Bilioni 7.4 zatumika kuing’arisha Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,702
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kupitia mradi wake wa Uimarishaji wa Halmashauri za Miji – Urban Local Goverement Strengthening Program (ULGSP), umetumia shilingi billioni 7.4 kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zenye urefu wa Km 7.7 ili kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mratibu wa TARURA Mkoa wa Katavi Mhandisi Henry Mtawa wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika Mkoa huo tangu kuanzishwa kwa TARURA.

“Ujenzi huu wa barabara ulianza mwaka 2017 na kukamilika mwaka 2019 na umesaidia kuboresha mandhari ya Mji kama unavyoona hata kipindi cha usiku wananchi wanaendelea na kazi zao kutokana na taa zilizopo”, amesema Mhandisi Henry Mtawa.

Mhandisi huyo ameongeza kuwa, kutokana na mradi huo wakazi wa Halamashauri ya Manispaa ya Mpanda wameondolewa kero ya muda mrefu ya mafuriko katikati ya mji hasa kipindi cha masika, na kupitia mradi huu maji yameweza kutengenezewa njia na sasa hakuna tena mafuriko kwa wananchi.
 
Miji mingi Kwa sasa naona inapendeza sana Kwa Barabara za Lami pamoja na Taa za Barabarani..

Sasa hofu yangu kuu ni; je hii miundo mbinu itakuwa inafanyiwa Periodic maintenance ili ibakie kwenye ubora wake muda wote?
 
Back
Top Bottom