Bila Elimu ya Sayansi hakuna Kilimo Kwanza: Kawambwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Bila Elimu ya Sayansi hakuna Kilimo Kwanza: Kawambwa
Tuesday, 14 December 2010 20:56

Minael Msuya na Emakulata Peter

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema, azimio la ‘Kilimo Kwanza' haliwezi kufanikiwa kama elimu ya sayansi haitaimarishwa. Dk Kawambwa alitoa kauli hiyo jana, katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo ,Selestine Gesimba, katika sherehe ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa sekondari waliofanya vizuri somo la Kemia. Dk Kawambwa alisema, elimu ya sayansi inatakiwa kutolewa kuanzia ngazi za msingi, sekondari na vyuo vikuu ili kuimarisha taaluma hiyo.

"Serikali ilitangaza azimio la Kilimo Kwanza na kulipa kipaumbele katika kuleta maendeleo ya Taifa, lakini haya yote hayawezi kufanikiwa pasipo kuimarisha elimu ya sayansi kuanzia mashuleni hadi vyuo vikuu'" alisema. Aidha, Dk Kawambwa alisema mafanikio ya kuboresha elimu ya sayansi yatafikiwa iwapo wadau mbalimbali wataungana na serikali na kuweza kusukuma maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.

Kwa mujibu wa Dk Kawambwa wizara yake itahakikisha tatizo la maabara na uhaba wa vifaa katika shule za kata linamalizika na kuwa wanafunzi watakuwa wanasoma kwa nadharia.

Kwa upande wake Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Matata aliwashauri wanafunzi kupenda kusoma masoma ya sayansi kwa kuwa ni marahisi na kwamba wasikimbilie masomo ya sanaa wakadhani kuwa ni mepesi. "Kuna vijana wengi wanakimbilia masomo ya sanaa wakidhani kuwa ni mepesi, sio kweli kabisa wanajidanganya hakuna somo jepesi kama la sayansi kwa kuwa kwanza unafanya na kusoma kitu unachokiona mwenyewe," alisema. Aliongeza kuwa, Ofisi ya Mkemia mkuu kwa kushirikiana na wizara ya elimu itajitahidi kuwawezesha na kutoa fasili nzuri katika maabara ili wanafunzi watakaoingia katika mchepuo wa sayansi wasome kwa urahisi.
 
Kawambwa naye asituchanganye....kwani kilimo siyo sayansi?........................kama ni sayansi huku kutofautisha kwatoka wapi?
 
Tatizo la wanasiasa wanaongea tu na wala hawatekelezi, walimu wenyewe wa sayansi hakuna sasa sijui nani atwafundisha wanafunzi hiyo sayansi. Pia hizo shule za kata zenyewe hata tu madarasa hayatoshi na walimu ndo hakuna kabisa ukilinganisha na shule za mijini.
 
Back
Top Bottom