Bigup kwa watu wote walioacha ajira za halmashauri na kufanya mishe zao, Mungu atawapigania

Sawa Mjuaji tajiri big boss mwenye akili
umesikika Kwangu wewe ni bonge la Mshamba wa Maisha na Mselamavi...
Kachezee uko, we mwehu nini kabishane na vilanga wenzako wa jukwaa la celebrities mshamba wewe. Kwenye Dunia ya sasa mtu anaishije na mshahara wa laki nne huna posho yoyote Ile afu unakuja kubwata apa au huwajui walimu wa hii bongo walivyopauka wananuka mpaka mabolingo
 
Unaweza kuta jamaa ni mkuu wa idara halmashauri fulani hivi
 
Brother unavyo itamka milioni kumi na tano unaitamka kama pesa ndogo sana shida ipo kwenye kuikusanya mpaka ifike hiyo milioni kumi na tano.
Pili kuna dogo mmoja nimesoma naye shule moja ya msingi maalufu kama Rickius Babylon, baake alikua mwalimu wa shule ya msingi.
Tulipotezana siku nyingi kama miaka kumi hivi, mwaka 2017 mwezi wa kumi na mbili akanipigia simu akaniambia uko wapi? Nikamweleza nipo Mwanza akanambia yeye yupo Katoro na kasema kwa kuwa kuna kipindi niliwahi kumsaidia basi nijitahidi nimtafute siku nikienda Katoro.
Baada ya kufika pale kanionyesha mali mbali ikiwa ni pamoja na flme za maduka akidai kwamba ni mali yake na alijitahidi kwa kila namna kufanya chochote ili anifanye nishawishike kua yeye ana fedha nyingi sana mpaka wakati mwingine kuazima magali ya watu akidanganya kua ni mali yake.
Katika pita pita zangu hapa na pale huko katoro nikaona kuna fursa ya kufyatua tofali za udongo za kuchoma na kiziuza. Hivyo nikatafuta eneo nikaanza husstling nikaajili watu wakafyatua tanuru ya tofali 58000 ambapo nilitumia gharama kama ya milioni moja na nusu nikitegemea kuuza kwa shilingi 150 kila tofali ambapo nilitegemea moja kwa moja ningepata fedha isiyo pungua milioni sita hata kama ningeuza tofali elfu hamsini tu kwa maana soko ni la uhakika.
Kizaa zaa kilikuja baada ya kua nimeivisha tofali nimetoka zangu mwanza nisha muandaa mteja kua naenda kumuuzia tofali, baada ya kufika mahali nilipo kua nimechomea tofali sikukuta hata tofali moja na yeye ndie alikua ananiangalizia.
Nilipo mpigia simu akaniambia kwamba amezichukua ameenda kumalizia nyumba yake atanipa fedha, nikamuuliza nyumba gani akanionyesha nyumba nikafatilia kumbe hata ile nyumba haikua yake ilikua ya mtu mwingine nikampa mda wa mwezi mmoja awe amelipa pesa yangu, mwezi ukaisha nikamuongezea mwezi mwingine uswahili mwingi.
Nikaenda kwenye ofisi ya mtandaji wa kijiji nikamkamata tukamuweka ndani pale pia nikaona kuna uswahili mwingi ujanja ujanja tukaenda polisi kisha mahakamani.
In short sikulipwa hata shilingi moja pamoja na yule jamaa mara ya kwanza kunishawishi kua nikiendelea na ualimu wangu nitakufa masikini.
Mwisho wa siku niligundua mimi pamoja na kupata fedha kidogo kidogo hii nilikua na maisha mazuri kuliko yeye na ndio maana alilenga kuniweka karibu ili anitapeli.
Tumeona wadada wengi hasa walimu na manesi wametpeliwa sana na watu wa mitaani wanaojifanya wafanya biashara na kuwaingiza kwenye mikopo mikubwa ambayo wanailipa mpaka kwa miaka nane na mwisho wa siku wanaambulia kuachwa na watoto wenye wazazi wasio eleweka kwa sababu ya tamaa.
Brother Mungu anagawa riziki kwa mafungu. Kuna wanao ingia mtaani kweli mambo yao yanawanyookea lakini pia kule mtaani kuna wanao pitia hustling ya hatari kiasi kwamba hata akimuona huyo mwalimu anaona kama ana maisha mazuri
Mimi ni mwalimu kwa kweli ninaifurahia kazi yangu na pia kazi yangu hainizuii kufanya hustling za mtaani
Kwa busara usipende kuidhalau kazi ya mtu kwa sababu huijui kesho yako. Kama Mwenyezi Mungu kakujalia kupata nafasi basi shukuru kwa hilo na sio kuwaona wengine wapumbavu
 
Inaukweli lakini mitaji ndio shida
 
Mm nimesema hazina masilahi kwahiyo waambien serikali yenu iwape mishahara mikubwa acha kutia Tia huruma apa, wewe ulitapeliwa kwasababu ni mwalimu, walimu wengi bado ni washamba saana nabora muendelee kupigwa mpaka akili ziwakae sawa
 
Umeshasema ukiingia kitaa ukiwa na milioni kumi na tano. Vipi kama huna?
 
Ww mpwayungu hv m15 ndo zakufanya uwe tajiri mtaani

Mxiiuuuuuuu
 
Huyu Mwalimu hajui maana ya maisha!!!hujui kuwa Duniani hakuna kitu hutokea bahati mbaya??each and everything was already planned,sisi tuko hapa kukamilisha ratiba tuu!Wewe Leo umesomea ualimu then hujaajiriwa,umejiajiri siyo Kwa bahati mbaya mkuu,ilipangwa.

Mimi nimezaliwa mwalimu Wala siyo mfanyabiashara kama wewe,Kila mtu na alichotunukiwa Mpwayungu Village ndiyo maana kwenye jamii zetu tuna Manesi,wafanyabiashara,wajasiliamali,bodaboda,wanajeshi,madaktari n.k lengo ni kukamilisha jamii,haiji kutokea jamii wote tukawa siyo wafanyakazi wa serikali haiwezekani
 
Jidanganye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…