bigger is better; simu kubwa na rahisi za android

bigger is better; simu kubwa na rahisi za android

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,073
Reaction score
43,522
simu nyingi za juu ambazo zina specification za ukweli zinauzwa bei kubwa approximation ni millioni moja kwenda juu. mfano wa simu hizo ni kama nokia lumia 920, samsung galaxy s3, htc droid dna na iphone 5. lakini ukiangalia kwa makini unakuta vitu vingi vinavyofanya hizo simu ziuzwe bei kubwa havina maana kwa mazingira ya kiafrica.





mfano network ya 4g(lte), kustream hd(network yetu ipo slow), vitu kama gps hatutumii na mambo ya location, wengi wetu hatujali toleo la operating system kama ni android hata ikiwa 2.3 inatosha.





kutokana na mambo hayo nikaona niandae hii makala ya kuonyesha aina za simu ambazo kimuonekano ni kama simu za bei ya juu lakini zimenyimwa vitu flani ambavyo si muhimu kwa muafrica kuvikosa na hivyo kufanya bei ishuke. kwa kubase kwa ukubwa wa screen (zaidi ya 4.2 inch) na udogo wa bei (china ya laki 5)





kambi ya htc


hapa kuna simu moja tu





htc inspire 4g


htc-inspire-4g.jpg



kwanini ununue?


kwa sababu ina screen ukubwa 4.3 yenye resolution ya 480x800, ina gorrila touch screen inayofanya kioo kiwe kigumu kuvunjika. ukubwa wa screen umeizidi iphone 5 na imepitwa kidogo tu na samsung galaxy s3 pia inauwezo wa kuchukua semi hd video 720p na camera ya 8mp.





general perfomance


inakubali android hadi 2.3 gingerbread ikiwa na processor ya 1ghz na ram 786 na internal memory ya 4gb ikisuport memory card ya 32 gb (memory card ya 8gb inakuja na simu). kwa specification hizo zinaifanya hii simu kuwa fair, itarun smooth. pia ina speed hadi 14.4 mbps kwenye internet kwa standard ya 7.2 mbps kwa tanzania simu itakua very fast.





kambi ya samsung


tuwe wa kweli ni vigumu kupata samsung kwa bei rahisi nyingi zinauzwa bei kubwa sana hapa nimepata simu moja tu ambayo haina 3g.


samsung galaxy s wifi


samsung-galaxy-s-wifi5.jpg



nisiizungumzie sana maana haina 3g wala haitasuport function zozote za simu lakini hii inaweza kua mbadala wa ipod maana ina kioo kikubwa cha inch 5, na storage ya 16gb au 8gb so ni nzuri kuangalizia movies, videos , kuhifadhi picha, kuskilizia miziki na kuchezea games.





kambi ya kaka lenovo


lenovo a800


lenovo-a800.jpg



huyu jamaa lenovo anakuja juu sana mwaka jana ilikua ndo kampuni iliouza sana computer na kwenye simu akampita nokia na samsung kwenye soko la china. hapa anakuja na simu yake a800, ikiwa na screen ya 480x800 kwenye kioo cha 4.5 inch na ram ya 512mb pamoja na processor 1.2 ghz dual core na operating system ya ice cream sandwitch inaifanya hii simu kuonekana bora zaidi.


bei pia sio mbaya sana kwa simu hii maana ni chini ya laki 4





kambi ya micromax


micromax a110


micromax-a110.jpg



wengi labda mtakua wageni wa hii kampuni lakini ni kampuni ya kihindi ambayo inatengeneza simu cheap sana za android na hii a110 ina screen 5inch ukubwa kama galaxy note ikiwa na resolution ya 480x800 na ram ya 512 mb. processor ni 1ghz dualcore na internal memory ni 4gb. hii nayo bei ni chini ya laki 4.





kambi ya ACER


acer liquid gallant e350


acer-liquid-gallant-e350.jpg



hii ndo simu ya MWISHO ikiwa na screen ya 4.3 ina internal 4gb ram 1gb na proccessor 1ghz. resolution kidogo kubwa ina 540x960
 
nemevutiwa na htc, japo haina 3G. Ningepata bei yake halisi ingekua vema zaidi.!
 
kambi ya kaka lenovo


lenovo a800


lenovo-a800.jpg



huyu jamaa lenovo anakuja juu sana mwaka jana ilikua ndo kampuni iliouza sana computer na kwenye simu akampita nokia na samsung kwenye soko la china. hapa anakuja na simu yake a800, ikiwa na screen ya 480x800 kwenye kioo cha 4.5 inch na ram ya 512mb pamoja na processor 1.2 ghz dual core na operating system ya ice cream sandwitch inaifanya hii simu kuonekana bora zaidi.


bei pia sio mbaya sana kwa simu hii maana ni chini ya laki 4
Mkuu chief unaweza kuniambia bei halisi ya hii simu na inapopatikana
 
Hiyo samsung sio simu ni media player. Hiyo HTC screen ni kubwa lakini resolution ni ndogo pixel density nayo inakuwa ndogo hauwezi kufananisha na iphone 5, wala s3. Unacholipia kwa simu za high end sana sana ni quality ya screen, uwezo was processor, camera + internal space. Hakuna smartphone utakayokosa 3G auto gps hata cheapest Huawei zinazo.
 
Mkuu chief unaweza kuniambia bei halisi ya hii simu na inapopatikana
mkuu mi nikiandika makala sipitii madukani na hata eneo nilipo haliniruhusu kufanya hivo. Itakua ngumu kukwambia inapatikana wapi lakini kwenye maduka makubwa ya simu hope utaipata na ukikosa unaweza ukatoa order kwa wale wanaosafiri kufungasha simu.

Bei sehemu nyingi kwa kutumia source za online ni 219usd hadi 230usd ambayo ni kama 350,000 so kibongo itapanda kidogo zaidi ya hapo
 
Hakuna smartphone utakayokosa 3G auto gps hata cheapest Huawei zinazo.

ur wrong broda... Kuna bunch of Blackbery Smartphones zenye Edge.... Model zote za blackbery Chini ya 9000 zna 2G
 
Wakuu hebu nisaidieni kuhusu Samsung Galaxy Y GT-S6102 maana nakusudia kununua hivi karibuni.Ushauri unaombwa yoyote anaejua vema anisaidie.
 
Hapana bhana cmu ya bei kubwa kama hiyo galaxy s3,iphone five n habar nyingine,natumia smsung galaxy s 4G yaan speed ya net tena ukiweka airtel haina mfano then naconnect na lap yap via wireless so inaact as moderm sema CMU ZA BEI ASILIMIA KUBWA ZNATATIZO LA.KUTOKAA NA CHARGE MAANA ZNA OPERATING NYING ZNAZORUN MUDA WOTE
 
Hiyo samsung sio simu ni media player. Hiyo HTC screen ni kubwa lakini resolution ni ndogo pixel density nayo inakuwa ndogo hauwezi kufananisha na iphone 5, wala s3. Unacholipia kwa simu za high end sana sana ni quality ya screen, uwezo was processor, camera + internal space. Hakuna smartphone utakayokosa 3G auto gps hata cheapest Huawei zinazo.
That is the facts
 
Wakuu hebu nisaidieni simu Samsung Galaxy Y GT-S6102 maana nakusudia kununua hivi karibuni pia simu hii ni Duos.
 
Ni simu gani inayofanana na iPhone 4s kwa features zake lakini ni cheap kuliko hiyo iPhone 4s?
 
Ericsson R250s PRO, kwa matumizi yangu inanifaa sana hasa betri kudumu.
 
Back
Top Bottom