ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,109
- 49,811
Rais Samia anaendelea Kupeleka matumaini Kwa Watanzania wa Ifakara.
Shilingi Bilioni 42 Zinatumika kujenga mradi mkubwa wa kuleta maji mjini Ifakara.
Mji wa Ifakara unapata maji Kwa Asilimia 34 tuu hivyo ujio.wa mradi huu utawezesha Wananchi kupata maji Kwa uhakika.
Hongera sana Rais Samia Kwa kumtua mama ndio kichwani.
---
Mkuu wa Mkoa Morogoro, Adam Malima ametembelea Mradi wa Maji wa Kiburubutu, Ifakara utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 42, ukitarajiwa kukamilika Oktoba 10, 2025.
RC Malima ameeleza kukerwa na baadhi ya watu wanaofanya shughuli za kibinadamu kandokando ya vyanzo vya maji na kueleza kuwa serikali inatumia fedha nyingi katika uendelezaji wa miradi hivyo ni wajibu wa kila mtu kutunza miradi hiyo.
Amesema mpango wa serikali ni kuwahudumia wananchi wa mijini na vijijini wote wapate kwa usawa huduma za kijamii na kwamba uharibifu huo umekua kikwazo kwenye miradi mingi ya maji na kushindwa kutoa huduma kwa wa sababu ya maslahi ya watu wachache.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Ifakara, Mhandisi Ahmad Mpambaike amesema hali ya sasa ya utoaji huduma ya maji katika Mji wa Ifakara ni asilimia 34 na kwamba mradi huo umefikia asilimia 7 ya ujenzi wake, ukisimamiwa na mkandarasi mshauri (Consultant), WAPCOS LIMITED INDIA na Mkandarasi Mjenzi (Contractor) Larsen &Toubro Limited India.