Bima ya afya na paper work kwa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bima ya afya na paper work kwa madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OMEGA, May 10, 2012.

 1. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Nilikuwa sijui jinsi bima ya afya inavyofanya kazi,juzi nilimsindikiza rafiki yangu kutibiwa hospitali moja ya wilaya/mkoa mpya.Nilishangaa mizunguko,mara nenda dirisha lile,ukifika wanahakiki na kujaza form kama tano hivi mtu mmoja inachukua takribani saa nzima,unapewa cheti ,ukiingia kwa daktari uko ndio balaa,ukiwa na bima ya afya daktari anatumia zaidi ya saa nzima kujaza vitabu mbalimbali kabla ya kukuhudumia,akiisha andikia prescription kwenye cheti anarudi tena kwenye register mbalimbali anaingiza entry kwa takribani saa nyingine tena,ukienda kwenye dawa kama kawaida unakuta dawa hakuna,unarudishwa kwa daktari anatumia tena saa nzima kujaza forms mbalimbali kabla ya kukupatia form inayopelekwa kwenye maduka ya madawa yenye makataba na Bima ya afya ili upate dawa bure.Rafiki yangu alikuwa anaumwa kitu simple tu lakini ilimchukua takribani masaa sita kukamilisha taratibu zote na kupewa huduma.Angalizo:Hii bima ya afya inawapunguzia madaktari uwezo wa kuhudumia wagonjwa wengi zaidi kwa siku kutokana na paper work na mabo kuwa monotony,pia sidhani kama ni kazi ya madaktari kujaza ma fomu kibao ya hiyo bima[after all sijui kama kuna posho separate ambayo madaktari wanapewa na Bima ya afya kwa kazi hiyo ambayo nina uhakika haiomo kwenye TOR ya kazi zao,pia BIMA ya afya ni biashara kama biashara nyingine za mifuko ya bima ,aina uhusiano na kazi za madaktari],kwa daktari mwenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 15 kwa siku,kwa utaratibu wa hizo fomu za bima atahudumia wagonjwa 5 tu kwa siku.Hiyo teknolojia wanayotumia ni outdated,ni ya mwaka 47.Inatakiwa wa centralize hiyo system ya bima ya afya na iwe computerized,pawe na data base ambayo inaweza kuwa accesed na hospitali zote nchini,vitu vyote vifanyike haraka na kiteknolojia,haya mambo niliyoyaona yalinikumbusha mbali enzi hizo kabla ya IT haijawepo
   
Loading...