Kwanza mkae mkijua meneja hamfanyi msanii kuwa bora, msanii mwenyewe juhudi zake humfanya kuwa bora na duniani hamna meneja anayependa kufanya biashara isiyo na faida, hv leo kuanguka kwa Bob Valentino na Chingy utamlaum Ludacris eti,kwa hiyo usimlaumu babutale kwakufeli kwa MB dog, PNC nk. Acheni ujinga ktk maisha hamna kitu kizuri kama kujitambua unataka nini, diamond platnumz anajua anataka nini na mkae mkijua diamond platnumz alikuwa anatoza ela ndefu hata kabla ya kuwa chini ya babutale wala sallam, kwa hata ilo dau naamini diamond ndiye aliyeliweka. Hata darasani Kuna kuwa na wanafunzi wengi lakini Kuna mmoja lazima atakuwa na uwezo wapekee, kwani wote hawawezi kuwa sawa, huwezi kofosi diamond awe sawa na yamotto, chege, temba nk, kwani kila mtu ana uwezo wake. Diamond kabla ya kuwa na babutale pamoja na sallam, alikuwa chini ya papaa misifa, Raquel badae ndio akawaomba babutale na sallam wammeneji. Kuhusu mameneja kumkimbia, mimi si shangai, kama biashara hamna kila mtu akafanye shughuli nyingine na ndio maana diamond anatoza ela ndefu , anajua siku akidondoka tayari kashapiga ela anakaa pembeni anaangalia vitega uchumi vyake. Wabongo mna maneno mengi hebu niambieni hao wasanii wengine ambao wana mameneja, je wataendelea kuwa meneji milele na milele, siku zote za maisha yao, naomba kama yupo meneja ambaye ata meneji wasanii milele bila kuangalia kama anapata faida (juma nature alikuwa chini ya P Funk, je leo nature yupo chini ya P Funk), kama yupo huyo meneja, atakae mmeneji msanii siku zote, nitajieni huyo meneja na msanii wake. Mwacheni dogo apige ela ndio muda wake huu na yy Shigongo ache kuponda wenzake baada ya kuona kitumbua chake kimeingia mchanganyiko, kama anataka faida kubwa atoe ela kubwa ili apate faida kubwa. Alafu nae Shigongo nimegundua hana busara, jana ktk kipindi cha SHILAWADU, alikuwa anamtishia babutale kwa kumtangazia vita, sasa yote ya nini au anajiona yy kwasababu anamiliki magazeti, anajua atayatumia (manake waandishi wahabari wengi wanatekeleza matakwa ya maboss wao) ili kumchafua diamond platnumz atakavyo, aache tabia zake kama za mkuu wa mkoa .