BIL. 11/- KUJENGA BARABARA NGORONGORO

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1552048158023.png

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetenga Sh bilioni 11 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Loduare hadi Golini kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 88 katika eneo la kushukia bonde la hifadhi hiyo.

Lengo la kujenga barabara hiyo katika kipindi cha mwaka huu ni kuondoa usumbufu wanaopata madereva wanaoendesha magari ya utalii, sambamba na watalii wanaoingia ndani ya hifadhi hiyo kujionea vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Fredy Manongi amewaeleza waandishi wa habari sema ujenzi wa barabara hiyo utawezesha kuondoa kero wanazopata watalii na madereva kwani barabara hiyo wakati wa mvua ina changamoto zake na hata nyakati za jua.

Barabara itakayojengwa ni kutoka Loduare hadi Golini kwa kilometa 88 na wanashukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kwa kukubali barabara hiyo kujengwa pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ndani ya hifadhi.

“Naomba madereva wanaoshuka kwenda kreta kuwa makini wakati wanapotumia barabara hii na hivi sasa tunasubiri mkandarasi atakayeshinda zabuni aanze kujenga barabara hii kwani fedha tayari tunazo,” amesema. Shabani Felician ambaye ni fundi sanifu wa NCAA, amesema mamlaka hiyo kila mwaka hutumia zaidi ya Sh bilioni tatu hadi bilioni tano kwa ajili ya kutengeneza barabara zilizopo ndani ya hifadhi hiyo, hivyo endapo watajenga barabara hizo kwa kiwango cha lami wataokoa mabilioni ya fedha. Alisema baadhi ya barabara zitajengwa kwa kiwango cha zege huku nyingine zitajengwa kwa kiwango cha lami ili kuokoa mazingira pamoja na uhifadhi katika hifadhi hiyo.
 
View attachment 1040871

Kiukweli huu utakuwa uamuzi sahihi sana.,ambao utachangia ongezeko la wageni kwa kiasi kikubwa kwani njia ilikuwa Kati ya changamoto mbaya iloligarimu taifa kwa muda mrefu.

Tatizo litakuwa Ni muda.iwapo busara ikatumika,wakapewa wakandarasi maalumu na kadhaa ili kumaliza kazi hiyo kwa wakati, ama kwa muda mfupi iwezekavyo basi, maamuzihayo yataitwa ya kizalendo.lkn Kama mchakato na ujenzi utakuwa Kama wa ile ya elerai, basi Mungu na asimame
 
Ni Jambo jema, lkn litafanyika kwa wakati?!Kama watatumia njia waliyojengea ile ya elerai,km 7 kwa miaka ,basi itakuwa janga.lkn wakitumia wakandasi making na wengi kutokana na umuhimu wa utalii basi huu utakuwa uzalendo wa Hali ya juu
 
Ni wazo zuri sana. Wengi wa wasafiri kutoka Mwanza, Musoma, Shinyanga kwenda Arusha tutakuwa tunatumia barabara hii ambayo itapunguza sana masaa mengi kufika Karatu, Mto wa Mbu, Makuyuni na hatimaye Arusha.
 
Kumbuka hapa hawajasema kipande cha serengeti ambacho bado kitakuwa ni changarawe kama kawa.
Hata hiyo lami ikiisha mpaka golin pale haitoshi .. kipande cha serenget bado kitabakia.
Hapa watu wa mabasi yanayotoka musoma ndio watapata unafuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barabara hii kwa kiwango cha lami ni zaidi ya 120bn/=. Mimi binafsi nafahamu sana kipande hiki. Kwa kweli kipande hiki kwa siku wakati wa high season yanapita sii chini magari 2000. Usiombe vumbi inayotifuliwa na magari ya kitalii. Omba gari lako liwe na kiyoyozi bila hivyo ukifika Oduare gate wewe mwenyewe utasimulia. Kwa kweli kipande hiki kinatakiwa kiwekwe lami mpaka Nabi gate upande wa Hifadhi ya Serengeti. Hapa pakiwekwa lami hakuna tena haja ya kuweka lami kuzungukia loliondo.
 
Na wale nyumbu watengenezewe daraja la kukatisha
Watanishangaa lakini acha niwaambie tu
Haki za wanyama zizingatiwe maana Mamba wamezidi sana kuwauwa Nyumbu

Kwa hilo la barabara ni sawa ila iwe ya kuzunguka zunguka kuona wanyama wote au vipi

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom