Rutunga M
JF-Expert Member
- Mar 16, 2009
- 1,769
- 1,390
MASWALI MAWILI YA MSINGI KUHUSU UBUNGE EALA.!
By Malisa GJ,
[HASHTAG]#Swali1[/HASHTAG]: Uchaguzi wa wabunge wawili wa EALA kupitia Chadema utafanyika lini?
[HASHTAG]#Jibu[/HASHTAG]; unapaswa kufanyika muda wowote haraka iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu wabunge waliochaguliwa jana (wa CCM na CUF) hawawezi kuwa HALALI mpaka pale wabunge wa Chadema watakapopatikana na kutimia 9.
Mkataba wa Afrika Mashariki (Ibara ya 50) na sheria ya uchaguzi wa wajumbe wa bunge la Afrika Mashariki ya mwaka 2011 zinapiga MARUFUKU nchi mwanachama wa EAC kupeleka wabunge wasiotimia 9 kwenye bunge la EALA. Kwa maana hiyo wabunge waliochaguliwa jana hawawezi kuapishwa, hawawezi kushiriki kikao chochote cha EALA, hawawezi hata kutambulishwa hadi wabunge wawili wa Chadema wachaguliwe ili watimie 9.
Kwa mantiki hiyo, uchaguzi wa wabunge wawili wa Chadema unapaswa kuitishwa haraka iwezekanavyo.
[HASHTAG]#Swali2[/HASHTAG]: Je wagombea waliokataliwa jana wanaweza kugombea tena?
[HASHTAG]#Jibu2[/HASHTAG]: Kwanza ieleweke kuwa kuna "loophole" ya kisheria kwenye kanuni, kwa sababu tukio lililotokea jana halijawahi kutokea wakati mwingine wowote tangu kuanzishwa kwa bunge la EALA. Hata hivyo hakuna popote ambapo kanuni zinazuia mgombea aliyekataliwa awali kugombea tena. Hivyo Masha na Wenje wanaweza kuruhusiwa kugombea tena ikiwa tu Chadema itaongeza jina la mgombea/wagombea wengine. Unless CCM waamue kucheza na kanuni.!
Malisa GJ