Bilioni 220 zatumika kukimbiza Mwenge mwaka huu 2016

Halafu Rais anakuja kukurupuka mwishoni anaokoa visenti kadhaa vya kuuzia magazeti kuwa rais kaokoa mapesa.
Tangu mwanzo rais alikuwa wapi?
Hizo lugha za kusema Rais kakurupuka sijui unazitoa wapi kila jambo lina mwanzo wake hapa Rais anatakiwa kupongezwa na si kubezwa,hata Baba yako huwezi kumbwambia eti kakurupuka.
 
Hivi nini hasa sababu na faida ya kukimbiza mwenge kila mwaka? Na hiyo miradi inayozinduliwa na mwenge isingeweza kuzinduliwa na waziri husuka? Na inasemekana mahali unapolala mwenge panakuwa ni kitovu cha maambukizi ya ukimwi
 
Kwa hela hizi wangeweza kulipa madeni yote ya mifuko ya hifadhi ya jamii na mifuko ingeendelea kulipa fao la kujitoa la wafanyakazi bila ya Serikali kugombana na wananchi wake
 
mi nahisi una kamzimu flani hatujui, ndo maana unang'ang'aniwa
 
mi wasiwasi wangu watanzania wengi hatujui dhima ya mwenge
hapa ndo pakuanzia ili tuweze kulinganisha FAIDA na HASARA (cost benefit analysis)
anaejua atupe ELIMU YA URAIA kuhusu MWENGE tafadhal
 
Haohao utawasikia kutokana na mbio za mwenge tumefanikiwa kuokoa hela za wananchi kiasi(wataandika tarakimu watakazozipenda wao) .
 
Tarehe 27 mwezi May, mwaka 2014 siku ya Jamanne majira ya saa 4 asubuhi, kwenye kipindi cha maswali na majibu, Naibu waziri wa habari vijana, utamaduni na michezo Juma Nkamia alieleza makadirio ya gharama za kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchini.

Nkamia alisema "serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika.. Mwaka 2012 jumla ya shilingi Bilioni 43 zilitumika ambapo kati ya hizo Bilioni kumi na moja (11) zilitengwa na serikali na Bilioni 32 zilichangwa na mashirika, taasisi, makampuni na wadau mbalimbali walioombwa kuchagia kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru." Taarifa zinaonesha kuwa mwaka 2014 inakadiriwa jumla ya Shilingi Bilioni 120 zilitumika kama gharama ya kukimbiza Mwenge nchi nzima.
CALCULATION.

Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza mwenge nchini (mwaka huu huenda zikaongezeka), zinatosha kufanya yafuatayo;

1. Kununua mashine 60 za MRI na CT Scan kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye kuhitaji vipimo hivyo. Ikumbukwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuna mashine moja tu ya MRI na moja ya CT Scan ambazo zote ni mbovu. Fedha za Mwenge zinaweza kununua mashine 60 za aina hiyo.

Rais Magufuli alijaribu kuhimiza ukarabati wa mashine hizo lakini zilifanya kazi kidogo tu kisha zikafa tena. Kwa sasa hakuna huduma za Vipimo vya MRI Hospitali ya Muhimbili, hadi imefikia hatua wagonjwa wametunga kirefu cha MRI kuwa ni;
-Magufuli -Rudi -Imeharibika tena.

2. Shilingi Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza Mwenge zinatosha kulipia mikopo ya wanafunzi 61,624 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini. Hadi sasa takribani wanafunzi 40,000 walioko vyuoni hawajapata mikopo. Kumbe fedha za Mwenge zingeweza kuwalipia mikopo wanafunzi wote waliobaki na chenchi ikabaki (61624 -40000) x 1,960,000 = 4,238,304,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 4.2

3. Bilioni 120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati 3,870 kwa gharama ya Mil.41 kila Zahanati. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka huu Tanzania ina jumla ya Kata 3,802. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati kila Kata nchini na chenchi ikabaki. (3870-3802) × 41,000,000 = 2,788,000,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 2.7

4. Bil 120 za Mwenge zinatosha kununua Boti 13 za kisasa za majini kama ile ya Bakharesa (Kilimanjaro 5). Ikumbukwe ukiondoa boti za Bakhresa, serikali haina usafiri wa kueleweka wa kwenda Zanzibar. Meli mbili za Mv. Spice Islanders na Mv.Scagget zilizama na kuua maelfu ya watanzania kutokana na uchakavu wa meli hizo. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zingeweza kununua meli mpya za kisasa kwa ajili ya usafiri wa Zanzibar na nchi jirani ktk bahari ya Hindi kama Msumbiji, Comoro na Kenya. Hii ingekua njia ya kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya usafiri majini.

On other hand tungenunua Boti za kisasa tungeweza kupromote utalii wa fukwe (Beach Tourism). Nchi ya Mauritius inaingiza zaidi ya Shilingi Trilioni 10 kwa mwaka (nusu ya bajeti ya Tanzania) kupitia utalii wa fukwe tu. Mauritius hawana Mbuga za wanyama, hawana mlima mrefu kama Kilimanjaro, lakini wanapata Trilioni 10 kwa mwaka kupitia utalii wa fukwe, Tanzania tuna vivutio vya kila aina lakini tunaingiza Trilioni 1.7 tu kupitia sekta ya utalii.

Kwahiyo tukitumia fedha za Mwenge tunaweza kuboresha utalii wa fukwe na kuvutia watalii wengi zaidi na kupata mapato makubwa zaidi kutokana na sekta ya utalii.

5. Bil 120 za Mwenge zikikusanywa kwa miaka mitano (120 bil x 5 = 600 Bil) zinatosha kununua Ndege kubwa za kisasa zipatazo 10 angalau na sisi tukawa na Shirika letu la ndege. Kwa mujibu wa mtandao wa www.aircraftcompare.com bei ya ndege aina ya Boeing 737 yenye uwezo wa kubea abiria 240 ni USD 43 Million sawa na Shilingi za kitanzania Bil.80.
Kwahiyo Bil.600 za Mwenge (kwa miaka mitano) zinaweza kununua ndege kama 10 hivi angalau na sisi tukafufua Air Tanzania yetu tukaanza kushindana na Kenya Airways, Rwandan Air au Ethiopian Airways.

Kwa ujumla yako mambo mengi sn fedha za Mwenge zinaweza kufanya ikiwa zitatumiwa vzr. Hizi nilizotoa ni alternatives chache tu lakini kama viongozi wetu wakiwa makini wanaweza kufanya makubwa zaidi ya haya.

Written By Malisa GJ
Aiseeee ama kweli ule utafiti wa watanzia tunatumia 1% kufikiri nawapa mia yaani bilion 200 na ushehe mara miaka iliyowahi kukimbizwa jama hapa si tunajenga treni za umeme kila mkoa mwee Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
 
Mkesha wa mwenge inadaiwa kuna vitendo vingi vya zinaa hufanyika pamoja na kuvuruga ndoa za watu, tathimini ya gharama za kununua madawa kwa wagonjwa wa ukimwi waliopatikana kwenye mikesha na wa vifua vikuu wanaugua tokana na vumbi linalotimuliwa,muda wa kazi unaosimama kila upitapo, inaweza kuwa kubwa sana. Japo nia ya mwenge kifikra bado ni nzuri, gharama zinatisha. Ni wakati sasa japo kukimbizwa kila baada ya miaka mitano.
 
Halafu Rais anakuja kukurupuka mwishoni anaokoa visenti kadhaa vya kuuzia magazeti kuwa rais kaokoa mapesa.
Tangu mwanzo rais alikuwa wapi?
kaka kuwa na staha ya lugha kwa kiongozi mkuu wa nchi jenga hoja na itetee kwa staha mambo ya kukurupuka rais cjui unapata faraja gani ukishaposti hivyo.
 
Mkesha wa mwenge inadaiwa kuna vitendo vingi vya zinaa hufanyika pamoja na kuvuruga ndoa za watu, tathimini ya gharama za kununua madawa kwa wagonjwa wa ukimwi waliopatikana kwenye mikesha na wa vifua vikuu wanaugua tokana na vumbi linalotimuliwa,muda wa kazi unaosimama kila upitapo, inaweza kuwa kubwa sana. Japo nia ya mwenge kifikra bado ni nzuri, gharama zinatisha. Ni wakati sasa japo kukimbizwa kila baada ya miaka mitano.
kama wewe ni mtu wa zinaa mwenge haukuzuii utaedelea tu.
 
Good analysis. Sio kwenye mwenge tu, yapo maeneo mengi ambapo nchi inatumia gharama kubwa ambayo kama ingekwenda kiuchumu na kimtazamo wa kimaendelo, nchi ingekuwa mbali sana.
 
Tarehe 27 mwezi May, mwaka 2014 siku ya Jamanne majira ya saa 4 asubuhi, kwenye kipindi cha maswali na majibu, Naibu waziri wa habari vijana, utamaduni na michezo Juma Nkamia alieleza makadirio ya gharama za kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchini.

Nkamia alisema "serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na gharama halisi ya wakati husika.. Mwaka 2012 jumla ya shilingi Bilioni 43 zilitumika ambapo kati ya hizo Bilioni kumi na moja (11) zilitengwa na serikali na Bilioni 32 zilichangwa na mashirika, taasisi, makampuni na wadau mbalimbali walioombwa kuchagia kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru." Taarifa zinaonesha kuwa mwaka 2014 inakadiriwa jumla ya Shilingi Bilioni 120 zilitumika kama gharama ya kukimbiza Mwenge nchi nzima.
CALCULATION.

Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza mwenge nchini (mwaka huu huenda zikaongezeka), zinatosha kufanya yafuatayo;

1. Kununua mashine 60 za MRI na CT Scan kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye kuhitaji vipimo hivyo. Ikumbukwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuna mashine moja tu ya MRI na moja ya CT Scan ambazo zote ni mbovu. Fedha za Mwenge zinaweza kununua mashine 60 za aina hiyo.

Rais Magufuli alijaribu kuhimiza ukarabati wa mashine hizo lakini zilifanya kazi kidogo tu kisha zikafa tena. Kwa sasa hakuna huduma za Vipimo vya MRI Hospitali ya Muhimbili, hadi imefikia hatua wagonjwa wametunga kirefu cha MRI kuwa ni;
-Magufuli -Rudi -Imeharibika tena.

2. Shilingi Bilioni 120 zinazotumika kukimbiza Mwenge zinatosha kulipia mikopo ya wanafunzi 61,624 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini. Hadi sasa takribani wanafunzi 40,000 walioko vyuoni hawajapata mikopo. Kumbe fedha za Mwenge zingeweza kuwalipia mikopo wanafunzi wote waliobaki na chenchi ikabaki (61624 -40000) x 1,960,000 = 4,238,304,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 4.2

3. Bilioni 120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati 3,870 kwa gharama ya Mil.41 kila Zahanati. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka huu Tanzania ina jumla ya Kata 3,802. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zinatosha kujenga Zahanati kila Kata nchini na chenchi ikabaki. (3870-3802) × 41,000,000 = 2,788,000,000. Ikabaki chenchi ya Bilioni 2.7

4. Bil 120 za Mwenge zinatosha kununua Boti 13 za kisasa za majini kama ile ya Bakharesa (Kilimanjaro 5). Ikumbukwe ukiondoa boti za Bakhresa, serikali haina usafiri wa kueleweka wa kwenda Zanzibar. Meli mbili za Mv. Spice Islanders na Mv.Scagget zilizama na kuua maelfu ya watanzania kutokana na uchakavu wa meli hizo. Kwahiyo Bil.120 za Mwenge zingeweza kununua meli mpya za kisasa kwa ajili ya usafiri wa Zanzibar na nchi jirani ktk bahari ya Hindi kama Msumbiji, Comoro na Kenya. Hii ingekua njia ya kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya usafiri majini.

On other hand tungenunua Boti za kisasa tungeweza kupromote utalii wa fukwe (Beach Tourism). Nchi ya Mauritius inaingiza zaidi ya Shilingi Trilioni 10 kwa mwaka (nusu ya bajeti ya Tanzania) kupitia utalii wa fukwe tu. Mauritius hawana Mbuga za wanyama, hawana mlima mrefu kama Kilimanjaro, lakini wanapata Trilioni 10 kwa mwaka kupitia utalii wa fukwe, Tanzania tuna vivutio vya kila aina lakini tunaingiza Trilioni 1.7 tu kupitia sekta ya utalii.

Kwahiyo tukitumia fedha za Mwenge tunaweza kuboresha utalii wa fukwe na kuvutia watalii wengi zaidi na kupata mapato makubwa zaidi kutokana na sekta ya utalii.

5. Bil 120 za Mwenge zikikusanywa kwa miaka mitano (120 bil x 5 = 600 Bil) zinatosha kununua Ndege kubwa za kisasa zipatazo 10 angalau na sisi tukawa na Shirika letu la ndege. Kwa mujibu wa mtandao wa www.aircraftcompare.com bei ya ndege aina ya Boeing 737 yenye uwezo wa kubea abiria 240 ni USD 43 Million sawa na Shilingi za kitanzania Bil.80.
Kwahiyo Bil.600 za Mwenge (kwa miaka mitano) zinaweza kununua ndege kama 10 hivi angalau na sisi tukafufua Air Tanzania yetu tukaanza kushindana na Kenya Airways, Rwandan Air au Ethiopian Airways.

Kwa ujumla yako mambo mengi sn fedha za Mwenge zinaweza kufanya ikiwa zitatumiwa vzr. Hizi nilizotoa ni alternatives chache tu lakini kama viongozi wetu wakiwa makini wanaweza kufanya makubwa zaidi ya haya.

Written By Malisa GJ
Mimi naona wange nunua mienge mingi sana ya kutosha kila kata. Ikifika siku ya kuwasha wanawasha kila kata huko waliko wanakuwa na galoni moja ya mafuta ya taa halafu siku ya kuzima wanakutana wote wanazima kwenye kata yao. Nilivyokuwa mdogo nikisoma nailikuwa naamini kuwa mafuta ya mwenge ndio mafuta gharama zaidi kwa kuwa nchi nzima ilikuwa inachangia mafuta ya mwenge. Sasa siku moja mwalimu akawa antuelezea stage za refinary ya mafuta anzia crude mpaka stage ya juu niakwa nasubiria tufike kwenye mafuta ya mwenge. sikuona nikamuuliza mwalimu akanimbia mwenge unatumia mafuta ya taa. Nilichoka kabisa aliponiambia kuwa ni kweli mafuta ya mwenge ndio ghali zaidi.
 
Mh. Rais kama kweli ana nia ya dhati ya kubana matumizi basi mbio hizi za mwenge ziishie kesho tar.14/10/2016. Mbali na hapo atakuwa anahubiri asichokiishi!
 
Back
Top Bottom