtue alisema "ATM yetu ya Welshpool ilikuwa ikitoa pound 20 kwa kila pound 10 iliyotakiwa kutoa".

  "Hii ilitokana na matatizo ya kiufundi ambayo tumeishayashughulikia, lilikuwa tatizo la muda mfupi tu" alisema msemaji wa benki hiyo.

  "Ilikuwa ni bahati ya wateja wetu usiku wa jumatatu, tungependa kuweka wazi kuwa hatuna mpango wa kuwadai" alimalizia kusema msemaji wa benki hiyo.

  Source: News Agencies
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu hiyo bingo ilitulia, hapa bongo iliwahi kuwatokea walimu kwenye benki ya NMB mjini Mbeya wakavuta na kuanza wakidhani wameongezewa mishahara, wakati ule wana mgogoro na serikali.Walivyorudi tena kucheck na account zao walikuta zimefungiwa kwa order ya manager, walipokwenda kumuuliza wakaambiwa walizidishiwa kwa makosa!!
   
Loading...