Bil. 43/- kulipa wakulima pamba mwisho wa mwezi

Bil. 43/- kulipa wakulima pamba mwisho wa mwezi

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema kiasi cha Sh. bilioni 43 kinachodaiwa na wakulima wa pamba kitalipwa mwisho wa mwezi huu.

Aidha, hadi sasa kiasi cha Sh. bilioni 437 kimelipwa kwa wakulima wa zao la pamba. Bashe alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Raphael Chegeni, ambaye alihoji serikali ina mkakati gani kutatua changamoto za wakulima wa mazao ili wapewe bei za kuwakomboa hususani zao la pamba.

Bashe alisema kuwa tatizo la pamba lililojitokeza mwaka huu ni kama ilivyojitokeza kwenye korosho mwaka jana na kwamba mwaka huu wameruhusu soko na minada ili wakulima wapate fedha kwa wakati. ”Tatizo la pamba lililojitokeza katika msimu uliopita halitajitokeza katika msimu ujao na serikali itakachofanya kwa wakulima wa pamba ili wasipate hasara ni kudhibiti gharama za viuatilifu, mbegu na mambo mengine lakini siku ya mwisho sokoni tutaruhusu bei ili wafanyabiashara wakutane na wakulima masokoni wanunue bidhaa hiyo na wahusika wapate pesa kwa wakati,”alisema.

Aidha, alisema bei ya pamba duniani ilianguka kutokana na mgogoro uliopo kati ya China na Marekani. ”Matokeo yake pamba ikakosa bei hivyo serikali ikaamua kutangaza bei kwa Sh. 1,200 ili wafanyabiashara wasipate hasara tukaamua kufanya mazungumzo na baadhi ya taasisi za fedha ili Hata hivyo, alisema kiasi cha Sh. bilioni 43 ambacho hakijalipwa serikali itahakikisha mwisho wa mwezi huu wakulima wa pamba wanalipwa.

Vile vile, aliwataka katika msimu unaoanza Novemba 15 wasambazaji wa mbegu wasambaze bila kuwadai wakulima chochote na kwamba watalipwa gharama zao msimu ujao.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alihoji maana ya dhana ya uchumi kukua ukilinganisha na maisha ya wananchi. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, alisema dhana ya uchumi kukua ukilinganisha na maisha ya wananchi inaweza kutafsiriwa katika dhana kuu mbili.

Alibainisha kuwa dhana hizo ni pamoja na kuangalia upatikanaji, ubora na gharama za huduma za jamii zinazotolewa na serikali.
 
Back
Top Bottom