Bil 40 zatumika kesi ya DOWANS!

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,300
2,000
MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika ametoboa siri kuhusu kesi ya Dowans akisema kuwa serikali imetumia dola za Kimarekani milioni 29, sawa na zaidi ya sh bilioni 40 (sh bil. 45.7) kwa ajili ya uendeshaji wake.

Kesi hiyo ya kupinga kulipa faini ya dola milioni 65 zinazodaiwa na kampuni hiyo, tayari imekatiwa rufaa na TANESCO na Desemba 5 mwaka huu itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Mnyika alitoboa siri hiyo juzi jijini Mwanza, wakati alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Movement for Change (M4C), ya chama hicho Kanda ya Ziwa, iliyofanyika Hoteli ya Gold Crest kisha kufanikiwa kupata jumla ya sh milioni 29.354. Ilihudhuriwa na wabunge, madiwani na viongozi mbalimbali wa CHADEMA.

Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Habari na Uenezi wa CHADEMA taifa, alibainisha kuwa Serikali ya Tanzania imeonekana kuchezea fedha za walipa kodi, kwani pamoja na kutumia fedha hizo zote katika kuendeshea kesi ya Dowans lakini bado haijamalizika.

“Dowans wanaidai serikali yetu dola za Kimarekani milioni 65. Na katika uendeshaji wa kesi hii Tanzania imetumia dola milioni 29, sawa na zaidi ya sh bilioni 40…na kesi bado inaendelea, hii ni moja ya udhaifu wa serikali,” alisema Mnyika huku akishangiliwa.

Mbali na hilo, Mnyika pia aliwageukia vigogo wanaodaiwa kuficha mamilioni ya fedha nchini Uswisi akisema kuwa baadhi yao ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema watuhumiwa hao wa ufisadi walihongwa mamilioni hayo ya fedha na baadhi ya wawekezaji wanaoingia Tanzania kufanya utafiti wa uchimbaji madini na mafuta, na kwamba wanafahamu idadi ya fedha hizo na wamiliki wake.

Katika hotuba yake, Mnyika aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa M4C, ambaye pia aliambatana na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA taifa, Godbless Lema, alisema kwamba vigogo hao wa CCM wamehongwa fedha nyingi na baadhi ya wawekezaji wanaomiliki makampuni hayo ya utafiti wa mafuta na madini.

“Ushahidi upo, mamilioni waliyoficha Uswisi wamehongwa na baadhi ya matajiri wenye makampuni yanayofanya utafiti wa kuchimba madini na mafuta hapa nchini kwetu Tanzania. Itafika siku tutawataja kwa majina,” alisema mbunge huyo wa Ubungo, ambaye hakufafanua zaidi ya hapo.

Aliitaka pia Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete kuacha kuziba pamba masikioni katika hilo, bali ifanye uchunguzi wake wa haraka kisha iwakamate na kuwafungulia kesi mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi huo wa kutisha.

Pamoja na hilo, Mnyika alisisitiza kuwa Rais Kikwete ni kiongozi dhaifu, kwani ameshindwa kuwawajibisha mawaziri na watendaji wake wanaoonekana kushindwa kutekeleza vema majukumu yao katika kuwatumikia Watanzania kama walivyoapa.

Alisema inashangaza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kutaka mawaziri wahojiwe na kujieleza kwenye vikao vya chama pale wanapoonekana kushindwa kazi, na kuhoji sababu za Rais Kikwete kushindwa kuwawajibisha viongozi na watendaji wake hao hadi kazi hiyo ifanywe na chama.

Kufuatia hali hiyo, Mnyika aliwasihi Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja na CHADEMA ili kuusaka ukombozi wa nchi hii ifikapo mwaka 2015 kwa kuiondoa madarakani CCM.

Katika uzinduzi huo wa M4C, Mnyika pamoja na mbunge wa Musoma mjini mkoani Mara, Vincent Nyerere walichangia kiasi cha sh milioni mbili kwa kila mmoja, huku Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Lema kila mmoja akichangia sh milioni moja.

Baadhi ya wajumbe wengine waliochangia na fedha zao kwenye mabano ni Meya wa Musoma, Alex Kisurura (sh milioni moja), Naibu Meya wa Musoma, James Bwire (sh 800,000), na mbunge wa Ilemela jijini Mwanza, Highness Kiwia ambaye alichangia sh milioni moja.
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
2,000
Dah!Tanzania inatisha kweli kila pesa utakayoisikia iwe imeibwa/imetumika vibaya ni ma'billioni ya shilingi.....ipo siku tutakula majani hapo ndipo tutaamka.
 

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,250
MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika ametoboa siri kuhusukesi ya Dowans akisema kuwa serikali imetumia dola za Kimarekani milioni 29,sawa na zaidi ya sh bilioni 40 (sh bil. 45.7) kwa ajili ya uendeshaji wake.

Kesi hiyo ya kupinga kulipa faini ya dola milioni 65, sawa na Bil 102 zinazodaiwana kampuni hiyo, tayari imekatiwa rufaa na TANESCO na Desemba 5 mwaka huuitaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Mnyika alitoboa siri hiyo juzi jijini Mwanza, wakati alipokuwaakizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya Movement for Change (M4C), ya chamahicho Kanda ya Ziwa, iliyofanyika Hoteli ya Gold Crest kisha kufanikiwa kupatajumla ya sh milioni 29.354. Ilihudhuriwa na wabunge, madiwani na viongozimbalimbali wa CHADEMA.

Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Habari na Ueneziwa CHADEMA taifa, alibainisha kuwa Serikali ya Tanzania imeonekana kuchezeafedha za walipa kodi, kwani pamoja na kutumia fedha hizo zote katika kuendesheakesi ya Dowans lakini bado haijamalizika.

"Dowans wanaidai serikali yetu dola za Kimarekani milioni 65 i.e Bil 102. Nakatika uendeshaji wa kesi hii Tanzania imetumia dola milioni 29, sawa na zaidiya sh bilioni 40…na kesi bado inaendelea, hii ni moja ya udhaifu wa serikali,"alisema Mnyika huku akishangiliwa.

Source: Tanzania Daima

Kwa akili ya kawaida kabisa nashawishika kusema kuwa hela za Dowans zimeamuliwa ziliwe kwa utaratibu mwingine ili kuwafidia wale walioumizwa kutokana na kashfa hii.

Wabunge tunaomba msiishie tu kuzungumza haya kwenye majukwaa ya siasa, tunataka kuona mchanganuo kamili wa namna mabilioni haya yalivyokuwa yanatumika kuendeshea hiyo kesi, kama kesi zote zingekuwa zinacosts zote hiz mwananchi wa kawaida angemudu kweli gharama za kesi?? Na kama kuendesha kesi ni ghali hivyo, je haki itatendeka/inatendeka kweli kwa wasiokuwa na billions za kuendeshea kesi zao????

Kama hadi sasa Bil 45 zishaenda na kesi ya kudai Bil 102 bado inaendelea, hivi mpaka kesi iishe si watatumia Bil 300 ili kudai hizo Bil 102??? Naona hapa kuna mchezo wa Kuuza Ng'ombe kwa kesi ya kuku!!Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni!! Hii kweli ni NGINJA NGINJA HADI 2015!!!!

Naomba kuuliza swali, Je hiyo mipesa ilikuwa inatandazwa kama carpet wakati wa kesi au ilikuwaje??? Babu zangu kule Mwandiga wanakosa hata Paracetamol na shuleni hata chaki hakuna huku mjini hela za kodi zinatapanywa hivi!!!! Naona serikali imeamua kukomoa wananchi wake kwa kuwa na kiherehere cha kushabikia ufisadi wa Dowans!!!!Je wanajamii hii ni sawa kweli???
 

Hiraay

Member
Jan 4, 2012
99
0
Actually serikali (TANESCO) ndiyo inadaiwa hizo bilioni 102 kwa kukatisha mkataba. Ndiyo maana ikakimblia mahakamani. SASA KAMA KWELI gharama zimefikia hapo na kesi (appeal) ndiyo kwanza inaanza basi zitatumika zaidi ya hizo tunazodaiwa. Ndiyo maana Ngeleja na mwanasheria mkuu walishatamka kwamba madai ya Dowans lazima yalipwe.
Kama ulivyosema zinaweza kutumika zaidi ya bil 300, na kesi tushindwe na kulipa hizo bil 102 pamoja na riba inayoendelea kupaa kadri siku zinavyokwenda.
Mwisho wa siku nani anayekomolewa?
 

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,254
1,195
Hii imeisha andikwa sana humu JF, saga zima, na Legal Advisers wa TANESCO (Rex Attorneys akina Maajar, Nguluma , Sinare na wenzake). Hawa Rex Attorneys wanatuingiza chaka sana, inabidi waangaliwa kwa jicho la tatu pia!
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,529
2,000
wakuu tungemsikiliza DR.Idris rashid haya yote yasingetokea!mitambo ingekua yetu kwa 40bn tuu!siasa ndio inatumaliza
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,480
2,000
Hii imeisha andikwa sana humu JF, saga zima, na Legal Advisers wa TANESCO (Rex Attorneys akina Maajar, Nguluma , Sinare na wenzake). Hawa Rex Attorneys wanatuingiza chaka sana, inabidi waangaliwa kwa jicho la tatu pia!
hapo kwenye red na underline naona mama kaamua kuanzisha hata wakfu (foundation) kutatua baadhi ya matatizo ya masikini wa Tanzania maana inaelekea fedha zinawazidia, wanatoa 'murahaba'!
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,188
2,000
Hii ni kesi ya kuku na jamaa kaamua kuuza ng'ombe
Kesi itaendelea kula pesa za walipa kodi na mwisho wa siku Tanesco watashindwa na watailipa Dowans madai yako na riba juu na gharama za mawakili wao
Na bado tutaendelea kuchekeana tuu as if hakuna kilichotokea
 

bayonamperembi

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
351
250
Dah! Kweli hii nchi tajiri sana. Yaani kila sehemu watu wanatafuna hela!! Hela zote hizi zinazopotea hovyo hovyo kiuchumi tungekuwa mbali sana . Hapa Africa tungekuwa ndo nchi tajiri kuliko zote.
 

Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
May 24, 2008
3,736
2,000
Hii ni kesi ya kuku na jamaa kaamua kuuza ng'ombe
Kesi itaendelea kula pesa za walipa kodi na mwisho wa siku Tanesco watashindwa na watailipa Dowans madai yako na riba juu na gharama za mawakili wao
Na bado tutaendelea kuchekeana tuu as if hakuna kilichotokea

mkuu mi ndio maana nakaa kimya au naenda kuleeee hapa naweza kupata bun muda wowote kwa jinsi jazba ilinikamata
 

Kakende

JF-Expert Member
Aug 18, 2012
2,741
2,000
Nimechoshwa na tuhuma za ufisadi kila siku, naanza kusahau tuhuma zingine. Tuwaache CCM wale wakichoka watwambie
 

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,300
2,000
E anayofanya zitto ni kinyume na matakwa ya chama?
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,360
2,000
Mambo yanaenda yakiongezeka!

CDM walisema serikali ikikurupuka na kulipa wataandamana!

Serikali inatafuta haki imekuwa shida tena! Hizo ndizo gharama za kutafuta haki! Inawezekana serikali ikashindwa huku imetumia pesa zote hizo na kuamuliwa kuilipa Dowans tuzo yao pamoja na gharama za kesi huku na yenyewe ikiwa imegharamia! Huenda tukaishia kuona serikali inaingia gharama mara tatu. Kama ingelipa mapema ingekuwa imelipa tuzo tu bila gharama hizi za ziada!
 

Manyi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
3,254
1,195
[h=5]John Mnyika
[/h][h=5]Ufafanuzi kesi ya Dowans

Ufafanuzi kuhusu gharama za uendeshaji kesi ya Dowans. Juzi kwenye harambee ya M4C nilisema kwamba kabla ya kwenda Mwanza nilikuwa nafanya mahesabu ya kiwango cha gharama ambazo TANESCO imetumia na ina mwelekeo wa kutumia kwenye kesi ya Dowans pekee nikasema ni dola zaidi ya milioni 29 (ambayo ni bilioni takribani zaidi ya 40).

Nitoe ufafanuzi kwamba katika mahesabu yangu nimejumuisha USD 2.9 ml/- (takribani bilioni 4) za gharama za mawakili katika mazingira yenye utata. Na gharama za kibenki iliyowekwa Uingereza katika mazingira ya hatari ya kupoteza (risk) ya dola zaidi ya milioni 28 (bilioni zaidi ya 40) na gharama nyinginezo ambazo nitazikokotoa baadaye. Ni vizuri mkarejea hotuba niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai, 2012 ambapo nilitaja namna kesi za Dowans, I... PTL, zinavyotumiwa kifisafi kama vitega uchumi kwa gharama zenye kubebesha mzigo kwa Tanesco na hatimaye wananchi kupitia bei ya juu ya umeme.

John Mnyika,
Waziri Kivuli, Wizara ya Nishati na Madini.


[/h]
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225


• SITTA ALIFUNGA MJADALA WAKE, LEO ANAIPINGA

na Mwandishi wetu


HATUA ya serikali kushindwa kufanya uamuzi mgumu na hivyo kuendekeza siasa katika sakata zima la malipo ya Kampuni ya ufuaji umeme ya DOWANS Tanzania Limited, imesababisha wananchi kuendelea kubebeshwa mzigo wa hasara, Tanzania Daima limebaini.


Hatua hiyo inatokana na serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kushindwa kulipa fidia ya takribani sh bilioni 104 za Kampuni ya DOWANS kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, 2010.

Mwenyekiti Gerald Aksen na jopo la wasuluhishi, Swithin Munyantwali, Jonathan Parker wa mahakama hiyo, waliiamuru TANESCO iilipe DOWANS kiasi hicho cha fidia kutokana na kukiuka mkataba.


“Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya sh bilioni 36 (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,” ilieleza sehemu ya uamuzi huo.


Pia jopo hilo liliamuru sh bilioni 60 (dola za Marekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.


Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala sh bilioni moja (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika.


TANESCO wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) sh bilioni 3 (dola 1,708, 521 za Marekani) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.


Hata hivyo, kitendo cha TANESCO kutolipa deni hilo na hivyo kukimbilia mahakamani kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo, kinazidi kuigharimu serikali kwani kodi za wananchi zinazidi kuteketea kulipia gharama za kesi.


Kulingana na taarifa zilizopo mpaka sasa ni kwamba kesi hiyo kati ya TANESCO na DOWANS imeigharimu serikali kiasi cha dola za Marekani milioni 29 (zaidi ya sh bilioni 40) ambazo zingetumia kuhudumia miradi mingine ya jamii.


Kiasi hicho kikubwa kisingetumika, laiti serikali ingefanya uamuzi mgumu mapema ikailipa DOWANS kutokana na uzembe uliofanywa na wataalamu wake kwenye mkataba husika.


Badala yake TANESCO wameendelea kukata rufaa licha ya kubwagwa mara mbili mahakamani na hivyo kuzidi kuongeza gharama za fidia husika kwa DOWANS na zile za mawakili
wanaoliwakilisha shirika hilo.


Fedha hizo ni nyingi kwa vile kesi itakapokuwa imemalizika TANESCO watapaswa kulipa fidia zaidi kwa DOWANS kuliko kiasi kilichoamriwa na mahakama kutokana na thamani ya dola kuzidi kupanda.


Kwa asilimia kubwa waliotufikisha hapa ni wanasiasa wetu ambao ama kwa maslahi yao binafsi au kulipiza visasi kwa wabaya wao, wananchi wamejikuta wakibebeshwa mzigo huu na hivyo kodi zao kuteketea bure.


DOWANS ndiyo ilirithi mkataba wa kampuni tata ya Richmond LLC ambao ulizua gumzo bungeni na kufikia hatua ya Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowassa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi pamoja na naibu wake Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu mwaka 2008.


Hata hivyo, Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza zabuni hiyo ya Richmond, chini ya uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe, ilishindwa kusimamia hadi mwisho kuhakikisha maazimio yao yanatekelezeka.


Dk. Mwakyembe pamoja na Spika mstaafu, Samuel Sitta, wamekuwa mstari wa mbele kupinga DOWANS kulipwa fidia hiyo, wakidai waliohusika kuingia mkataba huo ndiyo wabebe dhamana.


Lakini Sitta anasahau kuwa yeye ndiye alizima mjadala wa Richmond usiendelee kujadiliwa bungeni, huku akijua kabisa kuwa maazimio ya kamati teule yalikuwa hayajatekelezwa na serikali.


Hapa ndipo msigano wa makundi mawili katika sakata hilo unapojitokeza na kusababisha hali iliyopo sasa iendelee kuwaumiza wananchi na kodi zao kutumika kulipia uzembe wa watu wengine badala ya kugharamia huduma za maendeleo.


Kundi la kwanza ni la watendaji wa kisheria wa serikali chini ya Mwanasheria Mkuu, walioingia mkataba husika na baadaye kuuvunja huku wakielewa fika kuwa ni kinyume na matakwa na hivyo kusababisha hasara.


Lakini kundi la pili ni lile la wanasiasa kama Sitta, Mwakyembe na wengine wanaoendeleza mivutano katika sakata zima, wakipinga DOWANS isilipwe bila kujali kuwa uchelewaji wa TANESCO kulipa fidia hiyo ni kuongeza gharama zaidi.


Hawa ni pamoja na wale wanaoendelea kuishauri Tenesco ikate rufaa kupinga hukumu husika, kwani gharama za kuwalipa mawakili watetezi zinazidi kuongezeka na kuongeza hasara maradufu.


Pengine hasara hii ingeweza kuepukwa kama serikali ingekuwa makini na sikivu kwa kuchukua mawazo ya baadhi ya wananchi wenye mapenzi mema na taifa.


Mathalani mpango wa kuuza mitambo hiyo ya DOWANS uliwahi kutolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), lakini serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini baada ya malumbano kadhaa ilitangaza rasmi kuwa haina mpango wa kununua mitambo hiyo.


Kufuatia uamuzi huo, DOWANS iliamua kutangaza kuiuza mitambo yao nje ya nchi jambo lililosababisha serikali kuiwekea pingamizi katika Mahakama ya Biashara ikitaka wamalize kwanza masuala ya mikataba.


Siku chache baadaye, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), iliikamata mitambo hiyo kwa madai kuwa ilikuwa ikidaiwa ushuru.


Hatua ya kuiwekea pingamizi ili mitambo hiyo isiuzwe ilipingwa vikali na DOWANS na kuamua kukimbilia katika Mahakama ya ICC iliyopo nchini Ufaransa ili kuhakikisha mitambo hiyo inaweza kuuzwa.


Mara ya kwanza dhamira hiyo ya serikali kupitia TANESCO kutaka kununua mitambo ya DOWANS, iliibua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania, huku wakionyesha shaka kuhusu uamuzi huo.


Mjadala huo ulitokana na malumbano ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na William Shellukindo na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyokuwa chini ya Zitto.

Kamati ya Shellukindo ikisisitiza kutokuwepo umuhimu kwa TANESCO kununua mitambo hiyo.


Mvutano wa kamati hizo ulikuwa mkubwa, baada ya Zitto kusisitiza kuwa atamuomba Spika wa Bunge, wakati huo Sitta, kuitisha mkutano wa kamati hizo mbili ili kujadili upya suala hilo na kwamba utetezi wake wa kununua mitambo hiyo unatokana na kuweka mbele maslahi ya taifa.


Kutokana na mjadala huo uliochukua mwelekeo wa kupinga ununuzi wa mitambo hiyo, hatimaye TANESCO ilitangaza kuondoa nia yake hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa mjadala wake umechukua sura ya kisiasa kuliko kuzingatia utaalamu.


DOWANS ilirithishwa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006 baada ya kampuni iliyoshinda zabuni hiyo, Richmond Development Company LLC kushindwa kuleta mitambo hiyo na baadaye kukumbwa na kashfa ya ushindi wa zabuni hiyo.


Jenereta hizo za kufufua umeme ambazo zinatumia gesi asilia zilitangazwa kuuzwa nje ya nchi kwa zaidi ya sh bilioni 101 ingawa biashara hiyo serikali iliiwekea pingamizi mahakamani, lakini sasa imeuzwa kwa kampuni ya Marekani ya Symbion Power ambayo inauza umeme huo TANESCO.


Kama si siasa zetu mbovu, sakata hili la TANESCO na DOWANS lilipaswa kuwa limemalizika na kuokoa fedha zinazoteketezwa sasa zikaelekezwa kwenye kupatia wananchi huduma za maji safi na salama, barabara, makazi bora, elimu, afya bora na kulipa mishahara inayokidhi ili kuondoa migomo.


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom