DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Kuanzia leo Julai 1, 2025, huduma ya Mabasi ya Mwendokasi jijini Dar es Salaam imesitisha rasmi matumizi ya tiketi za karatasi kwa abiria wa kawaida na kuanza kutumia mfumo wa kadi maalum zenye salio.
Abiria sasa wanatakiwa kuwa na kadi hizo, zitakazopatikana katika kwa shilingi elfu moja na kujazwa salio katika vituo mbalimbali vilivyokuwa vikitoa tiketi.
Hali hiyo imeibua mtazamo tofauti kwa baadhi ya abiria, hususan maeneo ya Morogoro Road, ambao wamedai hawakufahamu kuhusu mabadiliko hayo mapya. Wengine wamesema mfumo huo mpya unaweza kuwa changamoto kwa wananchi wa kipato cha chini.
Wafanyakazi wa vituo vya Mwendokasi wameeleza kuwa tiketi za karatasi zitaendelea kutumika kwa wanafunzi pekee. Vituo kama Mbezi Mwisho, Kibanda cha Mkaa, Kwa Msuguli, Temboni, Suka na Stop Over vimewekewa mashine maalum za kuskani kadi.
Chanzo:Nipashe