BIMA KWA MAGARI YA SERIKALI

BIMA KWA MAGARI YA SERIKALI

Abuka

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
248
Reaction score
243
BIMA KWA MAGARI YA SERIKALI

Ndugu Wazalendo, nawapongeza kwa jitihada mbali mbali za kusukuma gurudumu la Taifa ili nchi yetu iweze kufikia katika uchumi wa Kati kama Dira ya Taifa inavyosema.

Kwa miaka mingi Sasa, utaratibu wa Magari ya Serikali kutolipia bima umezoeleka Duniani kote. Ni utaratibu ambao nchi nyingi Sana zimeamua kuufata ikiwemo nchi yetu ya Tanzania.

Katika kujadili hili napenda nianze na faida za jumla za BIMA ambazo ni pamoja na kulipwa fidia inapotokea ajali, fidia inaweza kuwa ni kwa aliegongwa na gari, au kutengenezwa kwa gari husika au hata kununuliwa gari mpya kulingana na kiwango chako Cha bima.

Hivi karibuni kumekuwa na ajali nyingi Sana za Magari ya Serikali zinazosababishwa na Mwendokasi, ubovu wa barabara pamoja hitilafu mbali mbali zinazoweza kutokea katika vyombo vya Moto.

*Ajali hizi zinapelekea kuharibu Mali za umma na hata kupoteza uhai wa wataalamu wetu mbali mbali.*

Mbali na Magari, barabara zetu pia hutumiwa na raia (ambao ndio wengi zaidi), pamoja na mifugo. Ajali inapotokea barabarani inaweza kuhusisha kimoja wapo au hata vyote.

Sheria inalazimisha gari kuwa walau na kiwango Cha chini Cha bima (hii inaitwa third-party) ili kumlinda anaetembea kwa miguu barabarani pamoja na mifugo.
Mtu akigongwa ataweza kutibiwa na kulipwa fidia na shirika husika la bima.

Gari za Serikali hazina hata hii third-party, hii inamaana gari ya Serikali ikigonga raia au mifugo, hakuna fidia yoyote itayolipwa, zaidi ya muhanga kutafuta namna mbadala ili maisha yaendelee.

*Katika mkutano Mkuu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (Road Safety Ambassadors) uliofanyika miezi michache iliyopita katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma*, nilibahatika kuhudhuria Kama Balozi na takwimu nyingi za ajali barabarani zilionyesha kusababishwa na uendeshaji mbovu wa madereva wetu, hii ikiwa ni pamoja na madereva wa Serikali wanaoongoza kwa spidi Kali barabarani bila kujali maeneo ya makazi ya watu.
Hivyo wahanga wa Magari ya Serikali kutokupewa fidia si Jambo jema Sana hasa ukiangalia chanzo Cha ajali nyingi raia wa kawaida hawahusiki.

*Ushauri/Mapendekezo*

1. Nashauri Magari ya Serikali walau yawe na *third-party insurance kutoka shirika la bima la Serikali.*
Kwa kuwa shirika Ni la Serikali na Magari ni ya Serikali Basi *hiyo pesa haitakuwa imepotea, bado ipo kwenye mzunguko wa Serikali* na zaidi inamlinda muhanga wa Barabarani lakini pia Serikali inayouwezo wa kuipangia matumizi mengine ikiwemo kutoa bonus kwa mashirika yaliyosimamia Magari Yao vizuri bila kusababisha ajali mwaka mzima.

2. Nashauri *madereva wa Serikali waongezewe Ada kidogo kwenye kupata lesseni*, Ada hiyo ya ziada (ambayo Ni kiasi kidogo tu) ipelekwe kwenye shirika la Bima na Serikali ili kusimamia third-party insurance. *Dereva wa Serikali anapokuwa anaendesha gari yoyote tayari lesseni yake iko attached na third-party*, hii Ada inaweza kulipwa maramoja kila baada ya Miaka mitatu (03) yaani kila anapo renew lesseni yake ya udereva.

Utaratibu huu unatumika katika state mbali mbali huko Marekani.

Kwa hapa kwetu Tanzania tumeshuhudia baadhi ya taaluma Kama sheria inayomlazimu muhitimu wa sheria kusoma Tena Chuo Cha Sheria kwa mwaka mmoja kabla hajaruhusiwa kuwa wakili ni utaratibu ambao tumeshauzoea sio kitu kipya.

Kwa madereva wa Serikali kuwa na third-party insurance ya moja kwa moja itasaidia Sana katika kuwalinda raia wanaokutwa na ajali barabarani.

Nawaombeni Sana Wazalendo katika kupita pita huko mjaribu kuliona hili kwa upana wake.

Tuko pamoja katika ujenzi wa Taifa.
Asanteni Sana[emoji120]
 
Nakumbuka Mizengo Pinda alizungumzia sana jambo hili sijui alikuwa anamwambia nani na kwanini halikufanyiwa kazi
 
Billions of money itatoka mkuuu. Potezea tu ingawa DFP zoooote lazima ziwe na Bima. Hayo mengine yasubiri tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom