mujunimunu
Member
- Jan 27, 2011
- 10
- 1
Heshima mbele,
Natambua kuwa, JF kuna wataalamu na wenye uzoefu mbalimbali. Naomba ushauri namna ya kuanzisha biashara hii.
Natanguliza shukurani
Natambua kuwa, JF kuna wataalamu na wenye uzoefu mbalimbali. Naomba ushauri namna ya kuanzisha biashara hii.
Natanguliza shukurani
Sawa ngoja nijaribu maana mimi si mtaalamu wa Bima ..ninaufahamu kidogo tu.......Insurance Company ndio anayebeba risk na linapotokea tatizo yeye ndio huwa yuko responsible moja kwa moja ........hizi Insurance Company pia huwa zinasaidiwa risk (kwa kiwango Fulani ) na Reinsurance Companies ambazo kazi yake ni kubeba risk kutoka kwenye Insurance Companies..........kwa Tanzania kutokana pengine na nature ya insurance business tuna Reinsurance Company moja tu ambayo ni ya Umma inaitwa TANRE .........
Insurance Companies wanafanya kazi na mawakala wao ambao ni 1) Insurance brokers 2) Insurance Agency ........tofauti ya insurance broker na agency ni kama ifuatavyo ......Insurance broker anapewa leseni ya kuruhusiwa kuhudumia Insurance Company zaidi ya moja .....while Insurance Agency unapewa leseni ya kuhudumia Insurance Company moja tu ..........ingawa baada ya miaka kadhaa insurance agency anaweza kuomba kuongeza Insurance company ila kuna limit ........hata masharti ya kuanzisha insurancy agency na insurance broker ni tofauti .......
Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) ndio mamlaka rasmi ya kusimamia BIMA hapa Tanzania na ndio wanaotoa hizi leseni.....kama kuna maelezo ya ziada kuhusu Bima website yao imetoa ufafanuzi wa kutosha kwa mambo mengi .........
Pamoja mimi binafsi kutokuwa mtaalamu wa Bima lakini kupitia BIMA nimegundua udhaifu mkubwa ktk Financial institution zetu zote kwa mfano......coordination ya mabenki na Bima ni ndogo sana ......kidogo walau siku hizi wameanza kushirikiana ............
Fikiria Kenya kuna Reinsurance zisizopungua tano while hapa ipo TANRE tu ambayo ni ya serikali .........Lakini pia kampuni nyingi za Bima (Insurance Company) zimetokea nje na za wazawa ni chache mno (sidhani kama zinazidi tatu) ........hapo utagundua tuna safari ndefu kufikia walipo wenzetu..........