Bilioni 60 zatengwa kufufua kiwanda cha matairi cha General Tyres cha Arusha

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

Aidha Mhe. Charles John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.
 
Chanzo: Mpekuzi
 
SINA Haja Ya Kumaliza Kuusoma Uzi Wako Mleta Huu UZI!!! COZ Kichwa Kinachobeba Uzi Na Na Maelezo Yanasigana Yenyewe!!!! JUU BILLION 60 ZATENGWA (YAANI ZIMESHATENGWA) While Ndani Ya Maelezo Ya Kumnukuu Waziri Husika Anasema "WIZARA YANGU INA MPANGO WA KUTENGA BILLION 60, KWA AJILI YA KUKIFUFUA KIWANDA HICHO " Pumbavuu!!!!! HIZO Ni Story Za Kisiasa Miaka Yote Tunazisikia Tu, BUNGENI Na MAJUKWAANI!!!! NAWE Mleta UZI Unaendeleza Tu Yale Yale!!!
 
Hii ni aibu sana kwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini, maana swali ambalo ilibidi aulize yeye, limeulizwa na mbunge wa arumeru mashariki.
WOOTE Ni Wa CHAMA Kimoja Na Mkoa Mmoja Tu!!! Kikubwa Ni WANANCHI Kupata Ajira, Ambazo Hazitakuwa Za ARUSHA Mjini Pekee!!!! JIPANGE Kujifunza Kujibu Na Kujenga HOJA!!!!
 
Wasikisahau hata kile cha karibu na polyster morogoro kinachomilikiwa na Abood amekibadilisha na kuwa mabanda ya kufugia mbuzi, na kile cha Komoa,
 
WOOTE Ni Wa CHAMA Kimoja Na Mkoa Mmoja Tu!!! Kikubwa Ni WANANCHI Kupata Ajira, Ambazo Hazitakuwa Za ARUSHA Mjini Pekee!!!! JIPANGE Kujifunza Kujibu Na Kujenga HOJA!!!!
maana yangu ni kwamba mbunge wa arusha mjini hajuai matatizo yaliyopo jimboni kwake ni aibu.
 
Unasema hivyo kwasababu inaonekana sio mfuatiliaji mzuri wa yanayojiri Bungeni.

Wimbo namba moja wa Lema umekuwa ni hiki kiwanda, nadhani kwa miaka yote ya awamu ya kwanza ya uwakilishi wake Bungeni....
 
Anatafuta sifa za kijinga badala ya kufanya mambo ya msingi, bora nasari kamshitua maana huo ni wajibu wake..
Nasari yuko serious...huyu Lema ni mtu asiyejua Majukumu yake...amebebwa tu na upepo wa mabadiliko...lakini kwa chadema he is one of many incompetent MPs wa opposition
 
Unasema hivyo kwasababu inaonekana sio mfuatiliaji mzuri wa yanayojiri Bungeni.

Wimbo namba moja wa Lema umekuwa ni hiki kiwanda, nadhani kwa miaka yote ya awamu ya kwanza ya uwakilishi wake Bungeni....
Ila hapo inasomeka swali limeulizwa na mbunge wa arumeru mashariki..leta inayosomeka mbunge wa arusha mjini akilizungumzia hilo, lema ni jipu na linatakiwa kutumbuliwa mapema.
 
Hii ni aibu sana kwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini, maana swali ambalo ilibidi aulize yeye, limeulizwa na mbunge wa arumeru mashariki.
Hayo matairi yakitengenezwa yatatumika Arusha mjini tu ?? Smh
 
Nasari yuko serious...huyu Lema ni mtu asiyejua Majukumu yake...amebebwa tu na upepo wa mabadiliko...lakini kwa chadema he is one of many incompetent MPs wa opposition
He is one among the competent kwenye kambi yao, ndio maana kapewa wizara kivuli ya mambo ya ndani, upepo wa mabadiliko unabeba hata visivyostahili kubebeka...kama lema ni mzigo kwakweli...isingekua ushabiki, huyu mtu hakustahili kurudi bungeni, hana mchango wowote positive kwa jimbo la arusha mjini...
 
Hayo matairi yakitengenezwa yatatumika Arusha mjini tu ?? Smh
Kumbe wale waliokua wakipigania mitambo ya gesi na kila kitu vijengwe mtwara ni kwakua gesi walikua watumie wao wenyewe, shule umekwenda wapi?
 
He is one among the competent kwenye kambi yao, ndio maana kapewa wizara kivuli ya mambo ya ndani, upepo wa mabadiliko unabeba hata visivyostahili kubebeka...kama lema ni mzigo kwakweli...isingekua ushabiki, huyu mtu hakustahili kurudi bungeni, hana mchango wowote positive kwa jimbo la arusha mjini...
yeah inabidi tukubali kwa sababu wananchi ndio wamechagua..imagine garbage nyingine kama msukuma wa geita..naye kabebwa na upepo wa CCM na ukabila kanda ya ziwa
 
Back
Top Bottom