Bili za Maji Zapanda kwa Asilimia 100 Musoma Mjini

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Kweli tunasoma namba Mjini Musoma bili za maji kwa mwezi zimepanda kwa asilimia 100. Mpaka sasa Muwasa wameshindwa kutoa maelezo kwanini bili za maji zimepanda kiasi hicho. Usomaji mita haufanyiki na sasa bili zinatumwa kwa message kupitia mitandao simu bila kutoa maelezo kwa mteja ametumia maji kiasi gani.
Naomba Waziri wa maji ashughulikie hili tatizo kwa haraka kwani itabidii watu wa Musoma mjini waamue kuchukua ndoo na kwenda kuchota maji ziwani kwani kwa sasa hali hii inatisha.
 
Aisee ngoja muisome no. tu nilifikiri huko mlichagua mbunge wenu wa CCM itakuwa ahueni kumbe no. Za kirumi tunasoma wote
 
Safi sana ongera idara ya maji musoma. Ongezeni ili kuongeza mapato kwa maendeleo ya musoma.
 
Waambieni waongezee zaidi ya hiyo 100%. Nyinyi badala ya kupiga kura kwenye mabox ya kura mkakimbilia kupiga deki barabara.
 
Back
Top Bottom