Bilioni 20 ambazo Mo aliwapa Simba kama Endowment Fund zinahitaji ufafanuzi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,230
12,733
Kwa ninavyoelewa, endowment fund huwa zinatolewa na matajiri kama msaada. Yaani hiyo pesa inawekezwa na faida anapewa yule mnufaika wa msaada. Lengo huwa na mnufaika kuwa na pato endelevu.

Sasa hiyo 20 ya Mo ilikuwa ni msaada wa Mo kwa Simba au ni kitu gani hasa?

IMG_20220528_195302.jpg
 
Si alishatolea ufafanuzi kuna siku alisema ameweka bond hizo hela faida ndo inatumika kuendesha team tatizo hamfuatilii vitu mnakuwa kama manara vile mnaropoka tu.
 
Si alishatolea ufafanuzi kuna siku alisema ameweka bond hizo hela faida ndo inatumika kuendesha team tatizo hamfuatilii vitu mnakuwa kama manara vile mnaropoka tu.
Akili za hawa watu mkuu ni shida. Kama midume mizima inaomba kupewa mimba na mayele ili imzalie mtoto unafikiri kuna watu hapo?
 
Si alishatolea ufafanuzi kuna siku alisema ameweka bond hizo hela faida ndo inatumika kuendesha team tatizo hamfuatilii vitu mnakuwa kama manara vile mnaropoka tu.
So pesa ni zake ila faida ndiyo inaendeeha timu?
 
Hili swala lishatolewa ufafanuzi na lishaeleweka labda kama kipindi icho aukuwa unafatilia mchakato wa transfomation.
 
Hili swala lishatolewa ufafanuzi na lishaeleweka labda kama kipindi icho aukuwa unafatilia mchakato wa transfomation.
Wewe uliyeelewa hebu tueleweshe sisi tusiojuwa lolote kuhusu Hilo, ndio faida za JF.

Inanikumbusha utotoni nilikuwa nawekewa pesa na mama, Sasa hadi ukubwani MTU akikwambia anakuwekea pesa zako halali hiyo ni zaidi ya dharau kama si utapeli.

Utapeli kama huuu Imani Madega aliukataa Yanga pale Manji alipotaka kuinunuwa Yanga Kwa shilling elfu Saba TU.

Amkeni.
 
Kwa ni navyoelewa, endowment fund huwa zinatolewa na matajiri kama msaada. Yaani hiyo pesa inawekezwa na faida anapewa yule mnufaika wa msaada. Lengo huwa na mnufaika kuwa na pato endelevu...
kunyimwa mkopo wa piki piki umeshakua kama vile chuchunge unachonga sana, kwani mpka saiv ww umeisaidia simba shilingi ngapi?

Sisi hta kama M0 ameichukua simba bure tumeridhika ww nenda ukasifie juhudi uko pengine ukapata uteuzi kumuongelea M0 ni sawa na kutaka kutikisa mbuyu mwisho wa cku matacoor yako ndyo yatatikisika
 
Kwa ni navyoelewa, endowment fund huwa zinatolewa na matajiri kama msaada. Yaani hiyo pesa inawekezwa na faida anapewa yule mnufaika wa msaada. Lengo huwa na mnufaika kuwa na pato endelevu.

Sasa hiyo 20 ya Mo ilikuwa ni msaada wa Mo kwa Simba au ni kitu gani hasa?

View attachment 2242527
Je sisi Team Kilomoni tulipouliza haya mbona mlituletea polisi pale block 41 Kinondoni?
 
Wewe uliyeelewa hebu tueleweshe sisi tusiojuwa lolote kuhusu Hilo, ndio faida za JF.

Inanikumbusha utotoni nilikuwa nawekewa pesa na mama, Sasa hadi ukubwani MTU akikwambia anakuwekea pesa zako halali hiyo ni zaidi ya dharau kama si utapeli.

Utapeli kama huuu Imani Madega aliukataa Yanga pale Manji alipotaka kuinunuwa Yanga Kwa shilling elfu Saba TU.

Amkeni.
Elfu 7 !
 
Buku Saba TU, Madega ni wakili msomi, Wana Yanga mpaka kesho hicho kikokotoo Cha buku Saba Bado hawakielewi lakini ndio ukweli wenyewe.

Ila kwakuwa Simba na Yanga zote Mbili zinamilikiwa na serikali basi Hawa Wahindi na Waarabu ni sehemu tu ya washereheshaji kutupa Raha Ili wafanye biashara bila bughuza lakini hizo timu hakuna mabadiliko yatatokea mpaka mmiliki wa hizo timu yani serikali iamuwe vinginevyo.

Ni lazima muelewe mmiliki wa timu hizo Mbili alizianzisha Kwa malengo yake maalum.
 
Hapana ni za simba ila hazijawekwa direct
Samahani mtaalam! Hebu fafanua kidogo kwa undani. Hizo bilioni 20 ni za simba, ila hazijawekwa direct wapi? Kwenye akaunti ya simba, au!

Kwa hiyo ziko indirect......! Ufafanuzi tafadhali. Maana jambo hili limetugawa sisi mashabiki wa simba.
 
Inawezekana mpaka leo bado simba sio kampuni, hivyo MO bado sio shareholder wa hio kampuni........
hio 'hundi' au tuseme hizo 'pesa' kaweka in 'good faith' kwamba mchakato utakamilika, na ukikamilika basi zitakuwa transfered kwenda kwenye account ya kampuni....

Nadhani kabla hatujamshambulia MO tujiulize swali hili,
Je, shares zingine za simba (hizo 51%) zimeanza kuuzwa? Kama bado ni kwanini?? Hilo litakupa jawabu kwamba mchakato haujakamilika, na MO hawezi kuthubutu kuweka pesa yake!

Matola
 
Hili suala limeibuka tena, I hope taarifa ya mapato na matumizi ya Club ya Simba kwa mwaka 2021/2022 itaonyesha ukweli. Halafu nafikiri wakati umefika Audit Report ya hivi vilabu kuwekwa wazi.
 
Back
Top Bottom