Peter maicko
Member
- Jul 21, 2012
- 12
- 2
Katika ile kesi inayomkabili sheikh ponda ambayo kwa sasa inaendelea kwa kutoa utetezi kwa upande wa washitakiwa,juzi alisimama mzee mmoja aitwae bilal waikela ktk kutoa ushahidi kwa upande wa mshitakiwa.
Mzee huyo mwenye mvi zenyekuonesha kiasi ya chumvi aliyokula alielezea historia fupi juu ya kiwanja cha chang"ombe na bakwata.
Pia alimuelezea mwalimu nyerere juu harakati zake za kuivunja EAST AFRICA MUSLIM SOCIAL WELFARE na kuunda BAKWATAA kama chombo cha Waislamu tz.kwa ufupi ameelezea mengi kuhusu bakwata,serikali na Nyerere.
Nahisi ni bora tukamjua ni nani,anamchango ganiktk kutafuta uhuru na undani ndani wa uwepo wa bakwata na wanachodai waislam juu ya mchango wao ktk uhuru wa nchi wa shutuma zao juu ya serikali zote zilizopita tangu ukolon mpaka uhuru.
Swali la msingi NI NANI BILaL WAIKELA
Nikushukuru sana mzee SAID kwa historia hiyo mujarabu kabisa na sisi vijna tupate jifunza ingawa umeweka kifupi sanaNdugu zangu,
Mimi ninaweza kusema kuwa namjua Mzee Waikela.
Mzee Waikela kabla sijakutananae uso kwa macho 1987 nyumbani kwake
Gongoni Tabora, nilisoma nyaraza zake zilizohusu kile lichokuja kujulikana
kama, ''Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society, (EAMWS),'' wa
mwaka wa 1968.
Nyaraka hizi Mzee Waikela alizikabidhi kwa Muslim Student Association of
Dar es University (MSAUD) nami nilizikuta katika hapo maktaba ndipo
nikapata nafasi ya kuzisoma.
Hizi nyaraka zilikuwa ni barua za EAMWS na ''cutting,'' za magazeti ya kipindi
kile cha kile kilichoitwa mgogoro.
Hizi nyaraka nilielezwa kuwa Mzee Waikela alizileta pale MSAUD kwa lengo la
kwanza zihifadhike na pia zitumike katika kuandika historia ya kweli ya Waislam
wa Tanzania na matatizo waliyokumbananayo baada ya uhuru mwaka wa 1961.
Mwaka wa 1987 nilisafiri hadi Tabora kwenda kumuona na kufanyane majadiliano
kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika yeye akiwa mmoja wa waasisi wa TANU.
Tunakusubiria kwa hamu.Ndugu zangu,

Kweli kabisa ipo haja ya kuongeza nyama zaidi ili tumjue zaidiNikushukuru sana mzee SAID kwa historia hiyo mujarabu kabisa na sisi vijna tupate jifunza ingawa umeweka kifupi sana
Pascal,Tunakusubiria kwa hamu.
P.
Pascal,
Ni vigumu kueleza historia ya Mzee Waikela katika mahali kama hapa JF
kwa ajili ya nafasi.
Kwani historia yake inaanza 1955 wakati wa kuunda TANU Tabora hadi
kufika kupatikana kwa uhuru mwaka wa 1961 yeye akiwa mshiriki mkuu
katika historia yenyewe ya kwanza kuundaTANU na kushiriki katika matukio
makubwa ya wakati ule kama Kura Tatu ya 1958 yeye akiwa kijana.
Mzee Waikela wakati ule alikuwa pia ni kiongozi wa EAMWS akiwa katibu
wa Western Province na mfuasi wa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Hassan
bin Amir.
Nilipokwenda kuonana na Mzee Waikela, hakuwa peke yake aliwaita wazalendo
wenzake, Abdallah Kassongo, Mohamed Mangiringiri na Ramadhani
Singo.
Sijapatapo kukutana wana TANU waliokuwa wanijua historia ya chama chao na
wakaieleza kwa utulivu na ufasaha kama watu hawa.
Baada ya hahojiano haya Mzee Waikela akanita pembeni mimi na walionisindikiza
kwake, marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu na shemeji yake Salum
Mkangwa.
Mzee Waikela alituambia turejee kesho atueleze yale yaliyotokea baada ya uhuru
kuatikana mwaka wa 1961.
Nilirejea na wenyeji wangu siku ya pili na Mzee Waikela alifunguka.
Alizungumza kwa takriban saa tatu sote tukiwa kimya tukimsikiliza.
''Mohamed mimi niliwekwa kizuizini jela ya Uyui mwaka wa 1964 na babu yako, Mkuu
wa Jela akiwa Bwana Munthali na Regional Commissioner akiwa Rashid Kheri
Bagdelleh, ilikuwa mwezi wa Ramadhani na walinifuata usiku kunikamata na ndiyo
kwanza nilikuwa naanza kula daku....''
Mazungumzo yale na Mzee Waikela ndiyo yaliyotengeneza sehemu ya tatu katika
kitabu cha Abdul Sykes na sehemu hiyo nikaipa jina, ''Njama Dhidi ya Uislam (1961 -
1970).
Tulipomaliza mahojiano nilimwambia Mzee Waikela, ''Mzee Waikela umenieleza habari
nzito sana na za kutisha mimi nataka unifahamishe ikiwa unanipa ruhusa ya kukutaja
wewe kwa jina kuwa hizi taarifa chanzo chake ni wewe.''
''Nitaje bila hofu waeleze kuwa hizi habari nimekupa mimi Bilal Rehani Waikela.''
Tulipokuwa tunaagana, Mzee Waikela alinyanyua mikono juu akaniombea dua ndefu
sana na akaniambia, ''Mohamed kitabu kitoke Waislam waujue ukweli wa historia yao
kisiishie katika makaratasi.''
Kokola,Jamani hii mambo ya Waislamu wakati hata Watanzania tu bado haijakaa sawa hivyo kweli tunajitakia heri au shari hapa...? Watu wenyewe sisi mpaka sasa hata maji ya safi hatujaweza kujikimu leo mnataka kuchimba sana haya mambo ya Waislamu au Wakristo kwenye hivi vinchi vyetu uchwara hivyo msidhani hakuna Tai huko juu wanasubiri mianya kama hii kuturudisha kwenye adha ya kutawaliwa au hatuamini kwamba historia hujirudia..? Wacheni mchezo nyie watu weusi mnatatizo gani..? Hamkomi tu..?!! Mmetumikishwa, mmenyanyaswa kupindukia na bado mnanyanyaswa na kudhalaurika lakini eti bado tunataka kuchimba chimba nyufa ili hata kidogo tulichojenga kiwe dhaifu Zaidi. Mwalimu marehemu Ali Mazrui aliwahi andika kuwa Waafrika weusi sio race iliyoteswa kuliko zote duniani maana kuna wengine kama Ma Aborigines na Wahindi wekundu wa bara la Marekani wao waliteswa Zaidi yetu, lakini Mwafrika mweusi ndie pekee Duniani aliedharirishwa kupita mfano!!!! Hebu tuchukue hii iwe dira katika kila tulifanyalo au kulifikiria tujiulize linatusaidiaje kujenga umoja wetu ili utusaidie kutokana na adha hii kama sio leo basi hata vizazi vijavyo. Tufike mahali tuseme imetosha. Hii oh mchango wa Waislamu oh mchango wa Wakristo upuuzi mtupu maana hizo dini zote hazikusaidia ilipofika sisi kuvishwa minyororo na mijeredi nyuma kuelekea utumwani. Wacheni upuuzi hapa.
Najua ni taabu sana kueleza uhuru wa Tanganyika na waliopigania uhuru huu bila kuwataja waasisi wa harakati na maisha yao kwaa ujumla, nakushukuru sana mzee wangu lkn naona kila wakati unapleta ufafanuz kuhusu historia ya nchi hii suala la dini hasa uislam lazima uingie, embu siku ukipta nafasi labda kama na historia pia inauunganisha ukristo na uhuru utueleze kidogo mchango wake ktka uhuru wa TANGANYIKAKokola,
Hapana haja ya kutukana.
Hapana "upuuzi," hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika ipo kwenye
kitabu cha Abdul Sykes na toka kichwapwe sasa ni miaka 20 kipo
madukani kinasomwa na sasa kinakwenda toleo la nne.
Hapajakuwa na tatizo lolote.
Mtu kamuuliza Rehani Waikela ni nani hata Zitto Kabwe afike
nyumbani kwake kumsalimia?
Mimi nimemweleza Waikela kadri ninavyomjua.
Huu si ''upuuzi,'' bali ni historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa
nchi yetu bega kwa bega pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere.
Ni bahati mbaya tu historia hii haikuthaminiwa ndiyo maana leo Waikela
hajulikani na anapta ummarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri.
LKN PIA NATAMANI SANA SIKU NIKIJA DAR NIPATE HATA WASAA NIKUSALIM, NAJUA UNA MENGI SANA YA KUTUFUNZA VIJANA KAMA MIMI HASA LINAPOKUJA SUALA LA HISTORIA YA NCHI YETUKokola,
Hapana haja ya kutukana.
Hapana "upuuzi," hii ni historia ya uhuru wa Tanganyika ipo kwenye
kitabu cha Abdul Sykes na toka kichwapwe sasa ni miaka 20 kipo
madukani kinasomwa na sasa kinakwenda toleo la nne.
Hapajakuwa na tatizo lolote.
Mtu kamuuliza Rehani Waikela ni nani hata Zitto Kabwe afike
nyumbani kwake kumsalimia?
Mimi nimemweleza Waikela kadri ninavyomjua.
Huu si ''upuuzi,'' bali ni historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa
nchi yetu bega kwa bega pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere.
Ni bahati mbaya tu historia hii haikuthaminiwa ndiyo maana leo Waikela
hajulikani na anapata umaarufu baada ya kutembelewa na mwanasiasi
kijana aliye mashuhuri - Zitto Kabwe.
Experience Kleist Sykes katika mswada alioandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 anaeleza kuwa wengi waliokuwa viongozi waasisi wa African Association ni Waislamu kwa kuwa Kanisa likiwakataza waumini wao kujihusisha na siasa. Unaweza kusoma habari hizi katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe (1973).Najua ni taabu sana kueleza uhuru wa Tanganyika na waliopigania uhuru huu bila kuwataja waasisi wa harakati na maisha yao kwaa ujumla, nakushukuru sana mzee wangu lkn naona kila wakati unapleta ufafanuz kuhusu historia ya nchi hii suala la dini hasa uislam lazima uingie, embu siku ukipta nafasi labda kama na historia pia inauunganisha ukristo na uhuru utueleze kidogo mchango wake ktka uhuru wa TANGANYIKA
shukrani jazzzakalahu kheir maali, niliuliza swali hili kusaidia wengine pia wapate elewa mchango wa uislam ktk uhuru. Mie nshashibisshwa muda sana nawe na ;ia na makongamano ya al marhum Sheikh HASSAN ILUNGA KAPUNGUExperience Kleist Sykes katika mswada alioandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 anaeleza kuwa wengi waliokuwa viongozi waasisi wa African Association ni Waislamu kwa kuwa Kanisa likiwakataza waumini wao kujihusisha na siasa. Unaweza kusoma habari hizi katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe (1973).
TANU ilipoasisiwa 1954 Kanisa Jimbo la Kusini likiwakataza waumini wake wasijiunge na TANU wakisema kuwa Waislam wanataka kuleta Vita ya Maji Maji kama walivyofanya 1907 dhidi ya Wajerumani.
Mwaka 1955 ukatumwa ujumbe uje TANU HQ ionane na uongozi wa juu wa TANU ili Nyerere aende Lindi akaeleze ukweli.
Waliokuja Dar es Salaam alikuwa Ali Mnjale na Salum Mpunga.
Nyerere alikwenda Lindi akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani.
Sina uwezo mimi wa kubadili historia hii.
Mkuu Maalim, Mohamed Said, kuna vitu unaeleza vinaumiza moyo na fikra na kuacha maswali bila majibu!.Pascal,
Ni vigumu kueleza historia ya Mzee Waikela katika mahali kama hapa JF
kwa ajili ya nafasi.
''Mohamed mimi niliwekwa kizuizini jela ya Uyui mwaka wa 1964 na babu yako, Mkuu
wa Jela akiwa Bwana Munthali na Regional Commissioner akiwa Rashid Kheri
Bagdelleh, ilikuwa mwezi wa Ramadhani na walinifuata usiku kunikamata na ndiyo
kwanza nilikuwa naanza kula daku.....''
Kokola,