Biharamulo: Mil 14 zakulipa madeni ya watumishi zinatolewa kibaguzi sana

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,137
3,323
Kwakweli kinachoendelea kwenye hii halmashauri yetu sio sawa kabisa. Tulipata taarifa kuwa zimetumwa milioni 14 kwa ajili ya kuwalipa watumishi(walimu) madeni yao. Japo ni kidogo sana lakini ingewekwa wazi hasa majina ya waliofanikiwa kulipwa.

Kinachofanyika wanalipwa wale wenye mahusiano na watu wa halmashauri. Hili jambo sio jema kabisa, wanaweza kulipwa hata wasiostahili kabisa maana imefanywa kwa usiri sana.
 
Fuatilia majina ya wanaostahili kulipwa toka kwa Katibu Tawala mkoani kwako yametumwa huko. Kama jina lako halimo basi liko kwenye orodha ya wale wenye madeni yaliyokataliwa.
 
Ok, ngoja nifanye hivyo mkuu. Lakini kwa nini hiyo orodha inafichwa pale halmashauri?
 
Walimu bana milioni kumi 14 mnazigombea hadi JF kweli njaa itawaua na hivi ninyi ndio wasimamizi wa uchaguzi ipateni fresh tu.
 
Walimu bana milioni kumi 14 mnazigombea hadi JF kweli njaa itawaua na hivi ninyi ndio wasimamizi wa uchaguzi ipateni fresh tu.
Mkuu usistudhihaki hatukupenda tuwe hivyo. Ni mfumo tu kama wewe umekufavour mshukuru Mungu. Ila na wewe idara uliyopo viongozi wakiamua kuipuuza lazima na wewe uwe na njaa kama sisi.
 
Back
Top Bottom