meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,832
Sijawahi kujisikia mtanganyika kama nilivyojisikia leo hii wakati nikisikiliza hotuba ya rais Kikwete.
Ni hotuba iliyoibua hisia za utanganyika zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
Hotuba yake imeitetea Zanzibar kwa kiasi kikubwa na kuionyesha Tanganyika ni wakandamizaji dhidi ya wanzanzibari kitu ambacho si kweli,hotuba imeonyesha kuwa zanzibar ina haki ya kupata favour inayopata bila kujali Tanganyika haina favour wala haki yoyote katika muungano!
Iweje Zanzibar waulizie hisa zao katika serikali ya muungano huku hakuna anayeuliza hisa za Tanganyika katika muungano?
Iweje Zanzibar iulizie haki za kuendesha biashara,bandari,mafuta n.k huku Tanganyika tumefumba mdomo?
Iweje zanzibar iogope kumezwa huku Tanganyika haijulikani ilipo?nani aliyeimeza zanzibar?kwa nini zanzibar iendelee kutetea uzanzibar wake wakati muungano ni wa kidugu?kwa nini wahehe hawatetei dola yao ya kihehe?kwa nini wamasai hawatetei dola yao ya kimasai dhidi ya kumezwa ndani ya Tanganyika?n.k n.k n.k!
Naamini hakuna muundo wa muungano usiokuwa na changamoto!anachokitetea mh rais ni uwoga wa kukumbana na changamoto au kwa lugha ya wazi kuvunjika kwa muungano au mahusiano.
Lakini ni kwa nini tuishi kwa kuogopa?nani anayetutisha?je ni watanganyika ambao hawapo?
Nimepata mkanganyiko,majonzi na utaifa wa kitanganyika.
Naona mh rais anatoa suluhisho la chokochoko za muungano ni kuwapa wazanzibari wanachokitaka kila baada ya muda au kila baada ya kujijengea uwezo wa kuhandle mambo yao,leo wanaweza kusajili magari tuwape,kesho wanaweza kusimamia mafuta na gesi tuwape na hatimaye wakimudu kusimamia ulinzi na usalama tutawapa?
Kuna msemo unasema ''GIVE HIM AN INCH HE WILL NEED A MILE" yaani leo tumewapa kidogo kesho watataka kikubwa.
Kuna siku wazanzibari watasema Dar,Tanga,Mafia,Pwani,lindi,mtwara na Morogoro ni vipande vya zanzibar havina budi kurudishwa....tutawapa?
Where is my Tanganyika?kwa nini Mmasai,------,mjita,muha,mkaguru,mmakonde na wengine wengi wanaendelea kutambulika huku miongo kadhaa imepita baada ya kuunganishwa chini ya mwamvuli wa utanzania?
Ama kwa hakika leo mh Rais kaibua hisia zangu za UTANGANYIKA!