Big Results Now: Karibuni Mlimani City - July 03, 2013

Joined
May 18, 2013
Posts
11
Reaction score
15
MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
Mada

Mada kuu ni kujadili, kushauri na kutoa maoni juu ya miradi mikubwa ya kitaifa ya sekta ya nishati itakayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kipindi cha miaka mitatu, Julai 2013 – Disemba 2015 ili kuliwezesha Taifa kufikia Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

Kiambatanisho: Taarifa ya Uchambuzi na Mapendekezo ya Utekelezaji wa Miradi Yenye Lengo la Kuleta Matokeo Makubwa Sasa Kwa Wizara ya Nishati na Madini

Taarifa ya kimaabara inayoelezea kwa kina uchambuzi wa miradi ya kipaumbele ya nishati iliyotokana na upembuzi wa kimaabara uliofanyika kwa kipindi cha wiki sita (6), kuanzia tarehe 22 Februari hadi tarehe 5 Aprili 2013. Utekelezaji wa miradi hii unaanza rasmi tarehe 1 Julai 2013 na wizara ina jukumu la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi hii kama ilivyopangwa pamoja na kutatua matatizo yote yanayoweza kukwamisha utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika mapema zaidi. Miradi hiyo yote inapaswa kukamilika utekelezwaji wake ifikapo mwezi Juni, 2016.

Wadau Wanaoalikwa

Mabenki washirika, Wakandarasi kwenye sekta ya Umeme, Wahandisi kutoka Taasisi na Vyuo Vikuu nchini, Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Wawakilishi kutoka Makampuni mbalimbali, Migodi, Viwanda vikubwa na vidogo na wananchi wote kwa ujumla. KAULI MBIU "Matokeo Makubwa sasa kwa Maendeleo ya Mtanzania"

Kiingilio

Kiingilio ni bure ni bure, wote mnakaribishwa.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini
754/33, Mtaa wa Samora
S. L. P. 2000
Dar es Salaam, Tanzania
info@mem.go.tz
www.mem.go.tz
 
Kidogo kidogo wataikubali tu hadi sasa inaonekana kuna wizara Mbili, Moja ni hii na ya pili ni ile ya Profesori Mama Tiba, japo tangu aweke il thread hajawahi kuonekana tena, ile ya China
 
Wala Rushwa hawawezi kupata big results hata wafanyaje acheni kupoteza muda takaseni nafsi zenu kwanza muwe na mioyo ya kizalendo mkishatambua kuwa mmepewa dhamana ya rasilimali ya nchi yetu kwa ajili ya watanzania wote na watanzania wa Miaka 50 hadi 100 ijayo wala hamtahitaji mikutano na makongamano kupata big results uadilifu peke yake unatosha kuleta big results mmeshawekewa hela Uswis na makampuni ya madini na Gesi halafu mnatukejeli hapo Mlimani City ndo nini sasa?
 
Ego won't get you anywhere... Kwa nini usiende afu uwaambie hayo? Jiulize wewe mwenyewe hapo una uzalendo kiasi gani?
 
It's more than ten years now tangu waanze kuambiwa wamebadilika? Au mpaka niwaambie mimi? Mimi ni mzalendo unataka kupima uzalendo wangu kwa kipimo gani? Atleast na comply na Tax regulations nalipa kodi zote zinazonihusu ipasavyo na sijawahi kuiba hela ya serikali that is the least I can do and make noise
 
walianza na, ARI MPYA, NGUVU MPYA na KASI MPYA; halafu tukaambiwa, ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI; wanamalizia na; MATOKEO MAKUBWA.

Hayo matokeo makubwa yanatokana na nini hasa, ama ndiyo mwendelezo wa kuibuka na vibwagizo vipya kila mara kama walivyozoea
 
Ego won't get you anywhere... Kwa nini usiende afu uwaambie hayo? Jiulize wewe mwenyewe hapo una uzalendo kiasi gani?

Hata hapa hapa ujumbe unawafikia, wewe unadhani ni kwanini wameamua kuja kututangazia hapa kama hawajui impact ya JF? Tata Sabayi kudos kwa kuwaambia ukweli bila kupepesa macho, usisshangae kukuta huyu anayejiita DMussa ni fisadi aliyeko wizara ya nishati na ujumbe wako umemchoma.
 
Last edited by a moderator:
Big Results now? Real? We needed big results "yesterday" people. Get real my leaders!! And stop politicizing. Results are not born from big words and catching phrases!! When Big results happen every mwananchi will see.

Halafu mbaya zaidi Big Results inatakiwa ionekane ndani ya miaka 3 . Yaani 2013-2015!!! Inalenga palepale kwenye uchaguzi mkuu. If this does not smell politics, I must go see my Doctor for something is terribly wrong with my sense of smell!! Tena kazi ya kupata big results imefanyika kwa wiki sita tu!! What an amazing laboratory work eeh? Get serious people.

Hivi kweli kazi ya BIG RESULTS inafanywa kwa wiki sita? Yaani mipango mikubwa ya miaka labda tuseme 100 au 200 ijayo inafanywa kwa wiki sita. Can any help me define what is zoo and zoo keeper? Please hurry!!
 
Hata hapa hapa ujumbe unawafikia, wewe unadhani ni kwanini wameamua kuja kututangazia hapa kama hawajui impact ya JF? Tata Sabayi kudos kwa kuwaambia ukweli bila kupepesa macho, usisshangae kukuta huyu anayejiita DMussa ni fisadi aliyeko wizara ya nishati na ujumbe wako umemchoma.
Real funny! Kwa hiyo kila asiyekubaliana na mawazo/fikra zenu lazma mumtafutie jina? I like your attitude but unfortunately this won't get us anywhere. Lets all have free and open minds that way we can at least agree to disagree without breaking our peace. Pole maana naona hata baba yako akiwaza tofauti na wewe najua utampa jina hehe
 
Last edited by a moderator:
Wekeni hapa na mikata yote pamoja na business plans za hiyo miradi, report za kimaabara za nini?
 
Ego won't get you anywhere... Kwa nini usiende afu uwaambie hayo? Jiulize wewe mwenyewe hapo una uzalendo kiasi gani?

Hawa wamekwishatuthibitishia kwamba sio wasikivu na ni wahuni, wameshindwa kufanya mijadara ya tija bungeni alafu wanataka kuleta mjadala vijiweni ili kutupumbaza. I will be there kuwachana though.
 
Great thinker you are!! Salute...
 
Real funny! Kwa hiyo kila asiyekubaliana na mawazo/fikra zenu lazma mumtafutie jina? I like your attitude but unfortunately this won't get us anywhere. Lets all have free and open minds that way we can at least agree to disagree without breaking our peace. Pole maana naona hata baba yako akiwaza tofauti na wewe najua utampa jina hehe

Tunacho chombo chenye nguvu za kisheria katika kujadiri mambo kama haya kwa uwazi (BUNGE) and we pay some people alot of money so that they can engage themselves in discussions and critical considerations of all these issues, surprisingly these issues are not tabled there, and when they are tabled we always observe how they are being politicied and reduced to fights of mere words.

why do they want to table this in unorganized an unauthoritative forums?
 
Great thinker you are!! Salute...

DMussa, wapi hivyo viambatanisho, au mnataka mje kutupatia hapo hapo uwanjani, wekeni hapa mapema tuvipitie, tuvijadili na kuvikiria kabla ya kuja kuwaeleza tunaona nini ndani yake.
 
Back
Top Bottom