'Bima gari ya Chenge ilikuwa ya mtu mwingine'
Na Hidaya Kivatwa
OFISA wa Kampuni moja ya Bima ya jijini Dar es Salaam, ameiambia Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kuwa stakabdhi ya bima aliyekuwa nayo waziri wa zamani wa Miondombinu, Andrew Chenge, ilikuwa ni ya mtu mwingine.
Ofisa huyo wa Kampuni ya Scan Insurance and General Services Limited, Raygon Njeje alitoa madai hayo jana, alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi kuhusu tuhuma kwamba Chenge, aliendesha gari bila kuzingatia sheria za usalama barabarani na hivyo kusababisha vifo vya watu wawili.
Njeje ambaye ni wakala wa kampuni hiyo, pia aliiambia mahakama kuwa Chenge hajawahi kuwa mteja wake kama inavyoonyeshwa katika stakabadhi hiyo.
Alidai kuwa stakabadhi hiyo iliyowasilishwa na Chenge, haikuwa ya gari lake na kwamba ilikuwa ya gari aina ya Toyota RAV4, iliyomesajiliwa kwa namba tofauti na ile ya kwake.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, gari hilo ni mali ya Evarist Bigurumba Sesa.
Shahidi huyo alielezea kushangazwa kuhusu stakabadhi hiyo akielezea kuwa kumbukumbu za kampuni hiyo, iliyoko chini ya Kampuni Phoenix of Tanzania Insurance, zinaonyesha kuwa Chenge hayumo katika orodha ya watu waliowahi kukata bima.
"Stakabadhi namba 1919156 ilisainiwa na mimi, lakini ilikuwa ni bima ya gari la Evarist Bigurumba Sesa na si la Chenge. Niliitoa kwa ajili ya matumizi ya miezi mitatu, kati ya Juni 29 mwaka 2007 hadi Septemba 28 mwaka 2007,"alisema Njeje.
"Kamwe hatujawahi kuwa na mteja anayeitwa Chenge na hii stakabadhi siyo yake, ni ya mtu mwingine, kwani namba moja ya stakbadhi haiwezi kutumika mara mbili," alisisitiza.
Ushahidi huo ulitolewa na wakala huyo wakati ambapo Ofisa wa Shirika la Bima la Taifa alikuwa ameiambia mahakama kwamba gari la Chenge, lilikuwa halina bima na hata kampuni iliyokuwa imetoa bima awali ilikuwa ni feki.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Septemba 7 mwaka huu, mahakama itakapotoa uamuzi wa ama mshtakiwa kuwa au kutokuwa na kesi ya kujibu.
Mapema, wakili Simon Mponda anayemtetea Chenge, alikuwa amekanusha vipengele tisa vilivyosomwa mahakamani wakati kesi iliposomwa kwa mara ya kwanza.
Chenge alishtakiwa kwa tuhuma za kutokuwa mwangalifu katika kufuata sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo vya wanawake wawili, Victoria George na Beatrice Constatine, Machi 27, mwaka jana.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Chenge alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hillux Double Cabin na akawa amezidi upande wa njia ya magari ambayo alipaswa kupishana nayo.
Inadaiwa kuwa katika mazingira hayo, aliigonga pikipiki aina ya Bajaj na kusababisha vifo vya wanawake hao.
Source: Mwananchi