BIMA (INSURANCE): Uliza chochote kuhusu biashara ya Bima

Ikiwa nilnekata bima ya gari yangu na ikatokea sijawahi kupata ajali au kusababisha ajali yeyote tangu nianze kumiliki hilo gari ..mimi kama mteja wenu nafaidikaje na bima yenu??
 
Ndio inalipa sana kulingana na utafutaji wako wa masoko (marketing). Mawakala hupata commission ya kila bima wanayoikatia. Commission hizo huanzia 10% na kuendelea.

Pia hutofautiana kulingana na aina ya bima iliyokatwa. Kuna magari, moto, wizi na nyingine nyingi.

Nyingine nyingi, zipi hizo?
Huwezi kuzitaja?
 
Mfano namiliki nyumba ya biashara na ambayo nimeikatia bima(hoteli, flem za maduka nk). Swali kwa kuwa siwezi kulipwa kwa wakati, je nitalipwa bima na ile income (faida) ambayo nimeikosa toka janga lilipotokea?
 
Nimjibie mleta mada.Hujaeleza uliikatia bima gani, kama ni moto, theft au burglary, na kama una moja ya bima hizo na ukapata tatizo linalotokana na bima hizo hutalipwa loss of profit, ndiyo maana baadhi ya makampuni yanatoa bima nyingine inayoambatanishwa na hiyo, inaitwa business interruption policy (BI).
 
Ikiwa nilnekata bima ya gari yangu na ikatokea sijawahi kupata ajali au kusababisha ajali yeyote tangu nianze kumiliki hilo gari ..mimi kama mteja wenu nafaidikaje na bima yenu??
Namjibia mleta mada kwa lile nalofahamu.
Bima hukupa faida kubwa mbili; moja ni fidia baada ya uharibifu wa gari yako, kuibiwa gari yako na au kusababisha uharibifu unaotokana na gari yako.

Faida ya pili ni 'peace of mind'. Ile hali tu ya kuwa na bima mathalani 'comprehensive' inakupa amani kuwa gari yako ikipata uharibifu utafidiwa tofauti na yule asiye na bima hiyo. Fikiria Jiji kama la Dar lenye foleni lukuki, ajali za kizembe halafu unapaki gari Kinondoni au Sinza kwenye risk kubwa za wizi wa magari au vifaa vyake halafu unaishi Tandika mahali ambapo hakuna ulinzi wa uhakika halafu huna 'comprehensive insurance cover'!!!
 
Kama nilikata bima kwenye kampuni yenu alafu ikafilisika madai yangu napataje
Nafikiri mfumo wa Bima kwenye ulinzi wa fedha za wateja huwa ni kama Benki. Makampuni ya Bima huwa yanahifadhi au kuweka fedha za bima kwa mfumo wa 'pool' kwa maana kwamba kila aina ya bima ina fungu lake linalojitegemea. Bima za magari zinawekwa tofauti na fedha za bima za moto nk. Na kampuni haziruhusiwi kuchukua risk kubwa kuliko uwezo wa kuzilipa ndiyo maanahuwa kuna nyakati fulani Kampuni moja ikipata biashara kubwa hugawana risk na makampuni mengine na claim inapotokea hugawana fidia kama ambavyo waligawana mapato. Na hufanyiwa auditing na Kamishna wa Bima mara kwa mara.

Hata hivyo pia, Makampuni ya bima nayo hu-insure bima hizohizo kwa Makampuni makubwa ya bima yanayoitwa Re-insurance.
 
Jamaa aliuliza magari ya serikali yanalipiwa bima?????
Ukajibu hapa.
Akuliza wat if yakisababisha ajali???
Hapo sijaona jibu lako
Plz hili ni swali la msingi naomba jibu

Mkuu,magari ya serikali hukatiwa bima na yakisababisha ajali kampunu husika ya bima huwajibika.

Sijui nimekujibu au bado?
 
Kuna suti zangu nazipenda sana nilinunua gharama naweza kukatia bima?
Je naweza kukatia bima nyumba ambayo ipo under construction

Hapana mkuu huwezi kukatia bima hizo suti zako.

Ndio unaweza kukatia bima nyumba ambayo iko under construction, bima yake itakuwa "Contractors all Risks insurance cover"
 
Nafikiri mfumo wa Bima kwenye ulinzi wa fedha za wateja huwa ni kama Benki. Makampuni ya Bima huwa yanahifadhi au kuweka fedha za bima kwa mfumo wa 'pool' kwa maana kwamba kila aina ya bima ina fungu lake linalojitegemea. Bima za magari zinawekwa tofauti na fedha za bima za moto nk. Na kampuni haziruhusiwi kuchukua risk kubwa kuliko uwezo wa kuzilipa ndiyo maanahuwa kuna nyakati fulani Kampuni moja ikipata biashara kubwa hugawana risk na makampuni mengine na claim inapotokea hugawana fidia kama ambavyo waligawana mapato. Na hufanyiwa auditing na Kamishna wa Bima mara kwa mara.

Hata hivyo pia, Makampuni ya bima nayo hu-insure bima hizohizo kwa Makampuni makubwa ya bima yanayoitwa Re-insurance.

Be blessed mkuu, umejibu vyema.
 
Ndio inalipa sana kulingana na utafutaji wako wa masoko (marketing). Mawakala hupata commission ya kila bima wanayoikatia. Commission hizo huanzia 10% na kuendelea.

Pia hutofautiana kulingana na aina ya bima iliyokatwa. Kuna magari, moto, wizi na nyingine nyingi .
Naomba ufafanuzi wa kina kwenye hili swali la je kuwa wakala/broker inalipa?je mtaji unatakiwa huwe na kiasi gani? Na je nipe tofauti kati ya Broker na Agent kiutendaji,kifaida na kimtaji na yupi anatengeneza faida kubwa, swali lingine ukitaka kuwa kati ya broker/Agent vigezo gani vinahitajika,mtaji kima cha chini ni kiasi gani na je utaratibu upoje?
 
Kuwa broker au agent inalipa kutokana na wewe jinsi utakavyopata wateja wengi.
Na tofauti ya agent na broker ni agent anakua chini ya kampuni moja ya bima ila broker anafanya kazi na kampuni nyingi za bima.
Vitu vinavyoitajika kuwa broker http://tira.go.tz/sites/default/files/Requirements -insurance brokers.pdf

Vitu vinavyoitajika kuwa agent http://tira.go.tz/sites/default/files/Requirements for licensing an insurance agent.pdf
 
Asante mkuu. Tupo kuelimishana, well said
 
Je namna gani ya kuanzisha kampuni binafsi la bima!!.. Au yote lazma yawe ya serikali na taasis maalum
 
Back
Top Bottom