Big up sana kwa Aliexpress (ALIBABA), wanafanya vyema sana katika kuhudumia wateja

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Habari!
Waswahili wana msemo kuwa asiyesifia kwao ni mtumwa. Ila mimi nina mtizamo wa tofauti ya kwamba utakuwa mtumwa wa fikra mara mbili kama unaujua ukweli halafu unasema unafiki ama uongo ambao unakinzana na ukweli.

Sasa leo hapa, nimeona niweke wazi jinsi kampuni ya alibaba/aliexpress wanavyofanya vema katika kumhudumia mteja wao.

Kwa wale wazio na uelewa wa alibaba/ aliexpress ni jambo gani, msijali nitawamegea ufahamu kidunchu.

Alibaba/ aliexpress ni kampuni moja ya mtandao inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa za aina mbali mbali kuanzia kilimo hadi kikolokolo chochote unachokijua wewe hapa duniani wao wanacho.

Branch hizi mbili zinafanya kazi chini ya mwamvuli m'moja. Yaani Alibaba inadili na wauzaji wa jumla na Aliexpress ikidili na uuzaji wa reja reja.

Kilichonifanya kuandika hili bango leo ni ukweli kwamba wamejitahidi sana kuicustomize application yao kiasi kwamba kwa sasa inakunyumbulishia bei kwa shilingi ya kitanzania, na nimesikia wapo mazungumzoni na kampuni za matandao ya sim ili tuweze lipia moja kwa moja bila kuhangaika na mabenki yetu uchwara haya yasiyo na faida zaidi ya kuibia senti zetu kila tunapoziweka.

Katika kulitazama hilo, nimewazia kuwa hapa tanzania hawa wanaoshiriki katika tasnia ya manunuzi ya mtandaoni wengi wanaonyesha kutokujiongeza, na hii inakwamisha sana wateja kupata huduma kwa urahisi.

Ila hawa jamaa wanakazana kila uchao ili kuahikikisha raia wa mataifa ya mbali kama Tanzania anapata huduma nzuri as if wao wapo nae katika ardhi moja .

Hii ni changamoto kubwa sana kwa hawa wanatasnia ya mauzo ya mtandaoni wa Tanzania ambao wameridhika na hawajiongezi.

Madereva wa tax walikuwa hivyo hivyo hadi zilipokuja bajaji, boda boda na sasa Uber.

Kwetu sisi wateja tunasema vita vya panzi ni faida ya kunguru. Sisi tunachotazama ni huduma bora na sio ubabaishaji na kero
zenu.

Asante
 
nilitaka nipost uzi km huu ila hawa jamaa ni big up nawapenda mno
 
Ni wiki moja na siku kadhaa sasa sijapokea mzigo wangu. Ni mzigo mdogo sana. Najaribu kuona efficiency yao compared to ebay.
Mpaka sasa ntabaki kusema ebay ni wa uhakika zaidi.
 
HABARI,
"toplemon,
Hongera sana Ila huwa unaagiza pc 50 Kwa shipping ya elfu 20 hizo ni pc za sindano au za bidhaa gani,
Ufafanuzi tafadhali.

small packages zote unazozijua

LUMUMBA
Ni wiki moja na siku kadhaa sasa sijapokea mzigo wangu. Ni mzigo mdogo sana. Najaribu kuona efficiency yao compared to ebay.
Mpaka sasa ntabaki kusema ebay ni wa uhakika zaidi.
ebay wanachukua siku ngp kusafirisha???
 
Asante boss

HABARI,
"Mr Suprize,
Karibu Tena,Ila kuwa makini Ndani Ya Alibaba kuna matapeli wengi sana sio wote watakuwa Halali wako wengi,Angalia Hasa kama anayekutumia anakupa Bank Account sio mambo ya western union ndani ya western union wapo halali ila matapeli ni wengi pia Kuwa Makini.

LUMUMBA
 
Ni wiki moja na siku kadhaa sasa sijapokea mzigo wangu. Ni mzigo mdogo sana. Najaribu kuona efficiency yao compared to ebay.
Mpaka sasa ntabaki kusema ebay ni wa uhakika zaidi.
Kaka kama uishawahi wafanya mihamala kutumia ebay naomba msaada km malipo
 
Back
Top Bottom