Bila maandamano kwa tz, haki tusahau???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila maandamano kwa tz, haki tusahau????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lusambara, Jul 29, 2011.

 1. L

  Lusambara Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg zangu wana JF, binafsi nakubaliana na wabunge wa CDM wanaosema kuwa maandamano ni lazima ili haki ipatikane. KUSEMA UWELI Kila mahali ambapo maandamano na migomo imefanyika, mabadiliko yametokea na kiasi fulani haki imepatikana.


  Jana niliangalia watoto wa S/M Minazi mrefu walipoandamana ili kudai kuwekewa matuta kwenye barabara, Matuta hayo kwa vile wameandamana, utaona yanawekwa mara moja. Wale madereva wa malori kule Tunduma walipogoma na kuandamana, haki imeanza kupatikana. Wanafunzi walipogoma na kudai nyogeza kwenye posho ya chakula, tayari serikali imeanza kulifanyia kazi na kiasi fulani kimeongezwa hata kama ni kidogo lakini ni majibu, Daladala Morogoro walipogoma na kuandamana kudai haki yao, nao wamesikilizwa nk. HIVI KWELI SERIKALI YA CCM NI SIKIVU KAMA INAVYOSEMWA KWELI???????????? MBONA MAHALI PENGI INASIKIA BAADA YA MAANDAMANO KUFANYWA??? INA MAANA INAPENDA WATU WADAI HAKI YAO ZAIDI KULIKO UTULIVU.

  Hynes amesema kuwa bado maandamano hayajafanyika na inayofanyika ni pasha joto tuu.

  HAKI YA TANZANIA INAPATIKANA KWA MAADAMANO NI LAZIMA TUIDAI NA TUANDAMANE

  FIKIRI HILI

  Mtu mmoja ni Mstarabu sana na wala hapendi fujo anapenda utaratibu katika kila jambo, ila ni mwizi na anakumbatia wezi na mafisadi wa rasilimali za nchi.

  Na wa pili ni Kichaa, kazi yake ni kupiga kelele ili watu wapatiwe haki zao, Mafisadi wakamatwe na wafungwe na rasilimali za nchi zisiibwe bali zitumike kwa manufaa ya wote.

  KATI YA HAO WAWILI YUPI NI BORA???
   
 2. Jigsaw

  Jigsaw JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,817
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mkuu si utaje tu majina ya watu hao wawili ili tumalize moja kwa moja?
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Wa pili nitampenda zaidi na zaidi
   
 4. L

  Lusambara Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo yamesemwa leo ikiwa ni ulinganifu kati ya Wabunge wa CCM na CDM. Mbuge wa ILEMELA ametumia mifano hiyo kuonyesha utofauti uliopo. AMESEMA HAKI YAKE NA UBUNGE WAKE NI MATOKEO YA MAANDAMANO, HIVYO KWAKE MAANDAMANO NI BABA NA MAMA, KAMWE HAWEZI KUDHARAU MAANDAMANO
   
 5. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hata mimi naamini,bila maandamano na migoma hatuwezi kupata haki zetu tz.
  Viongozi wameshiba,hiyvo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Maandamano ni Jawabu!
   
Loading...