Bila mbeleko ya dola hakuna CCM

Bila mbeleko ya dola hakuna CCM

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,743
Reaction score
1,164
CCM imechoka sasa kuliko wakati wote toka kuumbwa kwa dunia hii. Simba akizeeka hukimbilia kwenye vyanzo vya maji kuvizia wanyama wadogo wadogo, kutokana na kukosa nguvu ya kupambana katika mawindo yake.

CCM inavizia kwenye kurudisha fomu, kupora fomu na kupitisha wanaCCM bila kupingwa kuwa viongozi wa wananchi, na kuikanyaga mamlaka ya wananchi kwa mujibu wa katiba.

Imepoteza imani yake kwa wapiga kura kwa kushindwa kufanya siasa za ushindani wakitegemea mbeleko ya kupita bila kupingwa.

Ziko sababu zilizo pelekea kufanya yanayo fanyika katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa kama ifuatavyo:

1. Pamoja na serikali kupitia mwenyekiti wa CCM Taifa kuzuia vyama vingine kufanya siasa za wazi ilihali wao wana fanya, mwitikio wa wananchi kupinga siasa za kibaguzi umekuwa mkubwa sana kuliko wakati wowote na kuviimarisha vyama vya siasa vya upinzani kuliko wakati wowote.

2. CCM na serikali yake kushindwa kuhimili mnyukano wa hoja ikitegemea zaidi kubebwa na nguvu ya dola jambo linaloiweka nchi kwenye hali tete.

Ndo maana mawaziri wake wamekuwa wapiga ramli kwa yanayotokea, wakifikirishwa zaidi kujihami katika kulinda dhamana zao.

Waziri mzima ana thubutu kutamka ole wao wapinzani walio amua kujitoa kwenye uchaguzi, wakitegemea kufanya vurugu. Serikali imejipanga kuwadhibiti kwa nguvu kubwa. Lakini amesahau kuwa walio paswa kushughulikiwa kwa nguvu kubwa ni wale walioitwa Ikulu na kupewa maelekezo ya kuvuruga uchaguzi wa kidemokrasia.

3. Pamoja na serikali kufanya matumizi yasiyo rasmi ya kununua madege kama wanavyoita wao, hali ya Watanzania kiuchumi, kijamii na kiusalama haiko sawa kabisa.

Tumeona deni la Taifa likipaa kila kukicha, lakini hospitali hazina dawa. Tumeaminishwa elimu bure lakini michango inazidi utayari wa elimu bure.

Mzunguko wa uchumi wa chini umepotea na serikali kuwatumia wataalamu kupika takwimu kwa malengo ya kuiaminisha dunia.

Hali ya usalama ni tete kwa maskini, na hata matajiri. Kama hujatekwa utafunguliwa kesi ya kutakatisha fedha ili tu kukodhoofisha uchumi katika kutimiza lengo la Watanzania waishi kama mashetani.

Usalama unaolinda uchumi wa mtu mmoja mmoja umepotezwa kwa makusudi.

4. Kwa kuwa mikutano ilizuiliwa kwa muda mrefu, uchaguzi ndiyo jukwaa pekee la kufanya mikutano ya hadhara, ambayo Watanzania wengi watasikia maovu ya serikali na kupata mrejesho wa yanayofanyika ndani ya serikali, bunge na Mahakama.

Kupitisha wagombea wa bila kupingwa wawe viongozi wa wananchi, ni zuio lingine la vyama vya siasa kufanya kampeni na mikutano ya hadhara.

Ndiyo maana mkakati huu ukiuchunguza kwa kina utaona hauna lengo zuri kwa mshikamano wa kitaifa. Haikijengi CCM zaidi cha kukifanya kuwa chama Cha Majambazi, maana wenye tabia ya kupora ni majambazi.

#Ukimsikiliza waziri mwenye dhamana na TAMISEMI utasema wana nia njema, lakini kinacho fanyika na watendaji walio chini yake (WEO 's) ambao ndiyo wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ambao waliitwa ikulu na mwenyekiti wa CCM,kwa dhamana ya urais ambao TAMISEMI iko chini ya ofisi hiyo, na ukimya wa serikali kwa uhuni unaofanywa na watendaji hao, utaona wazi huu ni mkakati toka ikulu.

Waziri kuwataka waliokatwa kupeleka rufaa zao kwa waliowakata ni matumizi mabaya ya rasilimali muda, huo ni uhuni kama ulivyo uhuni unaofanywa kukandamiza demokrasia nchini.

Chokochoko hizi haziisaidi serikali zaidi ya kuzidisha hali tete ya usalama nchini. Kwa kuwa wenye mamlaka ya kuziweka serikali kwenye madaraka (wananchi) wameporwa haki yao ya kikatiba, wamepewa watendaji wa kata.

History inatueleza chokochoko zote kwenye mataifa mengi husababishwa na ukosefu wa huduma bora na chaguzi za kihuni kama huu wa TAMISEMI, ambazo husababisha serikali nyingi kuondolewa madarakani, kwa hali hii sasa rasmi CCM imechoka kutawala.

Mwalimu Nyerere alisema "bila CCM madhubuti nchi itayumba " ni kweli nchi inayumba, chaguzi si za haki wala huru. Matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi haziakisi maisha ya Watanzania.

Umadhubuti wa CCM aliyoifikiria Mwalimu ni ile yenye kuheshimu demokrasia, yenye kuwasikiliza Watanzania wanataka nini, si unataka nini ,ni ile yenye kuheshimu na kuitumia katiba kama mwongozo. Lakini leo imepoteza ideology yake kabisa, chama hakiamini katika ustaarabu tena, ndo maana nchi inayumba.

Kauli hii ya Mwalimu imegeuka fumbo la imani, linawatesa kutafuta uhalali wa kubaki madarakani kwa njia yeyote ile. Lakini wameshindwa kuheshimu kuwa Tanzania ni ya Watanzania, vyama vitapita nchi itabaki.
 
Mwisho wa Ulaghai wa CHADEMA na genge lake!
 
Hahaaaaa nacheka sana nionapo haya maana hapo kale kulikua na dola zenye nguvu km roman empire na hata juzi tu dola ya kinazi lakini leo wako wapi .....dunian tunapita tu tuache alama njema sio za kuumiza watu mkuu
Narudia tena kwa mara ya mia tano, CCM sio Chama Dola bali CCM NDIO DOLA yenyewe. Mengine yote ni mbwembwe na michezo ya kuigiza
 
M
Hahaaaaa nacheka sana nionapo haya maana hapo kale kulikua na dola zenye nguvu km roman empire na hata juzi tu dola ya kinazi lakini leo wako wapi .....dunian tunapita tu tuache alama njema sio za kuumiza watu mkuu
Mifano yote inayotolewa kuhusu mabadiliko na kurejesha nguvu kwa wananchi ni mifano kutoka nchi za Ulaya. Afrika tangia enzi za kina chief Mangunga wa Msowero, kina Bushiri waliokua wakisaidiana na Tipu Tip kuuza ndugu zao utumwani na wengineo wamefanya nini wao wenyewe kujikomboa?

Kina Mobutu walichokwa na mabeberu ndio ikatokea mabadiliko, Gadafi hakua na shida ila tulimuona mbaya kwa context ya hao mabeberu! Kwa ujumla hakuna tutakaloweza kufanya zaidi ya kusubiri fate ichukue mkondo wake

Kauli za kuuliza dikteta fulani yuko wapi sasa hivi ni kauli za uwoga na zakukata tamaa maana kama ni uharibifu utaendelea mpaka muhusika achoke na amalize umri wake wa kuishi aliopangiwa na Mungu hapa duniani kisha wanaojiita wana historia waibuke na kusema "Unamuona dikteta fulani yuko wapi sasa?" huku akiwa kafanya uharibifu wa kutosha kabisa
 
Mm ni mwana ccm ila kinacho ni shangaza ni kwamba Chadema wamejitoa kwenye uchaguzi ila Ccm bado wapo bize kuwazungumzia wakati wenzao wameshajitoa mda sasa uoga wa nini kwetu sisi wana ccm
 
Naom
Mkuu ustaarabu ndo ulianzia kwao hao mabeberu na sisi kwa haya yanayofanyika tutafika mahara haki zetu tutazidai kwa njia yoyote na huko ndo watawala wanataka watu wafike
Naomba Mungu ili akili ziwakae sawa mapema na wachukue hatua maana tatizo mambo yakisha haribika inakua vigumu kurudia kama mwanzo na inakua ni majuto tu
 
Naom

Naomba Mungu ili akili ziwakae sawa mapema na wachukue hatua maana tatizo mambo yakisha haribika inakua vigumu kurudia kama mwanzo na inakua ni majuto tu
Wanahangaika kuwataka wale waliopitishwa toka upinzani wagombee bila mwamvuli wa chama, yaani ukiwa diktekta unajiona Mungu, unaweza kusema iwe ikawa, hiyo sheria ya wagombea binafsi imepitishwa lini?
 
Nakupongeza sana mleta uzi, umeandika mambo ya maana sana!
Magufuri toka akiwa mbunge alikuwa anatumia mbinu hizi hizi za kupita bila kupingwa kwa kuwahonga washindani wake. Kwa mbinu zake hizo ameendelea kuwanunua akina waitara lakini ameshindwa kuudhofisha upinzani.
 
Nakupongeza sana mleta uzi, umeandika mambo ya maana sana!
Magufuri toka akiwa mbunge alikuwa anatumia mbinu hizi hizi za kupita bila kupingwa kwa kuwahonga washindani wake. Kwa mbinu zake hizo ameendelea kuwanunua akina waitara lakini ameshindwa kuudhofisha upinzani.
Lazima tukemee kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom