Bima ya afya kutoka Tigo

Bima ya afya kutoka Tigo

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
450
Napigiwa simu na nO 0658 999 345.. dada mmoja anaongea kwamba anapiga kutoka Tigo... na anataka kujua Jina langu.. namjibu kulikoni ..?? anasema kuna Bima ya Afya kwa ajili yangu kutoka Tigo lakin nitaje jina langu.. namwambia kama kweli uko Tigo namba yangu nimeisajili angalia kwenye mitandao yenu mtajua jina langu... dada kang'ang'ania nitaje jina langu !! .........hii ikoje kwa wale wenye kujua majambo.... uatapeli??
 
Ungempa na akaunti yako ya benki pia?
 
Mi nimepata message kuwa namba yangu imepewa ofa ya bima ya afya kwa mwezi mzima wa Aprili. Na nikapewa no niipige kwa maelezo zaidi.
Huwa sipendi kusubscribe kiholela vitu nisivyo na ulazima navyo. Mtu atuelimihe kuhusu hili kwa kweli
 
Hata mimi alinipigia akaongea wee akanipa hadi hospital za kwenda kwa bima ya tigo ila niende kujaza fomu. Nikamkatia simu baada ya kuona ni utapeli tu wa mjini hadi leo hajapiga tena.
 
KIMBEIYE hebu njoo utupatie taarifa nini kilifuata baada ya kujiunga na hii huduma tigo ihusuyo bima?
 
Last edited by a moderator:
kwenye window ya tigo hii huduma ya tigo bima ipo kweli. Ila inawezekana Kuna watu wanatumia hio loop, kutapelia wananchi kuweni makini. Kwa maelezo zaidi inhieni kwenye mtandao wao was tigo ujiridhishe. Hata mm nilipigiwa Sim nikaifatilia nikajiridhisha na nimejiunga. Ila wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza kuwa Sio smart kwenye kurefinancy mtu anapopatwa na majanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwenye window ya tigo hii huduma ya tigo bima ipo kweli. Ila inawezekana Kuna watu wanatumia hio loop, kutapelia wananchi kuweni makini. Kwa maelezo zaidi inhieni kwenye mtandao wao was tigo ujiridhishe. Hata mm nilipigiwa Sim nikaifatilia nikajiridhisha na nimejiunga. Ila wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza kuwa Sio smart kwenye kurefinancy mtu anapopatwa na majanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda Kama Kuna mtu yoyote ambae alishawah kupata majanga yyte tigo bima wakamsaidia aje atoe ushuhuda haapa. Tujiridhishe zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Tigo hawawezi kufanya kazi ya mawasiliano kama ilivyo sasa tangu jana hakuna mtandao, watawrza kazi ya bima? Ndio maana Trump anasemaga ukweli
 
Mimi waliponipigia niliwaomba wanipe muda nitawajibu. Muda huo nikautumia kuulizia customer care ya Tigo kama ni kweli huo utaratibu upo. Walinihakikishia kuwa ni kweli, na nilijiunga. Bahati nzuri sijapata majanga hadi sasa, kwa hilo la kunufaika siwezi kulisemea
 
Back
Top Bottom