Bila kutambua Kikwete ameibua Utanganyika!

Bila kutambua Kikwete ameibua Utanganyika!

Hii kero ya Watanganyika kuitwa wahamiaji haramu kule Zanzibar wakati ikiwa nchi moja huku Wazanzibar wakiwa wahamiaji halali huku bara si la kubeza. Naona CCM wamechoka Amani na hili wanaloliona dogo ndicho kitakuwa chanzo cha kuvunja amani. Dawa hapa ni serikali moja tu basi
 
Watanganyika wanashangaa kwa rais kuwatenga wazanzibar kwa sababu ya kujijengea uwezo.
Hii ni hatua ya kwanza ya ubaguzi. Watanganjika tusongeni nasi mbele ya Mungu ....maana wanajitenga hao.
 
umeandika ukweli sana , Tanganyika haitapotea kamwe ! CCM WANADHANI MUUNGANO NI WA VIONGOZI , KIKWETE ameboronga vibaya sana !

Nina uhakika hamjamuelewa vyema huyu mzee. Unayoyawaza hakika ndivyo alivyomaanisha na ndiyo mawazo na nasaha zake. Alitaka kuwafunulia pazia lote muamue wenyewe. Tafsida mkuu wangu. Au hamjakaa uswahilini?
 
Zanzibar kuwa na bendera, kuvunja katiba na kujiita nchi kwa tanganyika eti hiyo sio kero. Kuzungumzia kuvunja muungano nakubaki na nchi mbili kwa amani utaonekana kama unataka kupindua nchi. Naomba watanzania tuache uoga wa mambo mapya.

sio utani. cha ajabu nilijikuta nalia kama msiba nilipoulizwa nilijikuta nimeropoka; "nalilia Tanganyika"
 
Kikwete ana tatizo na serikali tatu!
Ametumia muda mwingi kuzungumzia changamoto za serikali tatu na kutaka kutuaminisha kuwa hazina majibu wakati kwa upande wa pili anaonyesha changamoto za serikali mbili ni chache na zipatiwe majibu kupitia mchakato huu na majibu yenyewe ni kuipa zanzibar inachotaka kila wanapodai au kujenga uwezo.Yaani ni kama vile serikali mbili ni mpango maalumu wa kuilea zanzibar mpaka itakapokuwa dola.

Kikwete mnamlaumu nini tena? Alikuwa anawafunulia mianya iliyofunikwa muamue moja. Hapa ni serikali moja au tatu. Na ameonyesha disadvantages na advantages za kila upande na ambazo zimeonyesha wazi kuwa Zanzibar ndio losers ikitokea hii boma imemeguka.
 
Kwa hali hii na huo muungano na usiwepo tu Tanganyika haiwezi kuwa looser wa kila kitu hatuwezi ujinga huo wa manufaa ya CCM.
 
Sijawahi kujisikia mtanganyika kama nilivyojisikia leo hii wakati nikisikiliza hotuba ya rais Kikwete.

Ni hotuba iliyoibua hisia za utanganyika zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Hotuba yake imeitetea Zanzibar kwa kiasi kikubwa na kuionyesha Tanganyika ni wakandamizaji dhidi ya wanzanzibari kitu ambacho si kweli,hotuba imeonyesha kuwa zanzibar ina haki ya kupata favour inayopata bila kujali Tanganyika haina favour wala haki yoyote katika muungano!

Iweje Zanzibar waulizie hisa zao katika serikali ya muungano huku hakuna anayeuliza hisa za Tanganyika katika muungano?

Iweje Zanzibar iulizie haki za kuendesha biashara,bandari,mafuta n.k huku Tanganyika tumefumba mdomo?

Iweje zanzibar iogope kumezwa huku Tanganyika haijulikani ilipo?nani aliyeimeza zanzibar?kwa nini zanzibar iendelee kutetea uzanzibar wake wakati muungano ni wa kidugu?kwa nini wahehe hawatetei dola yao ya kihehe?kwa nini wamasai hawatetei dola yao ya kimasai dhidi ya kumezwa ndani ya Tanganyika?n.k n.k n.k!

Naamini hakuna muundo wa muungano usiokuwa na changamoto!anachokitetea mh rais ni uwoga wa kukumbana na changamoto au kwa lugha ya wazi kuvunjika kwa muungano au mahusiano.

Lakini ni kwa nini tuishi kwa kuogopa?nani anayetutisha?je ni watanganyika ambao hawapo?

Nimepata mkanganyiko,majonzi na utaifa wa kitanganyika.

Naona mh rais anatoa suluhisho la chokochoko za muungano ni kuwapa wazanzibari wanachokitaka kila baada ya muda au kila baada ya kujijengea uwezo wa kuhandle mambo yao,leo wanaweza kusajili magari tuwape,kesho wanaweza kusimamia mafuta na gesi tuwape na hatimaye wakimudu kusimamia ulinzi na usalama tutawapa?
Kuna msemo unasema ''GIVE HIM AN INCH HE WILL NEED A MILE" yaani leo tumewapa kidogo kesho watataka kikubwa.
Kuna siku wazanzibari watasema Dar,Tanga,Mafia,Pwani,lindi,mtwara na Morogoro ni vipande vya zanzibar havina budi kurudishwa....tutawapa?

Where is my Tanganyika?kwa nini Mmasai,------,mjita,muha,mkaguru,mmakonde na wengine wengi wanaendelea kutambulika huku miongo kadhaa imepita baada ya kuunganishwa chini ya mwamvuli wa utanzania?

Ama kwa hakika leo mh Rais kaibua hisia zangu za UTANGANYIKA!

Pole sana mitz mingi ni mijuha, akili hamna yaani nhzemba kagulu ndio anaakili pamoja na minyinyiem yake, wengi kazi yao kupiga makofi kama kunguru anagombea mizoga
 
Back
Top Bottom