Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 14,455
- 31,063
Nimeanzisha huu uzi baada ya kuona comment ya huyu bwana johnthebaptist kwenye uzi mmoja. Naamini pasi na shaka huu ndo uongo mkubwa ambao watanzania wengi wameaminishwa. Hii kasumba ipo kila kona mitaani na kwenye uwanja wa siasa.
Wabongo wameaminishwa na wao wamekubali kwamba nchi yetu ni tajiri sana hivyo wao hawapaswi kufanya chochote wala kulipa kodi bali kuishi bure tu.
TZ tuna rasilimali kama nchi zingine hivyo tusijione special sana. Bongo inaizidi nini nchi kama South Africa, kama madini kule ndo kwao, mbuga za kutosha, natural gas, bahari nk na bado wanalipa kodi.
US ni amongst top producers of gold, oil, copper, natural gas na madini mengine worldwide. US kuna pacific na Atlantic ocean. Kuna national parks kibao grand canyon, Yosemite, Glaciers nk na bado US unaweza lipa kodi hata kwa kujamba tu. Same applies to China na Europe.
TZ haina mafuta wala sio hata top 5 of gold producers in Africa let alone duniani. Hatuna uspesho wowote hizi rasilimali kila nchi zipo. Rai yangu ni serikali iweke mazingira rafiki ya uwekezaji na itanue wigo wa kodi badala ya kukamua vyanzi vile vile kila siku.