Binafsi ninapenda sana kunyoa kipara

Binafsi ninapenda sana kunyoa kipara

MAFIA MGAX

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2023
Posts
430
Reaction score
552
Heshima yenu wana JF

Binafsi ninapenda sana kunyoa kipara,lakini changamoto kubwa ambayo huwa ninaipata japo si mara kwa mara ni maumivu na kuota kwa vipele upande wa kwenye kisogo.

Je ni nini chanzo cha tatizo na ni njia gani ya kutatua tatizo hilo?
 
Saluni nyingi ni chafu hawana muda wa kusafisha machine kwa kila mteja
Kama ni kipara mbona ni rahisi kujinyoa mwenyewe na vioo viwili.....
Huwa ninanyoa kwa kiwembe lakini siwezi kujinyoa mwenyewe nipe mbinu mkuu.
 
Nenda kwa watalaamu wa ngozi namaanisha Dr watakupa jibu murua ila kwa kuanzia hakikisha unanyoa kwa kufata ulalo wa nywele
 
Tafuta medicated soap...haswa papaya...ni nzuri...ama tumia zile after shave
 
Ukinyoa hakikisha kiwembe kinafata jinsi nywele zilivyolala kuanzia juu kushuka chini..
Na kama kisogoni nywele zako zimezunguka hakikisha kiwembe kifate nywele kadiri zilivyo kwenye mzunguko juu shuka chini.

Hutoona vipele hata siku Moja.
 
Back
Top Bottom